Wizara ya Mifugo na Uvuvi2026-03-162026-03-162025https://www.mkulima.sua.ac.tz/handle/123456789/969JaridaMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewataka viongozi wa sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha chakula katika ukanda wa Afrika. Mhe. Dkt. Mpango amesema hayo wakati wa hotuba yake ya Ufunguzi wa Maonesho ya kimataifa ya Nane Nane aliyoitoa Agosti 1, 2025 kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ambapo amesisitiza Viongozi hao kuwa kinara kwenye utekelezaji wa dira ya Taifa Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025-2050. Aidha Dkt. Mpango amewataka wafugaji kuwekeza katika uzalishaji wa kisasa wa bidhaa zinazotokana na mifugo ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje, kuendeleza uvuvi na ufugaji wa samaki na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwenye miundombinu baridi ya uhifadhi na usafirishaji wa mazao wa Mifugo na Uvuvi.otherMifugoUvuviMaonesho -nane naneJaridaJarida maalum la nane nane 2025Other