Browsing by Author "Kisanga, P."
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Maziwa ya mama(Shirika la Chakula na Lishe Tanzania, 1992-10-17) Kisanga, P.; Mella, O.; Masako, R.; Navetta, D.Kijitabu hiki cha maswali na majibu ni kimojatu kati ya vijitabu kumi vinavyotolewa aa Shirika la Chakula na Lishe Tanzania kutokana na barua za wasikilizaji wa vipindi vya redio vya "Chakula na Lishe". Vijitabu hivi ni: 1. Ujauzito 2. Maziwa ya Mama 3. Ulikizaji 4. Ukuaji wa mtoto 5. Kuharisha 6. Surua 7. Anemia 8. Upungufu wa Vitamini A· 9. Upungufu wa Madini ya joto 10. Muhogo Kila kijitabu kina maswali 10 tu na kijitabu kitakachofuaria katika fani moja kitaendeleza idadi ya maswali. Vijitabu hivi vinafaa sana kusomwa na wanafunziwa shule za msingi na sekondari na watu wote vijijini na mijini wanaopenda kuelewa zaidikuhusu Lishe bora. Mara kwa mara Shirika la Chakula na Lishe litatoa zoezi katika redio au gazeti la kiswahili kwa ajili ya watu wa vikundi mbali mbali na atakayepata alama nyingi atazawadiwa.Item Upungufu wa wekundu wa damu (Anaemia)(Shirika la Chakula na Lishe Tanzania, 1994-10-11) Maganga, S. J.; Kimboka, S.; Tatala, S.; Mduma, B.; Ballart, A.; Temalilwa, C. R.; Missano, H. M.; Kisanga, P.; Magalia, A. W.; Ng'wawasya, B. M.; Kayombo, J. K.; 5imonje, L. W.; Ndossi, G. D.; Rwebangira, C. G.; Kayombo, L. C.; Ntoga, B. A.Upungufu wa wekundu wa damu ni moja ya matatizo sugu ya utaptamlo yanayoathiri watu na kusababisha vito vingi hapa Tanzania. Kutokana na takwimu zilizopo Shirika la Chakula na Lishe Tanzania, inakadiriwa kuwa asilimia 32 ya watu milioni 23 (Sensa ya mwaka 1988) wanaathirika. Wanaoathirika zaidi ni wanawake wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa wanawake wajawazito wanaoathirika ni asilimia 80 na watoto chini ya umri wa miaka mitano ni asilimia 45. Tatizo la upungufu wa wekundu wa damu hutokana na sababu nyingi zikiwemo ulaji duni yaani kutokula chakula cha mchanganyiko na cha kutosheleza mahitaji ya mwili. Magonjwa mbalimbali hasa malaria na minyoo ni chanzo kimojawapo cha tatizo. Vile vile uzazi wa karibu karibu huchangia upungufu wa wekundu wa damu. Tatizo la upungufu wa wekundu wa damu hapa nchini limeenea zaidi sehemu ambazo magonjwa ya safura, malaria na kichocho hujitokeza kwa wingi. Kitabu hiki kina lengo la kuwaelimisha na kuwaongezea wataalam wa ugani na viongozi katika ngazi ya wilaya, kata na kijiji ujuzi, maarifa na uwezo wa kuelewa chanzo, dalili na athari za upungufu wa wekundu wa damu katika jamii. Maarifa haya yatawawezesha kuishirikisha jamii katika kuchunguza, na kupima ukubwa wa tatizo, kufanya uchambuzi wa kina wa tatizo na kubuni mbinu za kulitatua. Kitabu kina sura tano. Sura ya kwanza inazungumzia dhana ya utapiamlo na jinsi inavyotumika katika kuchanganua tatizo la upungufu wa wekundu wa damu. Sura ya pili inaelezea umuhimu wa madini ya chuma, vitamini aina ya folic acid na B12 katika mwili wa binadamu na madhara yatokanayo na upungufu wake. Sura ya tatu inaelezea dalili na athari za upungufu wa wekundu wa damu. Sura ya nne inaelezea mbinu za kukabili tatizo la upungufu wa wekundu wa damu na sura ya tano inaelezea majukumu na wajibu wa jamii katika ngazi mbalimbali