Browsing by Author "Wambura, R. M"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Uboreshaji wa vikundi vya wakulima - Utafiti Juu ya Mbinu za Uboreshaji wa Vikundi vya Wakulima Chiniya Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo, Tanzania (TARP II-SUA Project)(TARP II-SUA Project, 2003-12) Wambura, R. M; Rutatora, D. F; Shetto, M; Ishumi, O; Oygard, RKilimo ndio tegemeo kubwa na ndicho kinachohusisha idadi kubwa ya watu nchini Tanzania. Hata hivyo matokeo yake bado hayajawa ya kuridhisha kutokana na ukweli kwamba wakulima walio wengi uwezo wao bado ni mdogo kiasi cha kilimo chao kushindwa kutosheleza hata mahitaji ya familia. Hali hii imekuwa ikiendelea kuwa duni kwani mahitaji ya kilimo yamekuwa yakipanda siku hadi siku na hivyo mkulima mmoja mmoja kushindwa kuboresha kilimo kutokana na matatizo mbalimbali kama vile ushauri na pembejeo. Aidha kwa upande mwingine kidogo ambacho wakulima wamekuwa wakikipata kutokana na mfumo mzima wa soko kimekuwa hakipati bei ya kutosha ukilinganisha na gharama ya uzalishaji. Moja ya mikakati inayotiliwa mkazo na serikali ni kuwafundisha wakulima kwamba ili kujikwamua wanahitajika kuunganisha nguvu na kujenga mitaji itakayowawezesha kuboresha kilimo na hatimaye hali yao ya maisha kwa ujumla. Kwa kuzingatia hali hii, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH) kinatekeleza mradi wa uhakika wa chakula na pato la kaya kwa wakulima wadogowadogo nchini Tanzania. Mradi wa uboreshaji wa vikundi vya wakulima chini ya mradi wa TARP II-SUA unaendeshwa katika Mkoa wa Morogoro. Kwa kuanzia, kuna vijiji vinne katika Wilaya za Mvomero (Mkindo na Lusanga) na Kilombero (Sonjo na Mbasa). Kijarida hiki kimeandikwa ili kitumike katika kueneza mbinu mbalimbali za mradi kuhusu uimarishaji wa vikundi vya wakulima ambavyo ni vyombo vya kiuchumi ambapo mtu anaweza kujiunga na wenzake ili aweze kujiendeleza zaidi kiuchumi na hata kijamii katika lengo zima la kuondoa umaskini. Mambo muhimu yanayozingatiwa katika vikundi vya wakulima ni pamoja na: nia ya kufanya jambo kwa pamoja; shughuli au tatizo linalolengwa katika kutatuliwa; na mafanikio yanayotarajiwa kutokana na nguvu za pamoja.Item Ukame: Athari na mbinu za kukabiliana - Warsha ya Kwanza ya Wakulima lliyofanyika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE), Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), MOROGORO Tarehe 23-27 Aprili 2006(PANTIL - SUA, 2006) Mwaseba, D. L; Matee, A. Z; Wambura, R. MShughuli za utafiti chini ya Programu ya Mageuzi ya Kilimo na Maliasili kwa Maisha Bora (PANTIL) zilianza rasmi mwanzoni mwa mwezi Januari 2006. Lengo la programu hii ambayo itatekelezwa kwa muda wa miaka minne (2005-2009) ni kuchangia ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini na kuboresha ustawi wa jamii kwa njia ya uboreshaji wa sekta za kilimo na mali asili. Programu hii inazo sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza inashughulikia utafiti na uwezeshaji wa wakulima; na sehemu ya pili inashughulikia mageuzi ya kitaasisi na kuboresha uwezo wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ili kiweze kutekeleza majukumu yake ya kitaaluma. Shughuli za uwezeshaji wa wakulima zina lengo la kuwaongezea uwezo wakulima ili waweze kudai elimu husika, teknolojia inayofaa, pamoja na habari ill kuboresha tija, faida na kuchangia katika kuongeza kipato na kupunguza umaskini. Baadhi ya shughuli kadhaa ambazo zitafanyika katika kipindi cha 2006 hadi 2009 ni kama zifuatazo: • Uimarishaji wa vyama/vikundi vilivyopo vya wakulima na uanzishaji wa vikundi vipya kupitia mafunzo ambayo yatahusu uanzishaji vikundi, uendeshaji wake, na uongozi. Shughuli hizi zitahusisha uongozi husika, wadau katika ugani zikiwemo asasi zinazofundisha maafisa ugani. • Kusaidia kuanzisha shule za wakulima katika vijiji na wilaya zitakazochaguliwa • Uchapishaji na usambazaji wa nyenzo za ugani kama vile vipeperushi, vijitabu, n.k. • Uimarishaji wa mbinu za wakulima ili waweze kushiriki katika kutoa mafunzo na usambazaji wa teknolojia mpya kwa wakulima wengine, na kuyafikia maeneo yaliyo nje ya programu ili yaweze kufaidika na programu