Mifugo na Uvuvi
Permanent URI for this collection
Browse
Recent Submissions
Item Bata mzinga(Ufugaji bora group, 2024-10-11) Ufugaji bora groupBata mzinga ni bata ambao wanahitaji matunzo ya hali ya juu. Kwa kawaida bata mzinga hula chakula kingi kuliko kuku. Bei yake ni ghali zaidi. Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi.Item Mwongozo wa ufugaji bora wa sungura(Wizara ya mifugo na uvuvi, 2020) Wizara ya mifugo na uvuviSungura wako katika kundi la mamalia wadogo katika familia ya Leporidae ya oda ya Lagomorpha .Kuna aina zaidi ya 45 za sungura duniani kote ambazo zinatofautiana kulingana na rangi ukubwa pamoja na matumizi.Sungura hutupatia nyama nyeupe isiyo na mafuta ya lehemu(cholesterol ) na hivyo wataalamu wa lishe huimiza nyama ya sungura kwani ni bora kwa afya hivyo kuitwa nyama tiba.Item Mlo kamili wa kuku(Kuku site, 2024) Kuku siteMlo kamili wa kuku ni mlo wenye virutubisho vyote muhimu anavyohitaji kuku kwa kiwango na uwiano sahihi, Virutubisho vinavyohitajika katika mlo wa kuku ni kama ifuatavyo: 1.Wanga (carbohydrates) Wanga hutumika kama chanzo cha haraka cha nishati (nguvu) katika mwili wa kuku, na inapatikana katika nafaka mbalimbali kama Mahindi, Pumba ya mahindi, Ngano, Mtama, Mchele n.k 2. Protini ( protein ) Ni kirutubisho muhimu ambacho hujenga mwili. Protini inapatikana katika vyakula kama Mashudu ya Alizeti, Dagaa, Soya, Damu n.k 3.Mafuta (Fat) Mafuta ni muhimu sana katika lishe ya kuku kwani humuwezesha kuku kusharabu fat soluble vitamins kama vitamin A, D, E, na K, huhifadhi nishati, kutunza joto na kulinda ogani muhimu katika mwili wa kuku.Item Malezi ya vifaranga(Kuku site, 2024) Kuku siteBanda la vifaranga ni muhimu liandaliwe vizuri. Andaa banda/chumba (brooder room) utakachokitumia kwa ajili ya kulea vifaranga kiwe na sifa zifuatazo: • Hewa ya kutosha. • Mwanga wa kutosha • Chanzo cha joto kama vyungu vya joto au bulb zinazozalisha joto. • Mazingira rahisi ya kufanya usafi. • Nafasi ya kutosha kuepusha msongamano wa vifaranga.Item Kitabu cha mafunzo kwa wafanyakazi wa afya ya wanyama(International Livestock Research Institute untranslated, 2018-07) International Livestock Research InstituteSungura na dende huitwa pia mara nyingi mafugo ndogondogo (mini-élevage). Kundi hili pia lina ndani na nyama zingine zinazo kula majani kama vile « Agoutis ». Sungura na dende zinakula majani, matunda na mbegu. Hizo ni nyama muhimu kwa malisho bora ya binadamu kwa watu wenyi pato ndogo wanaokumbwa na shida za udongo katika inchi nyingi duniani pote, hasa Amerika ya Kusini. Sababu kuu zinazo tuma sungura na dende za chaguliwa kama wanyama wakutowa nyama kwa matumizi ya jamaa na kwa soko ni: • Wao wanatowa kiasi kikubwa cha nyama yenyi onjo bora, tamu, safi na yenye malisho bora iliyo na proteini nyingi (hadi 21 %), yenyi kalori (ya kupana nguvu) chini, mafuta kidogo hasa ile mafuta mabaya yano itwa 3cholestérol » na chunvi ndogo. • Tofauti na wanyama wakubwa, kama vile nguruwe na mbuzi, sungura na dende zinaweza kutumiwa kwa kukuliwa limoja ndani ya jamaa bila kuyiweka siku nyingi ijapokuwa