Browsing by Author "Laswai, H. S"
Now showing 1 - 3 of 3
Results Per Page
Sort Options
Item Kilimo bora cha nyanya(SUA-NORAD FOCAL PROGRAMME, 2005-08) Ishengoma, R. C; Mvena, Z. S. K; Tiisekwa, B; Laswai, H. S; Reuben, S. O. W. M; Nchimbi - Msolla, S; Maerere, A. P; Njau, P. J. RUtafiti huu unahusika na kuboresha uzalishaji, usindikaji na upatikanaji wa masoko ya nyanya Tanzania, ikichukulia wilaya mbili kama kielelezo. Wilaya hizo ni Kisarawe tarafa ya Maneromango na Msanga na Morogoro vijijini, tarafa ya Mikese. Utafiti huu shirikishi unafanyika kati ya wakulima, watalaamu kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Morogoro na wagani wa Kilimo kutoka wilaya zilizotajwa. Kijarida hiki kimeandaliwa ili kitumike katika kueneza mbinu mbalimbali zinazohusika na uzalishaji wa nyanya shambani. Mbinu hizi ni pamoja na kuchagua aina nzuri ya nyanya, matayarisho ya kitalu, utunzaji wa nyanya shambani na hatimaye uvunaji. Ni matumaini yetu kuwa kijarida hiki kitakuwa cha manufaa siyo tu kwa wakulima wadodgo wadogo wa nyanya bali pia kwa wadau wote wa nyanya.Item Kilimo bora cha nyanya - Uzalishaji, Usindikaji na Upatikanaji Masoko ya Nyanya unaotilia Mkazo Kupunguza Umasikini Kwa Wakulima Wadogo wadogo(FOCAL - SUA, 2005-08) Ishengoma, C. G; Mvena, Z. S. K; Tiisekwa, B; Laswai, H. S; Reuben, S. O. W. M; Nchimbi - Msolla, S; Maerere, A. P; Ashimogo, G; Njau, P. J. RUtafiti huu unahusika na kuboresha uzalishaji, usindikaji na upatikanaji wa masoko ya nyanya Tanzania, ikichukulia wilaya mbili kama kielelezo. Wilaya hizo ni Kisarawe tarafa ya Maneromango na Msanga na Morogoro vijijini, tarafa ya Mikese. Utafiti huu shirikishi unafanyika kati ya wakulima, watalaamu kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Morogoro na wagani wa Kilimo kutoka wilaya zilizotajwa. Kijarida hiki kimeandaliwa ili kitumike katika kueneza mbinu mbalimbali zinazohusika na uzalishaji wa nyanya shambani. Mbinu hizi ni pamoja na kuchagua aina nzuri ya nyanya, matayarisho ya kitalu, utunzaji wa nyanya shambani na hatimaye uvunaji.Item Soya kwa lishe bora: Virutubishi na matayarisho yake kwa mapishi mbalimbali(FOCAL - SUA, 2005-06) Laswai, H. S; Kulwa, K. B. M; Ballegu, W. R .W; Silayo, V. C. K; Ishengoma, C. G; Makindara, J. A; Mpagalile, J. J; Rweyemamu, C. LKatika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, tatizo la utapiamlo limekuwa tatizo sugu. Kiwango cha wanaosumbuliwa na tatizo hili katika nchi yetu kama asilimia thelatini ya watu wote. Jambo hili si la kufumbia macho kwa maana nguvu kazi kubwa ya nchi inapotea. Tatizo hili pia linasababisha watoto wengi mashuleni kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao. Kwa mantiki hii maendeleo ya nchi yanafifia kiuchumi na kielimu pia. Kujikwamua katika tatizo hili sio jambo rahisi. Hata hivyo, tunaamini kuwa, bila hata msaada kutoka nje ya kaya, kaya nyingi zinao uwezo wa kujinasua nalo. Kikubwa ambacho wanakikosa ni taaluma katika kutumia baadhi ya malighafi waliyo nayo kiutaalamu kuwaondolea kero hii. Zao la soya limesaidia sehemu nyingi duniani kuondoa utapiamlo, lakini katika Tanzania zao la soya halijatumika kikamilifu kwa sababu za kukosa taaluma za namna ya kulisindika na pia mapishi mbali mbali yanayotokana nalo. Kijitabu hiki ni juhudi makusudi za wataalamu wachache walioguswa na hili tatizo na kuamua kuwasaidia wale wengi wasio na hiyo taaluma kutangaza na kuhamasisha kilimo cha soya sio tu kwa ajili ya kupunguza utapiamlo na hivyo kuboresha afya bali pia kutumia zao hili hili kupunguza au kuondoa umaskini katika kaya. Azma ya juhudi hizi ni kuona Tanzania nzima ikinufaika na hivyo kupunguza asilimia ya wenye utapiamlo na maskini katika taifa letu.