Browsing by Author "Mtega, Wullystan"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Masoko ya mazao ya kilimo(Sokoine university of A griculture, 2020-05-20) Mtega, WullystanMkulima anatakiwa kutafuta soko la mazao yake kabla hajaanza shughuli ya uzalishaji shambani. Ili kupata taarifa za kutosha, mkulima anashauriwa kufanya utafiti wa soko. Mkulima anaweza tumia njia kuu mbili: (i) kuandaa dodoso na kuwauliza wadau muhimu wa soko la zao alilozalisha na, (ii) kutembelea masoko ya mazao na kukusanya taarifa kwa njia ya kuona. Utafiti wa soko humwezesha mkulima kutoa maamuzi sahihi juu ya uuzaji wa mazao yake. Katika kuuza mazao, mkulima lazima azingatie sheria, kanuni na taratibu za nchi na soko husika. Pia, ni muhimu kuelewa namna nguvu ya soko inavyofanya kazi. Hii itamsaidia mkulima kujua lini ayapeleke mazao sokoni na hivyo kupata bei nzuri zaidiItem Upatikanaji na matumizi ya taarifa za kilimo.(Sokoine University of Agriculture, 2021-05-16) Mtega, WullystanShughuli za kilimo huhusisha uzalishaji wa kumbukumbu tofauti. Kumbukumbu hizo hutokana na malipo mbalimbali yafanywalo shambani na shughuli za uzalishaji shambani. Kumbukumbu za kifedha hurekodi gharama za uwekezaji za kudumu na gharama za uendeshaji wa miradi ya kilimo. Zile za uzalishaji hurekodi taarifa mbalimbali zisizohusu pesa ambazo hutokea shambani. Kumbukumbu zote hizi ni lazima zirekodiwe kwa usahihi na kwa wakati ili zisaidie katika kutoa maamuzi. Wakulima wanatakiwa kutunza taarifa ya matukio yote ya muhimu yahusuyo shughuli za kilimo zinazofanyika katika mashamba yao. Bila kutunza kumbukumbu za kilimo wakulima hujikuta wanaingia kwenye hasara zisizo za msingi.