baridi ni shida. • Sungura na dende hujizidisha haraka. Ikiwa malisho yazo na matunzo ni bora, mufugaji ataweza anza ufogo na dike mbili (2) na dume moja (1) na ataweza eneza sungura makumi tano (50) ao zaidi ku mwaka. Hata wakati kuna chakula ya majani tu, dike tatu (3) na dume moja (1) wanaweza kutoa kilo 2 (2 Kg) cha nyama kwa juma na kuongeza chakula cha familia. Kwa upande mwingine, dike 50 hadi 150 hufanya kampuni (entreprise) kubwa ambayo hutoa kazi ku watu wengine na kuongeza pato ya zaidi. • Garama za chakula ni ndogo saana kwa sababu sungura na dende zinaweza kulishwa na majani mbalimbali, na kazalika. Sungura na dende zina tumbo sawa yenyi itaweza tumika sawa ngombe, farasi na tembo kuhusu chakula ya majani. • Sungura na dende zinatowa mboleo bora ambayo una vifaa mingi kuhusu malisho ya mimea hasa ma mbogamboga. Pia, mboleo ya sungura na dende ina proteini mingi, inaweza pia kukaushwa na kuongezwa ndani ya chakula cha wengine wa nyama sawa vile nguruwe, kuku, samaki na kazalika. • Sungura na dende ni rahisi kufuga, hata katika shamba ndogo au ndani za mijini. Nyumba za sungura na dende hazichukuwe nafasi kubwa na kwepesi kuzisafisha (sungura ni safi zaidi, kimya, dende kwa upande wake ni mchezaji mdogo). • Ngozi za sungura zina uzishwa. Kwa vile zinaweza tengeneza kofia, viato (pantouffles), na kazalika. Kwa kuendesha mradi mupya huyu wa ufugo ndogondogo ndani za jamaa inaitajika kuchunguza na kujuwa upendeleo ya wenyi watakao husika ila masuali za kiuchumi ni za maana sana. Jibu kuhusu swali la aina za wanyama wakufuga itazungumuzwa badaye kufwatana mambo itakayo zungumuzwa hapo chini. Ila ni muzuri kujuwa mbele kama siyo vema kufuga sungura dende fasi moja kwa sababu zina maitaji mbalimbali. Kampuni ya wanyama kutoka Ungereza inapendekeza: "Hatuna kupendekeza kuweka sungura na dende kwa sababu zina maitaji tafauti (kwa mfano chakula na nafasi). Sungura zinaweza kutisha dende, ambazo zinaweza kuzizuia ikiwa haziwezi kukimbia. Kuna pia vidudu sawa Bordetella bronchiseptica, inayopatikana katika sungura bila kuonyesha tatizo fulani ila itaweza leta shida za magonjwa za kifuwa/shida za kupumua kwa dende.Item Sera ya Taifa ya ufugaji nyuki(KIUTA Dar es Salaam - Tanzania, 1998-03) Wizara ya maliasili na utaliiSekta ya ufugaji nyuki Tanzania imeendeshwa bila ya kuwa na sera tangu mwaka 1949 wakati ilipoanzishwa rasmi kama idara katika Wizara ya Kilimo. Tangu wakati huo, mwongozo wa kuendeleza na kusimamia rasilimali za nyuki na mimea ya chakula chao umekuwapo kupitia maagizo ya kitaalamu na kiutawala. Madhumuni makuu ya mwongozo huo yalikuwa ni kuufanya ufugaji wa nyuki uwe wa kisasa kwa kuanzisha mizinga ya masanduku, kuongeza uzalishaji wa asali na nta na kuongeza mapato yatokanayo na uuzaji wa asali na nta nchi za nje . Mabadiliko mengi ya kijamii, kiuchumi na kimazingira yanayotokea pamoja na marekebisho ya sera kuu ya uchumi yaliyotekelezwa nchini, na ongezeko la kujali uhifadhi wa mazingira ili kuleta maendeleo endelevu ya ufugaji nyuki yamepelekea kuundwa kwa Sera ya Ufugaji Nyuki. Sera hii inazingatia