Kijitabu cha viua magugu na matumizi yake

dc.contributor.authorCFU-Tanzania
dc.date.accessioned2022-04-12T11:07:45Z
dc.date.available2022-04-12T11:07:45Z
dc.date.issued1996
dc.description.abstractJapokuwa kitengo cha Kilimo Hifadhi (CFU) hakihimizi matumizi ya Viua Magugu vya aina fulani au Viuatilifu vingine vya kukinga mimea, wakulima wanafahamu kuwa Viua Magugu vikitumika kwa usahihi aidhaa kwenye Kilimo Hifadhi au Kilimo cha mazoea huokoa muda mwingi unaotumika kwenye palizi linaloumiza mgongo. Wakulima ambao wanatumia viuatilifu hivi kwa usahihi wanaokoa muda mwingi na gharama zinazotumika kuajiri vibarua kufanya palizi. Wazalishaji na wafanyabiashara wanaosambaza Viua Magugu na Viuatilifu vingine vya mimea wamerahisisha upatikanaji wa viuatilifu husika kote nchi Zambia na ukanda mzima wa kusini mwa Afrika. Hii imefanya wakulima wengi kununua na kutumia viuatilifu mara kwa mara kwenye mashamba yao bila hata kuwa na mafunzo/elimu yakutosha. Wakulima aidha wa Kilimo Hifadhi au wa kilimo cha mazoea hutumia viuatilifu katika mfumo wao wa uzalishaji ili kuongeza kipato kwa lengo la kuongeza ubora wa maisha katika familia. CFU ni shirika kubwa na lenye uzoefu wa kutoa mafunzo ya Kilimo Hifadhi nchini Zambia na kwingineko. Hivyo basi, itakuwa ni kutokuwajibika kama CFU haitatoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu. CFU inaendelea kutoa mafunzo ya kina kuhusu Viua Magugu na matumizi yake kwa wafanyakazi/watumishi wake wote. Mafunzo haya hutolewa kwa Mabwana shamba ambao nao wanawafundisha waratibu wa wakulima. Baada ya hapo waratibu hutoa mafunzo hayo kwa wakulima wengine. Mafunzo haya ni kwa yeyote anayetaka kushiriki na hakuna malipo au gharama yoyote. Watumishi wengi kutoka wizara ya kilimo na kutoka mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali wamenufaika na mafunzo haya yanayotolewa kwa kina na kwa mbinu shirikishi. Kijitabu hiki kimeandaliwa na CFU kama muhtasari wa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya Viua Magugu ambayo yameshatolewa kwa maelfu ya wakulima na wanyunyizaji wa viatilifu hivi. Kijitabu hiki hakilengi kuwa mbadala wa mafunzo ya ana kwa ana.en_US
dc.identifier.urihttp://10.10.11.5/xmlui/handle/123456789/586
dc.language.isootheren_US
dc.publisherCROPBASE (T) Len_US
dc.subjectViua Maguguen_US
dc.subjectDawaen_US
dc.subjectBomba la kupiga dawaen_US
dc.subjectViuatilifuen_US
dc.titleKijitabu cha viua magugu na matumizi yakeen_US
dc.title.alternativeConservation Farming Uniten_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
FINAL_KIJITABU_CHA_VIUA_MAGUGU_NA_MATUMIZI_YAKE.pdf
Size:
4.77 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Main article
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: