Uboreshaji wa vikundi vya wakulima - Utafiti Juu ya Mbinu za Uboreshaji wa Vikundi vya Wakulima Chiniya Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo, Tanzania (TARP II-SUA Project)
Loading...
Date
2003-12
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
TARP II-SUA Project
Abstract
Kilimo ndio tegemeo kubwa na ndicho kinachohusisha idadi kubwa
ya watu nchini Tanzania. Hata hivyo matokeo yake bado hayajawa ya
kuridhisha kutokana na ukweli kwamba wakulima walio wengi uwezo
wao bado ni mdogo kiasi cha kilimo chao kushindwa kutosheleza hata
mahitaji ya familia. Hali hii imekuwa ikiendelea kuwa duni kwani
mahitaji ya kilimo yamekuwa yakipanda siku hadi siku na hivyo
mkulima mmoja mmoja kushindwa kuboresha kilimo kutokana na
matatizo mbalimbali kama vile ushauri na pembejeo. Aidha kwa
upande mwingine kidogo ambacho wakulima wamekuwa wakikipata
kutokana na mfumo mzima wa soko kimekuwa hakipati bei ya kutosha
ukilinganisha na gharama ya uzalishaji.
Moja ya mikakati inayotiliwa mkazo na serikali ni kuwafundisha
wakulima kwamba ili kujikwamua wanahitajika kuunganisha nguvu
na kujenga mitaji itakayowawezesha kuboresha kilimo na hatimaye
hali yao ya maisha kwa ujumla. Kwa kuzingatia hali hii, Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo
na Chakula (MAFS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway
(NLH) kinatekeleza mradi wa uhakika wa chakula na pato la kaya kwa
wakulima wadogowadogo nchini Tanzania. Mradi wa uboreshaji wa
vikundi vya wakulima chini ya mradi wa TARP II-SUA unaendeshwa
katika Mkoa wa Morogoro. Kwa kuanzia, kuna vijiji vinne katika
Wilaya za Mvomero (Mkindo na Lusanga) na Kilombero (Sonjo na
Mbasa).
Kijarida hiki kimeandikwa ili kitumike katika kueneza mbinu
mbalimbali za mradi kuhusu uimarishaji wa vikundi vya wakulima
ambavyo ni vyombo vya kiuchumi ambapo mtu anaweza kujiunga na
wenzake ili aweze kujiendeleza zaidi kiuchumi na hata kijamii katika
lengo zima la kuondoa umaskini. Mambo muhimu yanayozingatiwa
katika vikundi vya wakulima ni pamoja na: nia ya kufanya jambo kwa
pamoja; shughuli au tatizo linalolengwa katika kutatuliwa; na
mafanikio yanayotarajiwa kutokana na nguvu za pamoja.
Description
Keywords
Vikundi, Ushirika, Wakulima