Browsing by Author "Wizara ya Kilimo"
Now showing 1 - 6 of 6
Results Per Page
Sort Options
Item Kilimo cha Tungule(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2013-10) Wizara ya KilimoNdugu wakulima, kupata chakula cha kutosha na kilicho bora kwa kila mwananchi ni suala gumu ambalo linahitaji mipango na mikakati mizuri ya serikali kupitia Wizara husika. Matatizo makubwa yanayowakabili wananchi ni kuchelewa kukamilisha hatua za mwanzo za matayarisho ya mashamba, kulima eneo kubwa ambalo hawana uwezo nalo na kutokutumia njia za utaalamu pamoja na pembejeo bora za kilimo. Ndugu wakulima, moja ya kikwazo kikubwa ni uwezo mdogo wa kutumia zana bora za kilimo, mbegu bora, mbolea na kutozingatia kanuni na taaluma bora za uzalishaji ambazo zinatolewa na Wizara ya Kilimo na Maliasili. Vikwazo hivi humsababishia mkulima kutumia nguvu nyingi, muda mrefu na kupata mavuno hafifu na tija ndogo. Ndugu wakulima, kwa miaka mingi neno “Ukulima wa Kisasa” limekuwa ni wimbo lakini bado mkulima wa visiwani anategemea zana na pembejeo duni kama vile mbegu na jembe la mkono (kijembe kongoroka). Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili inafanya mabadiliko makubwa katika kilimo ili kukifanya kilimo hicho kiwe katika mfumo wa kisasa “Mapinduzi ya Kilimo”. Ndugu wakulima, katika kufanikisha suala hili Serikali imeongeza upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo yakiwemo matrekta makubwa na madogo, mbegu bora na mbolea, kuongeza usamabazaji wa taaluma kwa wakulima kwa kuongeza idadi ya mabwana/ mabibishamba katika shehia pamoja na kutoa ruzuku ya aslimia 75% kwa kazi za utayarishaji wa mashamba na ununuzi wa mbegu bora na mbolea. Ndugu wakulima, hatunabudi kuunga mkono juhudi hizi za Serikali ili kufanikisha azma ya “Mapinduzi ya Kilimo” hivyo tunaipongeza na tunaiomba iendelee na juhudi zake za kuwashajiisha na kuwashirikisha wakulima kikamilifu katika kupanga malengo yao juu ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini. Ndugu wakulima, kwa kuunga mkono juhudi hizi za Serikali, Wizara ya Kilimo na Maliasili itaendelea kutoa mafunzo ya utumiaji bora wa zana na pembejeo za kilimo na kuweka mipango maalumu ya mafunzo kwa kila shehia juu ya umuhimu wa zana hizo pamoja na matumizi yake ili kufikia lengo la wakulima katika kujitosheleza kwa chakula na kuimarisha afya za jamii pamoja na kuinua hali zao za maisha na kuipunguzia mzigo Serikali kwa kuagiza chakula kutoka nje ya nchiItem Maeneo ya Kilimo ya Unguja na Pemba(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2011-06) Wizara ya KilimoItem Mbegu bora zinazoweza kutupatia tija(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2011-07) Wizara ya KilimoNdugu wakulima, kupata chakula cha kutosha na kilicho bora kwa kila mwananchi ni suala gumu ambalo linahitaji mipango na mikakati mizuri ya serikali kupitia Wizara husika. Moja ya tatizo kubwa linalowakabili wananchi ni kuchelewa kukamilisha hatua za mwanzo za matayarisho ya mashamba, kulima eneo kubwa ambalo hawana uwezo nalo na kutokutumia zana na pembejeo bora za kilimo. Ndugu wakulima, moja ya kikwazo kikubwa ni uwezo mdogo wa kutumia zana bora za kilimo, mbegu bora, mbolea na kutozingatia kanuni na taaluma bora za uzalishaji ambazo zinatolewa na Wizara ya Kilimo na Maliasili. Vikwazo hivi humsababishia mkulima kutumia nguvu nyingi, muda mrefu na kupata mavuno hafifu na tija ndogo. Ndugu wakulima, kwa miaka mingi neno “Ukulima wa Kisasa” limekuwa ni wimbo lakini bado mkulima wa visiwani anategemea zana na pembejeo duni kama vile mbegu na jembe la mkono (kijembe kongoroka). Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili inafanya mabadiliko makubwa katika kilimo ili kukifanya kilimo hicho kiwe katika mfumo wa kisasa “Mapinduzi ya Kilimo”. Ndugu wakulima, katika kufanikisha suala hili Serikali imeongeza upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo yakiwemo matrekta makubwa na madogo, mbegu bora na mbolea, kuongeza usamabazaji wa taaluma kwa wakulima kwa kuongeza idadi ya mabwana/mabibishamba katika shehia pamoja na kutoa ruzuku ya aslimia 75% kwa kazi za utayarishaji wa mashamba na ununuzi wa mbegu bora na mbolea. Ndugu wakulima, hatunabudi kuunga mkono juhudi hizi za Serikali ili kufanikisha azma ya “Mapinduzi ya Kilimo” hivyo tunaipongeza na tunaiomba iendelee na juhudi zake za kuwashajiisha na kuwashirikisha wakulima kikamilifu katika kupanga malengo yao juu ya mpango wa utumiaji wa zana na pembejeo bora za kilimo. Ndugu wakulima, kwa kuunga mkono juhudi hizi za Serikali, Wizara ya Kilimo na Maliasili itaendelea kutoa mafunzo ya utumiaji bora wa zana na pembejeo za kilimo na kuweka mpango maalumu ya mafunzo kwa kila shehia juu ya umuhimu wa zana hizo pamoja na matumizi yake ili kufikia lengo la wakulima katika kujitosheleza kwa chakula, kuinua hali zao za maisha na kuipunguzia mzigo Serikali wa kuagiza chakula kutoka nje ya nchiItem Tathmini ya asali za kiangazi katika mabonde a mpunga(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2011-03) Wizara ya KilimoNdugu Wakulima; sote tunakubaliana kwamba kilimo cha umwagiliaji maji ndio mkombozi wetu kwa ukulima wa mpunga, umuhimu wake umezidi kuwa mkubwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa yanayotokea duniani kote, hali inayosababisha kilimo cha kutegemea mvua kutokuwa cha uhakika na cha matumaini. Hivyo, tunahitaji kujipanga vyema na kukiimarisha kilimo cha umwagiliaji maji ili tuwe na uhakika wa chakula na kupunguza uagizaji. Kwa mujibu wa Mpango Mkuu wa Umwagiliaji maji wa mwaka 2003, Zanzibar tunalo eneo la ekari 21,300 ambazo zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji maji. Hadi sasa eneo lililojengwa miundombinu ni ekari 1,750 sawa na asilimia 8% tu ya eneo lote. Eneo lililobaki lenye ukubwa wa ekari 19,550 kati ya hizo ekari 200 zimejengwa makinga maji, ekari zilizobaki 19,350 zinaendelea kutumika kwa uzalishaji wa mpunga wa kutegemea mvua. Ndugu Wakulima pamoja na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu, bado tunakabiliwa na changamoto za gharama kubwa za ujenzi wa miundombinu, ukarabati wa visima na pampu kutokana na teknolojia duni upungufu wa wataalamu na elimu ya uendeshaji wa jumuiya za wakulima na upungufu mkubwa wa mitaji, utegemezi mkubwa wa nishati ya umeme, uharibifu wa vianzio vya maji pamoja na ukosefu wa zana maalum za utayarishaji wa ardhi. Kutokana na changamoto hizo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya eneo linalofaa kwa umwagiliaji maji linalimwa kwa kutegemea mvua hali ambayo inapelekea uzalishaji na tija ndogo. Ndugu Wakulima, kwa kipindi cha miaka mitano ijayo 2011 – 2016 Wizara ya Kilimo na Maliasili imekusudia kuutekeleza kikamilifu Mpango Mkuu wa Umwagiliaji maji ambao unatarajiwa kutatua changamoto zote za kilimo hicho. Wizara imezungumza na Serikali ya Korea kupitia Benki ya EXIM – ambao wamekamilisha uhakiki wa eneo la ekari 5250 ambalo litajengwa mindombinu ya umwagiliaji maji. Serikali ya Japan na Benki ya BADEA pia wameonesha nia ya kutusaidia katika Kilimo cha umwagiliaji maji. Ndugu Wakulima, Wizara imekusudia kuendeleza ujenzi wa miundombinu na utunzaji wa vianzio vya maji ili sekta ya umwagiliaji maji ipate maendeleo endelevu na kuwawezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga. Kuzijengea uwezo Jumuiya za Wakulima wa umwagiliaji maji ziweze kushiriki kikamilifu katika uendeshaji na utunzaji wa miundombinu, uhifadhi wa vianzio vya maji na utoaji wa huduma za Kilimo. Wizara inaendelea kuwashajihisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kuchagua miradi ya kijamii ya umwagiliaji maji ikiwemo ujenzi wa miundombinu na makinga maji kila wanapopata fursa ya usaidizi wa Washirika wa Maendeleo. Ndugu Wakulima, napenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa wakulima wa mpunga wa umwagiliaji maji watumie mbegu bora na pembejeo zinazotolewa na Wizara ya Kilimo na Maliasili ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo na kuhakikisha kuwa miundombinu ya umwagiliaji maji iliyojengwa kwa gharama kubwa tunaitumia kikamilifu katika uzaalishaji wa zao hili.Item Umuhimu wa kushirikisha jamii katika uhifadhi wa maliasili za