Wyss, Eric2018-02-232018-02-232009http://10.10.11.5/handle/123/114Kwa mtazamo wa kiekolojia, viumbe wote ni sehemu ya mfumo asilia bila kujali vinafanya nini. Kwa mkulima, viumbe vyote ambavyo hupunguza mavuno ya mazao yake huchukuliwa kuwa ni wadudu waharibifu, magonjwa au magugu. Wadudu, ndege au wanyama wengine pia ni waharibifu wakati wanapo sababisha uharibifu kwa mimea au mazao yaliyohifadhiwa ghalani. Fangasi, bakteria na virusi pia hutambulika kama vijidudu vinavyosababisha magonjwa wakati vinapoingilia au kubadilisha michakato muhimu kwenye mmea unaokua au mavuno yaliyohifadhiwa. Mimea yote isiyotakiwa ambayo hustawi ndani ya shamba pamoja na mazao na kushindania virutubisho, maji na mwanga huchukuliwa kuwa ni magugu. Mimea ya namna hii pia ndio inaweza kuwa hifadhi kwa wadudu/wanyama waharibifu na magonjwa. Kuwepo kwa viumbe hivi katika mashamba ya mazao sio tatizo mpaka pale idadi yao inapoongezeka kupita kiwango ambacho wanaposhambulia husababisha kupungua kwa kiasi kikubwa wingi wa mavuno na ubora wa mavuno na mazao yaliyohifadhiwa. Wakulima wanaosubiri hadi wakati huu, mara nyingi hutegemea kutumia njia ambazo zina athari na uharibifu mkubwa ili kudhibiti uharibifu kwa mazao. Hata hivyo, kwa vile wakulima wengi wadogo wa Kiafrika hawawezi kupata au kumudu njia na bidhaa za kufanya hivyo, matokeo yake ni hasara kubwa kwenye mavuno na ubora wa mazao. Kwa ujumla, changamoto zinazo ambatana na udhibiti wa wadudu, magonjwa na magugu zinaweza kufafanuliwa kwa muhtasari kama ifuatavyo;otherKilimo haiKilimo nadhifuWaduduMagonjwaMaguguWadudu,magonjwa na maguguBook