Browsing by Author "TARP II SUA Project"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Kilimo cha mpunga(Chuo cha kilimo cha Sokoine., 2004-03) TARP II SUA ProjectZao la mpunga liliingizwa nchini Tanzania miaka mingi iliyopita na wafanya biashara wa kutoka Mashariki ya Kati na India. Katika ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika zao hili hulimwa kwa wingi nchini Madagascar na Tanzania inafuatia.Nchini Tanzania, zao la mpunga hulimwa katika mikoa yote na ni la pili kwa umuhimu wake kama zao la chakula baada ya mahindi. Asilimia 60% ya Watanzania waishio mijini hula wali, chakula kinachotokana na zao hili. Ingawa zao la mpunga huzalishwa kwa wingi nchini, kiwango cha mavuno yanayopatikana kwa ekari au hekta moja bado ni cha chini sana ukilinganisha na nchi nyingine zinazolima zao hili. Hii inatokana na wakulima wengi kutokuwa na elimu ya zao la mpunga na kutozingatia kanuni za kilimo bora cha zao hili.Item Kuku wa kienyeji(Chuo cha kilimo cha Sokoine, 2002-12) TARP II SUA ProjectWarsha iliandaliwa na Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania (TARP II SUA) unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoinc cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula pamoja na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo (NLH). Lcngo kuu la warsha lilikuwa ni kubaini sababu zinazofanya uzalishaji wa kuku wa kienyeji kutokidhi mahitaji ya soko na kubuni mbinu za kukabiliana nazo ili mkulima aweze kuongeza uzalishaji wa kuku wa kienyeji na anufaike na soko lililopo la kuku wa kienyeji. Warsha ilikuwa na madhumuni mahsusi yafuatayo ili kufanikisha lengo hilo.