nafasi ya ushirikiano na uratibu wa sekta mtambuka ambao utaimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali za nyuki na mimea ya chakula chao katika mashamba ya kilimo, misitu na maeneo ya wanyamapori yaliyohifadhiwa. Rasimu ya sera ya ufugaji nyuki awali ilitayarishwa kama sehemu ya Sera ya Misitu na utayarishaji wa rasimu hii ulihusisha washikadau husika katika warsha tatu tofauti, mikutano mbali mbali ya Idara ya Misitu na Nyuki, Washauri wa Kitaalamu na kikosi maalumu cha utekelezaji. Rasimu ya mwisho ilitayarishwa kwa kuboresha na kuunganisha hoja, mapendekezo na maazimio yaliyopitishwa na warsha hizo tatu na katika mikutano mingine ya kiushauri. Chanzo kingine muhimu cha habari zilizotumika katika rasimu hii ya mwisho ni Mpango wa Utekelezaji wa Misitu Tanzania (TFAP) ambao unajumuisha Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki (NBP). Masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya sekta ya ufugaji nyuki yaliyokuwamo katika Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ambayo yalitayarishwa mwaka 1989 yakiwahusisha washikadau wakuu katika mikutano ya vijiji na warsha za kitaifa, yamejumuishwa katika sera hii. Iliamuliwa kuwa rasimu inayojitegemea ya Sera ya Ufugaji Nyuki iandikwe badala ya kuijumuisha na ile ya Misitu, ili malengo na madhumuni yake yawe bayana na yenye kueleweka. Hii pia inatazamiwa kuwa itawezesha kuzingatiwa kikamilifu kwa masuala ya sekta ya ufugaji nyuki na yale ya sekta mtambuka zenye misingi yake katika ufugaji nyuki na matamko ya sera ambayo ndiyo msingi wa uundaji wa Sheria ya Ufugaji Nyuki. Sheria ya Ufugaji Nyuki itakuwa ndiyo nyenzo kuu ya utekelezaji wa sera hii.Item Ufugaji wa nyuki kibiashara na ubora wa mazao yake.(Wakala wa misitu Tanzania, 2019-05-02) Wakala wa misitu TanzaniaKarne mbili zilizopita, ufugaji wa nyuki kibiashara ulianza baada ya kuibuka kwa teknolojia za kukabiliana na wadudu hao na kupanuka kwa soko la asali na mazao yake ikiwamo nta inayotumika viwandani. Licha ya kuwa na zaidi ya miaka 100 ukifanyika, bado biashara ya asali duniani ni fursa kwa wananchi, lakini wengi hawajui kama ipo na imekumbatia utajiri mkubwa. Tanzania ni nchi ya pili duniani katika uzalishaji asali; zao kuu litokanalo na nyuki ikiwa nyuma ya Ethiopia. Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), inaratibu shughuli za ufugaji wa nyuki na ushauri wa kibiashara kwa wazalishaji na wauzaji wa asali na mazao yake. Kalenda ya ufugaji wa nyuki nchini imegawanyika katika misimu minne kulingana na majira kwa mwaka, ambayo hutofautiana kati ya mkoa na mkoa. Kaimu meneja mawasiliano wa TFS, Tulizo Kilaga anasema katika kila msimu, kazi ya ufugaji wa nyuki hutegemea na kundi la nyuki linahitaji nini na mfugaji afanye nini kuweza kuzalisha mazao ya nyuki. “Ipo misimu minne ya nyuki kwa mwaka ambayo ni msimu wa njaa, kujijenga kwa nyuki, mtiririko wa asali na msimu wa mavuno kwa mfugaji wa nyuki,” anasema Kilaga.Item Maua kwa wakulima na wafanyabiashara(Chuo cha kilimo cha Sokoine., 2009) Programu ya pantilCarnation’ ni ua ambalo asili yake ni nchi za Ulaya