Ghala la Taarifa na machapisho ya kilimo
Ghala hili,limebeba machapisho na taarifa mbalimbali za kilimo zilizo rahisishwa kwa matumizi ya wakulima, wafugaji, wavuvi, maafisa ugani na wadau wengine wa kilimo.

Recent Submissions
Hatua 10 za kuanzisha bustani ya nyumbani
(Zomboko, 2014-05) Zomboko, Zomboko
Baadhi ya umuhimu wa bustani ya nyumbani ni pamoja na:
1. Kupata hewa safi na ya asili
2. Kupata sehemu nzuri ya kupumzikia nje ya nyumba.
3. Kupendezesha muonekano wa nje wa nyumba yako.
4. Kupangilia na kuainisha matumizi ya ardhi ya nje.
Jinsi ya kulima mgagani: kilimo bora cha mgagani
(Melkisedeki, 1998) Melkisedeki, Melkisedeki
Migagani, migange, mikabili au miangani ni mimea ya jenasi Cleome katika familia na oda Brassicales (kabichi). Mgagani (Cleome gynandra) au Spider plant kwa kingereza, ni mmea wa asili ya Afrika unaostawi vizuri kwa kumwagiliwa hapa afrika ya mashariki wakati wa joto. Pia huchumwa mashambani ikiwa imeota yenyewe zao hili hushambiliwa na magonjwa na wadudu mara chache. Majani na Matawi machanga yana virutubisho kuliko Sukuma wiki na kabichi. Mahitaji yake yanaongezeka kwenye miji midogo na mikubwa kila siku.
Mgagani wa kawaida, huliwa takriban kila mahali pa Afrika na katika mabara mengine pia. Wanawake wengi wenye mimba au waliozaa hula mmea huu, kwa sababu una chuma nyingi kiasi na husaidia kuongeza damu. Mboga ya mgagani huitwa magagani.
Kilimo Bila Udongo
(Globalpublishers.co.tz, 2020-01) Globalpublishers, Globalpublishers
kilimo Bila Udongo,katika teknolojia hii, kinachofanyika ni kujua ili mmea uweze kumea, kukua na kutoa mazao, huwa unahitaji virutubisho na madini gani katika ardhi? Ukishajua mahitaji hayo, basi zinatafutwa kemikali zenye virutubisho vinavyotakiwa, zinachanganywa kwenye maji na kuwekwa kwenye mabomba maalum ambayo kwa juu, huwa yana matundu maalum ambapo ndipo mmea unaotakiwa kulimwa,/huwekwa.
Ijue Faida Ya Kula Magimbi Kiafya Muungwana Blog ,2018
(Muungwana Blog, 2018) Muungwana Blog
Magimbi ni kinga na pia ni tiba kama ambavyo nitakueleza leo faida za magimbi.
Kilimo cha Nyanya Chungu
(Mjasiriamali Hodari, 2018-02)
Nyanya chungu ni zao jamii ya mbogamboga linalotumika kwa matumizi mengi kama mboga, dawa n.k. Zao hili hustawi maeneo yenye halijoto tofauti tofauti nchini Tanzania.