Browsing by Author "Bakari, A"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Athari za Uharibifu wa Mazingira Katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya - Warsha ya Saba ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki lIiyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003(TARP II-SUA Project, 2004) Bakari, A; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway. . Chapisho hili Iinawasilisha mwenendo wa Warsha ya saba ya Wakulima wa Mikoa ya Kanda ya Mashariki kuhusu Athari za Uharibifu wa Mazingira katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya iliyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano kati ya wakulima, watafiti na wataalamu wa ugani ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na wataalamu wa ugani ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo na ufugaji 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo na mifugo.Item Warsha ya Tatu ya Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Kuhusu Mahusiano Baina ya Wakulima na Wafugaji Iliyofanyika Mjini Songea Tarehe 26 - 29 Novemba 2001(TARP II-SUA Project, 2002) Bakari, AChapisho hili linawasilisha Mwenendo wa Warsha ya Tatu ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki kuhusu uimarishaji wa mahusiano yaliyopo baina ya wakulima wa mazao na wafugaji. Warsha ilifanyikakatika Kituo cha Don Bosco Mjini Songea tarehe 26 hadi 29 Novemba 2001. Warsha hii ni moja ya warsha ambazo zimepangwa kufanyika kama shughuli muhimu za kuutekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD), na unatekelezwa na Chuo Kikuu eha Sokoine eha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo. Warsha hizi zina madhumuni yafuatayo: I. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo na washika dau wengine ill kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikishakilimo. 2. Kuchambuana kuainishamatatizo yanayowakabillwakulima wadogowadogo. 3. Kudadisi illkutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi. 4. Kushirikikatika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Kamati ya Utekelezaji wa Mradi inatarajia kuwa chapisho hili litakuwa la manufaa kwa wadau mbalimbali, na mapendekezo yaliyotolewa na washiriki wa warsha yatachangia katikajuhudi za kuimarisha uhakika wa chakula nchini.