Mwongozo wa magonjwa ya kuku vijijini

dc.contributor.authorTARP II-SUA Project
dc.date.accessioned2023-09-19T11:28:06Z
dc.date.available2023-09-19T11:28:06Z
dc.date.issued2002
dc.description.abstractUtambuzi yakinifu wa magonjwa ya ndege wafugwao ni mgumu kupita ule wa magonjwa ya mifugo mengine. Hii ni kwa sababu dalili za ugonjwa kwa mnyama hai peke yake hazitoshi kusema ugonjwa usumbuao kwa hakika, hivyo uchunguzi wa mnyama aliyekufa ni muhimu sana katika kutoa uamuzi wa ugonjwa usumbuao kwa ndege wafugwao. Mara nyingi, dalili za mgonjwa hai na za yule aliyekufa kwa magonjwa ya ndege wafugwao huwa zinaoana. Pia kwa magonjwa mengi, kuna upungufu au kutokuwepo kabisa kwa ugunduzi yakinifu wa kuaminika, hivyo historia ya ugonjwa pamoja na kufuatilia kwenye kundi ni vitu muhimu katika uchunguzi wa ugonjwa. Pale popote inapowezekana, uchunguzi wa mnyama aliyekufa ufanywe kwenye zaidi ya mnyama mmoja toka kwenye kundi la waathirika na pia uchunguzi wa maabara ufanyike kwenye vipimo vilivyochukuliwa na kuhifadhiwa vyema.Kijitabu hiki cha magonjwa ya ndege wafugwao vijijini kinadhamiria kutoa taarifa za haraka na muhimu kwa magonjwa yaliyozoeleka kwa ndege wafugwao vijijini nchiniTanzania. Kimedhamiriwa kwa wasaidizi wa waganga wa mifugo wanaofanya kazi vijijini ambako kuna upungufu wa vitabu vya kusoma. Msisitizo umewekwa kwa magonjwa yaliyozoeleka ambayo yanaripotiwa mara kwa mara kwa kuku wanaotunzwa kwa ufugaji huria hapa Tanzania. Maelezo mengi yanahusu mfululizo wa magonjwa yaliyozoeleka yasababishwayo na virusi, bakteria, na ukosefu wa virutubisho mwilini.en_US
dc.identifier.urihttp://10.10.11.5/xmlui/handle/123/729
dc.language.isootheren_US
dc.publisherSokoine university of agricultureen_US
dc.subjectMagonjwaen_US
dc.subjectKukuen_US
dc.subjectVijijinien_US
dc.titleMwongozo wa magonjwa ya kuku vijijinien_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mwongozowamagonjwa.pdf
Size:
370.74 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections