Ghala la Taarifa na machapisho ya kilimo
Ghala hili,limebeba machapisho na taarifa mbalimbali za kilimo zilizo rahisishwa kwa matumizi ya wakulima, wafugaji, wavuvi, maafisa ugani na wadau wengine wa kilimo.

Recent Submissions
Utayarishaji wa mboga za majani
(Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA ), 2015) Kinabo J. L.; Msuya J.M.; Mnkeni A.P.; Nyaruhucha C.; Ishengoma J.
Mboga za majani zinashika nafasi muhimu
sana katika vyakula vyetu. Zinaliwa kila siku
na mara nyingi zaidi ya mara moja kwa
siku. Zipo aina nyingi za mboga za majani,
nyingine zinalimwa na nyingine zinaota
zenyewe porini na mashambani wakati wa
msimu wa mvua. Mboga zina virutubishi
kama madini na vitamini ambavyo
vinahitajika mwilini kwa afya bora. Hata
hivyo pamoja na kwamba zina virutubishi
vya kutosha na zinaliwa kila siku, watu
wengi wanapata matatizo ya afya
yanayotokana na ukosefu wa
virutubishi
vinavyopatikana katika mboga za majani
kwa mfano upofu na upungufu wa damu.
Hali hii inajitokeza kwa sababu gani?
Kiliko cha Pilipili Mtama
(Wizara ya kilimo na Chakula, Tanzania, 2022) Sehemu ya Uinuaji Mazao, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Pilipili mtama ni zao ambalo asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar. Matumizi Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki na kwa mapishi mengine mbalimbali
Utayarishaji wa mboga za majani
(Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), 2015) Kinabo J. L; Msuya J.M; Mnkeni A.P; Nyaruhucha .C; Ishengoma .J
Utangulizi
Mboga za majani zinashika nafasi muhimu
sana katika vyakula vyetu. Zinaliwa kila siku
na mara nyingi zaidi ya mara moja kwa
siku. Zipo aina nyingi za mboga za majani,
nyingine zinalimwa na nyingine zinaota
zenyewe porini na mashambani wakati wa
msimu wa mvua. Mboga zina virutubishi
kama madini na vitamini ambavyo
vinahitajika mwilini kwa afya bora. Hata
hivyo pamoja na kwamba zina virutubishi
vya kutosha na zinaliwa kila siku, watu
wengi wanapata matatizo ya afya
yanayotokana na ukosefu wa
virutubishi
vinavyopatikana katika mboga za majani
kwa mfano upofu na upungufu wa damu.
Hali hii inajitokeza kwa sababu gani?
Uhakika wa Chakula Katika Kaya
(Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, 2001) Kinabo J. L.
Uhakika wa chakula unamaanisha kuwepo kwa
chakula cha kutosheleza mahitaji ya jamii nzima kwa
muda wote kwa ajili ya afya bora. Kaya ambayo hai-
wezi kutimiza mahitaji yake ya chakula kwa kipindi
cha mwaka mzima haina uhakika wa chakula. Kaya
hiyo inatambulika kuwa ina tatizo sugu la uhakika wa
chakula. Mara nyingi kaya hizo huwa ni maskini
kupindukia na hasa wale wasio na ardhi au kitega
uchumi chochote. Tatizo la muda mfupi wa uhakika
wa chakula ni lile ambalo kaya ina uwezo wa kupata
chakula kwa kipindi kifupi tu cha mwaka.
Zao la iliki
(Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), 2022) TARI
Utangulizi
Iliki ni moja kati ya mazao ambayo yanatumika sana
karibia kila siku kwenye matumizi ya nyumbani,
hutumika kama viungo kwenye chai, chakula na pia
kama tiba ya magonjwa mbalimbali