Ghala la Taarifa na machapisho ya kilimo
Ghala hili,limebeba machapisho na taarifa mbalimbali za kilimo zilizo rahisishwa kwa matumizi ya wakulima, wafugaji, wavuvi, maafisa ugani na wadau wengine wa kilimo.

Recent Submissions
Four Orange - Fleshed Sweetpotato (OFSP) - Vines of Gold (Capacity Development for Impact)
(International Potato Center (CIP), 2024) IITA
Orange-fleshed sweetpotato (OFSP) vine multiplication in Hindi village, Bahi District, Dodoma Region, Tanzania, demonstrates the potential of irrigation and farmer training to support agricultural production in semi-arid environments. Despite limited rainfall, committed OFSP growers utilize water from wells supported by the high water table associated with nearby Lake Manyara to sustain productive vine multiplication fields. This initiative highlights the role of capacity building in strengthening farmers’ technical skills and promoting sustainable sweetpotato production. In December 2015, Julius Kayongola, a farmer from Hindi village, participated in an OFSP seed production and multiplication training course organized by the Sugar Research Institute (SRI-Kibaha), Tanzania, with funding from the Food and Agriculture Organization (FAO). His experience illustrates how targeted training, access to irrigation water, and farmer commitment can contribute to the development of OFSP vine multiplication and root production in semi-arid areas. The experience offers valuable insights for agricultural extension services, researchers, and development practitioners seeking to improve the availability of quality planting materials and strengthen climate-resilient food production systems.
Nini maana ya mifumo ya chakula ?
(The Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN), 2021) The Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN)
Mifumo ya Chakula ni watu, maeneo na shughuli ambazo hutupatia chakula. Huwezesha uwepo wa chakula kwa njia nyingi tofauti ambazo hushawishi na kuchagiza maamuzi tunayofanya kuhusu kinacholiwa, kwa wakati upi na namna gani. Mifumo hii ina mchanganyiko wa mambo mengi na hubadilika mara kwa mara -inajumuisha masuala mtambuka na yaliyochangamana na husaidia watu wengi kupata riziki zao. Mifumo ya chakula hujumuisha minyororo ya ugavi wa chakula, mazingira ya chakula na tabia za watumiaji au walaji. Hutegemea vigezo mbalimbali vikiwemo uchumi, utamaduni, teknolojia, na demografia, pamoja na maamuzi na shughuli nyingine za kitaasisi.Mifumo yetu ya chakula kwa maana ya tunakula nini, kwa namna gani na kinatoka wapi, kwa kiasi kikubwa inaamua uwezo wetu wa kufanikisha malengo ya kidunia kwa ajili ya ustawi wa binadamu na sayari yetu nzima. Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yakiwemo kutokomeza umasikini, kutokomeza njaa, afya bora na ustawi, na ulaji na uzalishaji makini yanahusiana moja kwa moja na chakula. Mifumo ya chakula ipo katika kiini cha changamoto nyingi ambazo zinatukabili hivi sasa, zikiwemo afya duni inayochochewa na lishe duni na uharibifu wa mazingira. Theluthi tatu ya dunia inakabiliwa na njaa au lishe duni, zaidi ya nusu ya mzigo wa magonjwa duniani husababishwa na lishe duni, na mifumo ya chakula inachangia uzalishaji wa robo ya gesi ya ukaa duniani. Mifumo ya chakula ipo pia kwenye kiini cha ufumbuzi wa matatizo mengi. Mifumo hiyo hulisha mamilioni ya watu zaidi leo kuliko wakati wote ule. Inaweza sasa kutoa chakula chenye lishe bora zaidi, riziki kubwa zaidi kwa wafanyakazi katika sekta hii, na kurutubisha sayari yetu kwa usalama.
Ijue TFRA
(TFRA, 2024) Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania - TFRA
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ni Mamlaka ya Serikali chini ya Wizara ya Kilimo iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mbolea Na. 9 ya Mwaka 2009 kwa lengo la kudhibiti uzalishaji, uingizaji, usafirishaji na usambazaji wa mbolea nchini ili kuongeza tija ya kilimo na usalama wa chakula.
Kilimo hai mboji ya udongo
(Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM), 2023) Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM)
Mboji ni muhimu kwa uwezo wa udongo kutunza virutubisho na kuvitoa kwa mimea inapohitaji .Kitu chochote chenye asili ya mmea au mnyama kinapowekwa ardhini huoza na kugeuka kwa kiasi fulani kuwa udongo au mboji. Katika mazingira asilia kiasi cha mboji kilichoko kwenye udongo .Hali ya hewa ya joto na yenye fukuto huongeza kuoza kwa vitu hivi.Lakini hali hiyo ya hewa huleta mabadiliko kwenye muundo wa mboji (na kuchukua sifa za madini). Shughuli za utifuaji wa ardhi pia huharakisha mchakato huu kwani huongeza kiasi cha hewa ya oksijeni kwenye udongo. Kwahiyo kuongeza mboji na kupunguza utifuaji wa ardhi zinahitajika ili kuendeleza viwango vinavyostahili vya mboji kwenye udongo.
Kanuni bora za kilimo endelevu cha Miwa
(TARI, 2024) National Sugar Institute
Miwa ya sukari ni zao muhimu la biashara nchini Tanzania, wastani wa uzalishaji wa miwa kwa wakulima wadogo wanaotegemea mvua ni kati ya tani 70-80 kwa hekta. Katika jitihada za kuwawezesha wakulima kuongeza kipato, kupunguza umasikini na kuinua uchumi; Shirika la kimataifa la uhifadhi wa asili na mazingira (IUCN) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Kibaha, Chuo cha Sukari cha Taifa (NSI), Kampuni ya Sukari Kilombero (KSCL) na Halmashauri ya Mji Ifakara wameandaa mikakati ya kuwaelimisha wakulima ili kuongeza tija kwa kufuata kanuni bora za kilimo cha miwa.