Matumizi Bora ya Ardhi
Permanent URI for this collection
Browse
Recent Submissions
Item Usimamizi endelevu wa ardhi ya kilimo(Vi Agroforestry, 2015) Wekesa, Amos; Jönsson, MadeleineMABADILIKO YA TABIA NCHI na hali ya hewa isiyotabilika kwa pamoja huchangia changamoto kubwa kwa wakulima wadogo wadogo katika eneo la Afrika Mashariki.Vi Agroforestry inafanya kazi na wakulima pamoja na asasi za wakulima kuongeza ufahamu wao wa mazingira, kuwasaidia wakulima kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza matumizi ya nishati mbadala/endelevu na pia kuzuia na kupunguza athari za majanga asili yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.Usimamizi Endelevu wa Ardhi ya Kilimo (SALM) ni mbinu zinazotumiwa na wakulima katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza tija katika uzalishaji kwenye kanda mbalimbali za kilimo ikolojia. Mbinu hizi pia zinaweza kutumiwa katika maeneo ya mijini kwa mfano bustani za mbogamboga, mbinu zinazohusu ukulima, nishati mbadala na usimamizi wa maji na maji taka. Mwongozo huu umeweka mbinu mbalimbali ambazo mkulima anaweza kuzitumia kama hatua ya kweli katika kuongeza tija na faida hata kwa vizazi vijavyo hasa kutokana na ufahamu wa hali ya hewa na tabia ya nchi inayobadilika duniani kote na kuathiri uzalishaji wa tijaItem Kilimo bora cha nyasi(Shirika la kilimo Uyole, 1990-05) Myoya, T.JKatika Nyanda za Juu za Kusini ni Mikoa miwili tu (Iringa na Mbeya) ambayo idadi ya ng'ombe wa maziwa imeongezeka sang. Hii ni baada ya kuanzishwa kwa mradi wa kushughulikia wafugaji wadogo wadogo kati ya nchi ya Uswisi na Tanzania. Katika sehemu hizi nyasi za asili zilizopo ni zile za kuezekea na utafiti uliofanyika Uyole unaonyesha kuwa nyasi hizi kutoa chakula kidogo kwa msimu. Vile vile baada ya msimu wa-mvua kuanza nyasi hizi hukua upesi upesi na baada ya miezi miwili tu, hutoa mbegu na hivyo ubora wake kupungua. Hi mifugo ya kisasa iweze kutoa maziwa mengi inahitaji chakula chenye asili mia protini zaidi ya saba kiasi ambacho hakipatikani kwenye nyasi za asili. Hivyo kwa ufugaji wa kisasa ni lazima mbinu nyingine za kuweza kupata malisho bora zitumike. Hata hivyo katika nyanda hizi msimu wa ukuaji wa mimea ni siku 180 tu yaani toka mwanzo wa Desemba hadi mwisho wa Mei. Baada ya hapo malisho hayakui kwa sababu ya baridi kali ya usiku, hasa mwezi wa sita mpaka wa nane, na baada ya hapo kwa ajili ya ukosefu wa unyevu. Hivyo tunakabiliwa na miezi sita ambayo lazima mbinu ya kupata chakula bora zitumike.Item Kilimo na hifadhi ya mazingira(Inades Formation Tanzania, 1993) Gilla, AlliKwa muda mrefu wazee wetu wamekuwa wakitegemea kilimo. Mahitaji yao yote yamekuwa yakitokana na mashamba yao na misitu. Hawakuwa na shida kubwa ya chakula au kuni Leo hii mabadiliko mengi yametokea. Watu wameongezeka sana. Sasa hivi huwezi kufungua shamba mahali popote tu; kila shamba lina mwenyewe. Sio ajabu siku hizi kusikia kesi nyingi zinazohusu mashamba na mipaka. Sasa hivi huwezi kulima kilimo cha kuhamahama au kupumzisha shamba kama walivyofanya wazee. . Siku hizi rutuba ya udongo imepungua sana; matokeo yake mavuno nayo yamepungua. Sehemu nyingine watu wanatumia mbolea kupita kiasi na kuharibu udongo. Sasa hivi upatikanaji wa kuni umekuwa wa tabu. Katika sehemu za milimani kama Mgeta matatizo hayo ni makubwa zaidi. Wakulima wa huko kila siku wanayashuhudia matatizo haya.Item Cascade bonsai(Sokoine university of agriculture, 2023-09-23) Arcoya, EncarniBonsai ya maporomoko ya maji kwa kweli ni mti mdogo unaojulikana na ukweli kwamba shina limeinama kuelekea msingi wa sufuria., kwa namna ambayo matawi na majani yanakua chini, na kufanya sufuria hizi zinapaswa kuwa katika maeneo yajuu kwa sababu matawi mengi ni marefu kuliko sufuria na yanahitaji nafasi kwa urefu.Ni moja ya vielelezo nzuri zaidi kwenye soko, lakini pia ni ngumu kupata, kwani zinahitaji mkonowa mwanadamu kufikia sura hiyo (mara nyingi) na kupata bonsai "kuuza" ni muhimu kwamba miaka kadhaa ipite. .Kati ya hizi, kuna aina mbili ambazo unapaswa kuzingatia: Bonsai ya maporomoko ya maji: Ni bonsai nzuri zaidi, kwani shina huanguka kwenye msingi wa sufuria na ukuaji hutokeachini, na baadhi ya matawi na majani hufuata mwanga (juu). Bonsai ya nusu mteremko:Hizi ndizo