Browsing by Author "Mwatawala, M. W"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Uthibiti wa nzi waharibifu wa matunda: Mwongozo kwa wakulima na maafisa ugani(Kurugenzi ya Utafiti na Uzamili, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine - SUA, 2012) Mwatawala, M. W; Meyer, M. De; Seguni, Z; Rwegasira, G. M; Muganyizi, J; Senkondo, F; Sechambo, L; Shempemba, D; Kweka, EKilimo cha mboga na matunda ni mojawapo ya tasnia za kilimo inayokua kwa kasi hapa nchini kulinganisha na ilivyokuwa hapo awali. Kwa mfano, takwimu za uzalishaji wa matunda katika msimu wa 2008/2009 ni tani 1, 205,340.5 ikiwa ni ongezeko la asilimia 39.3 kutoka tani 865,540 za msimu wa 2002/ 2003. Halikadhalika, uzalishaji wa mboga nao umeongezeka japo hakuna takwimu sahihi za ongezeko hilo. Uzalishaji wa mboga na matunda licha ya kuongezeka unakabiliwa na changamoto nyingi kama ukosefu wa mitaji, uwezo mdogo wa kununua pembejeo, utaratibu mgumu wa kumiliki ardhi ambao hautoi nafasi kwa uwekezaji wa kudumu, uhaba wa wataalamu, ukosefu wa miundombinu, magonjwa na wadudu waharibifu, hasa nzi waharibifu wa matunda.