Uthibiti wa nzi waharibifu wa matunda: Mwongozo kwa wakulima na maafisa ugani
Loading...
Files
Date
2012
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kurugenzi ya Utafiti na Uzamili, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine - SUA
Abstract
Kilimo cha mboga na matunda ni mojawapo ya tasnia za kilimo inayokua kwa
kasi hapa nchini kulinganisha na ilivyokuwa hapo awali. Kwa mfano, takwimu
za uzalishaji wa matunda katika msimu wa 2008/2009 ni tani 1, 205,340.5 ikiwa
ni ongezeko la asilimia 39.3 kutoka tani 865,540 za msimu wa 2002/ 2003.
Halikadhalika, uzalishaji wa mboga nao umeongezeka japo hakuna takwimu
sahihi za ongezeko hilo. Uzalishaji wa mboga na matunda licha ya kuongezeka
unakabiliwa na changamoto nyingi kama ukosefu wa mitaji, uwezo mdogo wa
kununua pembejeo, utaratibu mgumu wa kumiliki ardhi ambao hautoi nafasi
kwa uwekezaji wa kudumu, uhaba wa wataalamu, ukosefu wa miundombinu,
magonjwa na wadudu waharibifu, hasa nzi waharibifu wa matunda.
Description
Keywords
Nzi, Matunda