zenye hali ya hewa ya baridi. Hapa Tanzania maua ya ‘carnation’ yaliletwa na wazungu katika vipindi tofauti. Mpaka sasa maua haya yanalimwa vijiji vya Tchenzcma na Nyandira huko Mgeta na kijiji cha Ruvuma (Morning Side) mkoani Morogoro. Maua aina ya ‘carnation’ pia yanalimwa na kampuni ya Highlanders wilayani Njombe na kijiji cha Ndiwili wilayani Kilolo katika mkoa wa Iringa. Mpaka sasa ugavi wa maua ya ‘carnation’ hautoshelczi mahitaji ya soko la ndani. Kwa mfano, wafanyabiashara wanahitaji zaidi ya banchi 100,000 kwa mwaka wakati wakulima hawawezi hata kuzalisha nusu yake. Matokco yakc maua mengi ya ‘carnation’ kwa ajili ya soko la ndani hununuliwa toka Nairobi nchini Kenya. Ni dhahiri kuwa watu wengi nchini Tanzania hawajui kiliino cha maua ya ‘carnation’. Sehemu hii ya kijitabu ina lengo la kuelezea juu ya kilimo cha ‘carnation’ kwa wakulima wadogo wadogo. hasa uzalishaji wa michc, upandaji wa michc bustanini, utunzaji wa bustani na uvunaji wa maua.Item Mwongozo wa kutengeneza chakula cha samaki na ulishaji wa samaki(Chuo cha kilimo cha Sokoine, 2022) Chuo kikuu cha kilimo cha sokoineSamaki kama viumbe hai wengine wanahitaji kula chakula ili waishi na kukua. Katika mazingira ya asili kama vile mito, maziwa na bahari, samaki hula chakula cha asili kinachopatikana ndani ya maji. Vyakula hivyo ni pamoja na jamii ya mimea na vijidudu wanaopatikana kwenye maji. Lakini, samaki wa kufugwa hususan ufugaji wa kibiashara, huhitaji kulishwa chakula cha ziada chenye ubora iliyo na virutubisho vinavyohitajika ili aweze kukua vyema na kwa haraka zaidi. Uandaaji wa chakula cha ziada cha samaki hutegemea zaidi aina ya samaki, mfumo wa samaki husika katika kumeng’enya (kusaga) chakula pamoja na kiasi cha virutubisho vinachohitajika.Item Kuku wa kienyeji(Chuo cha kilimo cha Sokoine, 2002-12) TARP II SUA ProjectWarsha iliandaliwa na Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania (TARP II SUA) unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoinc cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula pamoja na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo (NLH). Lcngo kuu la warsha lilikuwa ni kubaini sababu zinazofanya uzalishaji wa kuku wa kienyeji kutokidhi mahitaji ya soko na kubuni mbinu za kukabiliana nazo ili mkulima aweze kuongeza uzalishaji wa kuku wa kienyeji na anufaike na soko lililopo la kuku wa kienyeji. Warsha ilikuwa na madhumuni mahsusi yafuatayo ili kufanikisha lengo hilo.Item Mafunzo ya ufugaji(inades formation Tanzania, 1992) Inades formation TanzaniaTanzania ina idadi kubwa ya kuku wa kienyeji wanaofugwa kwa mtindo wa huria vijijini na hata mijini. Katika mtindo huu wa ufugaji, kuku huachwa huru mchana kutwa kujitafutia chakula wao wenyewe. Pengine baadhi ya wakulima huwatupia kuku wao mabaki ya chakula, chenga za nafaka au nafaka zenyewe. Wapo pia wakulima walio na utaratibu wa kuwapa kuku wao pumba za nafaka na maji ya kunywa kila inapowezekana. Zinapofika nyakati za jioni kuku hulala jikoni, au ndani ya nyumba ya mkulima mwenyewe. Ingawaje ufugaji wa aina hii ni rahisi, lakini faida inayopaikana (kama ipo) ni ndogo sana. Kutokana na kuzaana wenyewe wa wenyewe (kutobadili jogoo), lishe duni n.k., kuku hawa wana umbo dogo. Hutaga mayai machache, tena madogo madogo. Nyama yao ina ladha nzuri, lakini kwa vile wana umbo dogo, kiasi cha nyama wanayotoa ni kidogo tu. Katika kijitabu hiki “Kufuga na Kuboresha Kuku wa Kienyeji” tutazungumzia jinsi ya kuboresha kuku wa kienyeji kwa njia ya uzalishaji, kutumia jogoo bora, kuboresha lishe ya kuku. Tutazungumzia pia njia mbalimbali za kufuga zinazoweza kumnufaisha mfugaji mdogo. Kutokana na maarifa haya wewe mkulima utaweza kuona haja ya kufanya mabadiliko katika ufugaji wako. Hi uweze kunufaika na ufugaji ni lazima uwe na mifugo bora. Kitabu hiki kimeandikwa ili kukupatia maarifa na mbinu za kutumia ili upate kuku bora kutokana na kuku wako wa kienyeji. Katika kitabu kingine “ Kufuga kuku wa biashara” Utajifunza maarifa na mbinu bora za ufugaji wa kuku wa biashara. Hawa ni kuku wa kigeni. Wanahitaji matunzo maalum tofauti na yale ya kuku wa kienyeji wanaoboreshwa.Item Ngozi ni mali(chuo cha kilimo cha Sokoine, 2015) chuo kikuu cha kilimo cha sokoineNgozi ni mail kwako wewe na kwa nchi yako. Ngozi za Tanganyika huuzwa mahali pote duniani. Ngozi za nchi yetu lazima ziwe safi kabisa ill ziweze knstahili sifa nzuri katika soko la dunia.Item Kuanzia ngozi, nyama, maziwa na hata manyoya, ngamia ni lulu katika jamii(Shirika la chakula duniani, 2018-02) Shirika la chakula DunianiNgamia ni mnyama muhimu katika maeneo ya ukame au baridi kali anakotumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo usafiri, chakula kupitia maziwa na nyama yake, kuwawezesha wanawake kiuchumi na pia kulinda mazingira. Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limeutenga mwaka huu wa 2024 kuwa wa wanyama wa jamii ya ngamia ambao ni waokozi wa jamii za maeneo ya mbali katika zaidi ya mataifa 90.Item Ufugaji wa kuku(Kituo cha mafunzo ya wakulima, 2023) SATMfugaji wa kuku ana jukumu la kuhakikisha kuku wake wanaishi katika mazingira mazuri kiasi cha kutosha kufanya uzalishaji.Kuku ni jamii ya ndege wanaofugwa.Vifaranga ni watoto wa kuku waliotoka kwenye yai wenyeumri kuanzia siku ya 0 mpaka miezi Kuku wanaokuwa: Hawa ni kuku waliotoka kwenye hatua ya vifaranga,umri ni miezi 2.5- 5.Kuku wakubwa ni kuku waliomaliza hatua ya kuku wanaokuwa,umri wao ni kuanzia miezi 5 na kuendelea.Item Nzige(Wingu la mashahidi, 2022-11-14) Wingu la mashahidiHii ni jamii ya Panzi, ambayo ndio jamii kubwa kimaumbile kuliko jamii zote za panzi, Nzige wanasifa ya kutembea kimakundi na wanahama kutoka ukanda mmoja kwenda mwingine, na wanapotua mahali wanaharibu mazao ndani ya muda mfupi sana. Sifa ya nzige ni kwamba hawana kiongozi kama walivyo wadudu wengine kama Nyuki au Mchwa Lakini Nzige wanatabia ya kula Matawi ya Nafaka na kubakisha mapengo mapengo na kishaItem Uzalishaji bora wa mbuzi wa nyama(Sokoine university of agriculture, 2018) Ndemanisho, Edith EKitabu hiki cha “Uzalishaji bora wa mbuzi wa nyama" kimetayarishwa na mtaalam na muelimishaji wa somo la mbuzi na kondoo kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kwa Aiidi ya miaka 35, Profesa Edith Ndcmanisho. Lengo kubwa la kitabu hiki ni kuwaelimisha wafugaji wadogo wadogo wa mbuzi juu ya ufugaji wa kisasa ili kuongeza pato na lishe kwa familia. Aidha, kimetayarishwa kwa kutumia lugha rahisi inayomwczesha mkulima kuelewa yaliyomo kwa urahisi. Nchini Tanzania kuna mbuzi wanaokadiriwa kufikia milioni 24.5. Hadi sasa. kuna miradi michachc ya utafiti na macndclco ya uzalishaji wa wanyama hawa. Wafugaji wa inbuzi hawajaelimishwa juu ya mbinu mbali mbali za uzalishaji. Kwa hiyo kuna matatizo mengi yanayoathiri shughuli za uzalishaji wa mbuzi ikiwa ni painoja na ulishaji bora, uzalishaji (breeding), mabanda. magonjwa na utunzaji kwa ujumla. Soko la mbuzi ni kubwa hasa katika nchi za Uarabuni na huwa wanatafuta mbuzi wa nyama kwa wingi kutoka Tanzania. Ni vyema wafugaji wa mbuzi wakachangamkia hili soko kwani majirani zetu Kenya huwa wanao mbuzi bora ila idadi yoke sio kubwa kama ya nchini Tanzania.Item Kuku mashuhuri Tanzania(WIKIPEDIA, 2020) WIKIPEDIAKuku Mashuhuri Tanzania ni aina mbalimbali za kuku ambao wanafugwa kwa kiwango kikubwa nchini Tanzania.Item Kitabu cha afya ya wanya mapori(Amerika ya Kaskazini na mradi wa health for animal and liverhood improvement - Hali, 2011) Clifford, Diana; walking, David; Muse, AlexWanyamapori kwenye hifadhi ya wanyama wako chini ya mbinyo wa matishio mbalimbali kama vile ukame uwindaji haramu ujangili mioto na uharibufu wa makazi yao.Tishio jingine kwa wanyama pori ni ugonjwa.Item Mwongozo wa magonjwa ya kuku vijijini(Sokoine university of agriculture, 2002) TARP II-SUA ProjectUtambuzi yakinifu wa magonjwa ya ndege wafugwao ni mgumu kupita ule wa magonjwa ya mifugo mengine. Hii ni kwa sababu dalili za ugonjwa kwa mnyama hai peke yake hazitoshi kusema ugonjwa usumbuao kwa hakika, hivyo uchunguzi wa mnyama aliyekufa ni muhimu sana katika kutoa uamuzi wa ugonjwa usumbuao kwa ndege wafugwao. Mara nyingi, dalili za mgonjwa hai na za yule aliyekufa kwa magonjwa ya ndege wafugwao huwa zinaoana. Pia kwa magonjwa mengi, kuna upungufu au kutokuwepo kabisa kwa ugunduzi yakinifu wa kuaminika, hivyo historia ya ugonjwa pamoja na kufuatilia kwenye kundi ni vitu muhimu katika uchunguzi wa ugonjwa. Pale popote inapowezekana, uchunguzi wa mnyama aliyekufa ufanywe kwenye zaidi ya mnyama mmoja toka kwenye kundi la waathirika na pia uchunguzi wa maabara ufanyike kwenye vipimo vilivyochukuliwa na kuhifadhiwa vyema.Kijitabu hiki cha magonjwa ya ndege wafugwao vijijini kinadhamiria kutoa taarifa za haraka na muhimu kwa magonjwa yaliyozoeleka kwa ndege wafugwao vijijini nchiniTanzania. Kimedhamiriwa kwa wasaidizi wa waganga wa mifugo wanaofanya kazi vijijini ambako kuna upungufu wa vitabu vya kusoma. Msisitizo umewekwa kwa magonjwa yaliyozoeleka ambayo yanaripotiwa mara kwa mara kwa kuku wanaotunzwa kwa ufugaji huria hapa Tanzania. Maelezo mengi yanahusu mfululizo wa magonjwa yaliyozoeleka yasababishwayo na virusi, bakteria, na ukosefu wa virutubisho mwilini.Item MLO KAMILI WA MBWA UNATAKIWA KUWA NA VITU GANI?(Animal Care Unit, 2018-06-11)