misitu(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2016-07) Wizara ya KilimoKabla ya jamii kushirikishwa katika uhifadhi wa maliasili misitu eneo la Jozani na ghuba ya chwaka, Ndugu Simai alieleza kwamba Serikali pekee ndio iliyokuwa ikilinda rasilimali hizo zilizozungukwa na vijiji tisa vyenye wakaazi wasiopungua 42, 000. Ilionekana kwamba mwananchi wa kawaida kama ni adui wa maliasili japokuwa ndio mwenye mahitaji makuu ya kutumia maliasili hizo kwa maisha ya kila siku. Mwananchi alijenga dhana kwamba maliasili za misitu ni za Serikali na wao hawana mamlaka ya kufaidika na hilo na kupelekea kuwepo na mvutano baina ya mwananchi na Serikali katika matumizi ya maliasili na kusababisha uharibifu katika matumizi. Baada ya Serikali kutanabahi kwamba haitamudu kazi ya uhifadhi kwa ufanisi, wakati uharibifu wa maliasili za misitu unaongezeka na mvutano baina ya Serikali na wananchi unaongezeka, Idara ya Misitu ilitoa wazo la kushirikisha jamii katika uhifadhi wa maliasili za misitu ili iwe na hisia kwamba rasilimali zilizowazunguka ni zao na wanahusika katika jukumu la uhifadhi. Mnamo mwaka 1996 likatolewa wazo la kuanzisha Kamati za Uhifadhi. Kamati saba za kusimamia matumizi ya maliasili zilianzishwa katika Shehia za Pete (Jozani), Unguja Ukuu, Cheju, Chwaka, Charawe, Ukongoroni na Bwejuu. Baadae iliundwa Kamati ya ushauri baina ya Idara ya Misitu na kuwashirikisha wajumbe wawili kutoka kila kamati ambapo kazi za uhifadhi zikiratibiwa na mradi wa kimataifa wa CARE. Kamati hiyo ya ushauri ilifanya kazi kwa pamoja ambapo Idara ilitoa wazo la kuundwa kwa Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira Jozani (JECA) kwa lengo la kuendelea na kazi za uhifadhi baada ya mradi wa CAREItem Utunzaji wa Miti(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2012-10) Wizara ya KilimoNdugu wakulima; sote tunaelewa kwamba ili kupata chakula kilicho bora na cha kutosha mbinu mchanganyiko na mikakati ya utumiaji mzuri wa mbolea unahitajika. Njia hii inamsaidia mkulima kurutubisha ardhi na kupata mazao mengi na yaliyo bora kutokana na matumizi ya mbolea za mboji, samadi za wanyama na za viwandani. Ndugu wakulima; mimea ni kama binadamu inahitaji lishe nzuri na ili mimea iwe yenye afya. Lishe hiyo hupatikana kwa matumizi bora ya mbolea hizo tulizozitaja na pindipo ikikosekana mimea hudumaa, majani huwa na rangi ya kijani kibichi kilicho fifia na kushindwa kutengeneza chakula ipasavyo hatimae mazao hupungua shambani. Ndugu wakulima; ili mavuno yaweze kuongezeka na kuwa bora wakulima wanapaswa kufuata kikamilifu kanuni za kilimo bora. Moja kati ya kanuni hizo ni matumizi ya mbolea yanayozingatia utumiaji, muda mzuri unaofaa kuweka mbolea na kufahamu mahitaji halisi pamoja na kiwango kinachohitajika kwa kila eneo pamoja na aina ya mbolea. Ndugu wakulima; matumizi ya mbolea hupelekea mimea kustawi kwa haraka na kuongeza mavuno mara dufu. Mbolea inapotumika vizuri mazao hupatikana kwa gharama ndogo ambapo uwezo wa asili wa udongo kutoa mazao kutegemea rutuba huwa mkubwa. Ndugu wakulima; ni vizuri tufahamu kuwa matumizi bora ya mbolea ni muhimu sana ambapo inaaminika kuwa matumizi ya hayo peke yake huongeza mazao kwa asilimia 50 kama takwimu zinavyoonesha na humsaidia mkulima kupata fedha za kulipia gharama nyingine zitakazotumika kwa kufuata kanuni za kilimo bora ikiwemo kutumia mbegu bora, madawa ya kuzuwia wadudu, magonjwa, kupanda kwa wakati kuongeza mazao kwa asilimia 50 iliyobakia. Ndugu wakulima; kwa kuzingatia matokeo muhimu ya uzalishaji matumizi ya mbolea yatapungua iwapo vipo vitu vyengine vitakavyopunguza mavuno ya mazao, kwa mfano magugu yanaokwamisha ukuaji mzuri wa mazao. Hivyo, faida ya matumizi ya mbolea hugeuka na kuwa hasara ikiwa mbolea hiyo itawekwa katika shamba lenye magugu, kwa sababu gugu likipata mbolea hupata nguvu na kufanya mimea kunyong’onyea. Ndugu wakulima; ili kufanikisha mpango wa taifa wa kujitosheleza kwa chakula Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili inaendeleza juhudi za kuwasaidia na kuwahamasisha wakulima wazidi kujitokeza kwa wingi katika kutumia mbolea