Browsing by Author "TARP II-SUA Project"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Mwongozo wa magonjwa ya kuku vijijini(Sokoine university of agriculture, 2002) TARP II-SUA ProjectUtambuzi yakinifu wa magonjwa ya ndege wafugwao ni mgumu kupita ule wa magonjwa ya mifugo mengine. Hii ni kwa sababu dalili za ugonjwa kwa mnyama hai peke yake hazitoshi kusema ugonjwa usumbuao kwa hakika, hivyo uchunguzi wa mnyama aliyekufa ni muhimu sana katika kutoa uamuzi wa ugonjwa usumbuao kwa ndege wafugwao. Mara nyingi, dalili za mgonjwa hai na za yule aliyekufa kwa magonjwa ya ndege wafugwao huwa zinaoana. Pia kwa magonjwa mengi, kuna upungufu au kutokuwepo kabisa kwa ugunduzi yakinifu wa kuaminika, hivyo historia ya ugonjwa pamoja na kufuatilia kwenye kundi ni vitu muhimu katika uchunguzi wa ugonjwa. Pale popote inapowezekana, uchunguzi wa mnyama aliyekufa ufanywe kwenye zaidi ya mnyama mmoja toka kwenye kundi la waathirika na pia uchunguzi wa maabara ufanyike kwenye vipimo vilivyochukuliwa na kuhifadhiwa vyema.Kijitabu hiki cha magonjwa ya ndege wafugwao vijijini kinadhamiria kutoa taarifa za haraka na muhimu kwa magonjwa yaliyozoeleka kwa ndege wafugwao vijijini nchiniTanzania. Kimedhamiriwa kwa wasaidizi wa waganga wa mifugo wanaofanya kazi vijijini ambako kuna upungufu wa vitabu vya kusoma. Msisitizo umewekwa kwa magonjwa yaliyozoeleka ambayo yanaripotiwa mara kwa mara kwa kuku wanaotunzwa kwa ufugaji huria hapa Tanzania. Maelezo mengi yanahusu mfululizo wa magonjwa yaliyozoeleka yasababishwayo na virusi, bakteria, na ukosefu wa virutubisho mwilini.Item Pesti ya nyanya(TARP-Sua, 2003) TARP II-SUA ProjectNyanya ni moja ya mazao ya mbogamboga muhimu Tanzania hususan katika wilaya ya Muheza. Zao la nyanya humwongezea mkulima kipato na kuboresha lishe ya mlaji. Pamoja na faida zake hizi. zao la nyanya ni la msimu na linakabiliwa na matatizo mcngi likiwemo la kuharibika haraka mara tu baada ya kuvunwa. llali hii pia humlazimisha mkulima auze nyanya zake haraka na kwa bei ya chini ambayo humpunguzia kipato. Wakulima wa Muheza kama walivyo wakulima wa sehemu nyingine Tanzania hawasindiki nyanya zao kwa sababu hawana ujuzi huo. Kijitabu hiki kimetayarishwa ili kumsaidia mkulima au mtu yeyote mwingine kusindika pesti ya nyanya na kuhifadhi katika chupa kwa ajili ya matumizi ya baadaye.