rahisi zaidi kupata, lakini hiyo haimaanishi kuwa ni za bei nafuu. Zinatofautiana na zingine kwa kuwa kuanguka kwa mti hakutamkiwi kama kwenye maporomoko ya maji na huwafanya kuwa na umbo la mwelekeo kidogo. Lakini zaidi kidogo.Item Acaccia(Sokoine university of agriculture, 2023-09-16) sarmiento, lourdesAcacia ya Constantinople Ni mti wa asili katika bara la Asia . Inaweza kupima hadi mita12, ingawa ni nadra kwake kuzidi mita 6-7 katika kilimo. Haina ukuaji wa haraka sana au polepole sana, badala yake kiwango cha ukuaji ni cha kati. Katika maeneo yenye upepo inahitaji kuwa chini ya mkufunzi kwa angalau mwaka mmoja au miwili, kwani shina linaweza kuvunjika kwa urahisi, haswa ikiwa mfano ni mchanga. Unaweza kutumia logi ya kuni ambayo unaweza kuzika karibu na mfano mdogo au tumia zabibu ya chuma isiyo nene sana. Kwa kamba kidogo itakuwa sawa.Item Mulberry(Sokoine university of agriculture, 2023-08-10) Segu, Mayka JMorus Alba ni mojawapo ya miti ambayo unaweza kupanda kwenye bustani yako bila kuhangaikia sana. Inakua haraka na inatoa kivuli kizuri, haihitajiki sana katika suala la utunzaji, na ina maalum ambayo inafanya kuwa ya kipekee: haitoi matunda nyeusi.Kwa kuwa haina matunda meusi, hayataishia ardhini, ambayo ni ya vitendo sana, kwa sababu blackberry ni tunda ambalo ni chafu sana na, kwa kuongeza, linaweza kuwa hatari ikiwa utaikanyaga, kwani juisi yake huteleza. . Kwa hivyo ikiwa unafikiria tengeneza bustani ya ndoto yako Kumbuka mti huu.Item Nerine(Sokoine university of agriculture, 2023-10-01) Arcoya, EncarniKama tulivyokuambia hapo awali, jenasi ya Nerine imeundwa na mimea ya bulbous. Hawa wana asili ya Afrika na baadhi yao wanajulikana zaidi kuliko wengine. Ukweli ni kwamba, ingawa kuna spishi ishirini (wengine wanasema ishirini na tano), ni nne au tano tu ndizo zinazojulikana zaidi katika upandaji bustani.Pia huitwa Nerina, Cape of Good Hope Lily au Guernsey Amaryllis. Moja ya sifa za Nerine ni, bila shaka, maua yake. Tofauti na mimea mingine, maua haya hua katika vuli, kuwafanya kuwa na tofauti nzuri ya rangi. Kwa kweli, inasemekana kwamba mimea itatoa maua, lakini hakutakuwa na majani juu yake, lakini badala yake inawajenga katika chemchemi na kuwapoteza katika majira ya joto ili kuacha maua tu kwenye shina.Item Mti wa Palo santo(Sokoine university of agriculture, 2023-09-07) Arcoya, EncarniJambo la kwanza unapaswa kujua ni kwamba asili ya miti ya palo santo ni kutoka kwa mti wa Bursera graveolens. Mti huu ni wa kawaida kwa eneo la Amerika Kusini, haswa kwa nchi za Peru, Ecuador na Brazil. Ina sifa ya kukua hadi karibu mita 10 kwa urefu, na gome laini. Unaweza kujiuliza kwa nini mti huu na si mwingine, na kwa nini inaitwa "kuni takatifu." Kweli, sababu ni kwamba shamans wa Inca wenyewe walitumia. Walichofanya ni kuchukua matawi ya mbao za Bursera graveolens na kuzichoma katika taratibu za kidini na kiroho. Kwao, njia hii ilikuwa na uwezo wa kuvutia bahati nzuri, lakini pia kuwafukuza hasi yoyote.Item Mzeituni(Sokoine university of agriculture, 2023-08-03) Arcoya, EncarniMzeituni wa Arbequina. ni aina ambayo inatoa matokeo mazuri sana na inatumika hatua kwa hatua nchini Uhispania. Inajulikana kuwa, katika mwaka wa 2000, kulikuwa na hekta elfu moja na shamba hili la mizeituni, lakini miaka kumi na saba baadaye idadi hii imeongezeka hadi zaidi ya elfu sabini, ambayo ina maana kwamba ni mojawapo ya bora zaidi. Lakini, unajua nini kuhusu mzeituni wa Arbequina? Unahitaji huduma gani?Item Maeneo ya Kilimo ya Unguja na Pemba(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2011-06) Wizara ya KilimoItem Tathmini ya asali za kiangazi katika mabonde a mpunga(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2011-03) Wizara ya KilimoNdugu Wakulima; sote tunakubaliana kwamba kilimo cha umwagiliaji maji ndio mkombozi wetu kwa ukulima wa mpunga, umuhimu wake umezidi kuwa mkubwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa yanayotokea duniani kote, hali inayosababisha kilimo cha kutegemea mvua kutokuwa cha uhakika na cha matumaini. Hivyo, tunahitaji kujipanga vyema na kukiimarisha kilimo cha umwagiliaji maji ili tuwe na uhakika wa chakula na kupunguza uagizaji. Kwa mujibu wa Mpango Mkuu wa Umwagiliaji maji wa mwaka 2003, Zanzibar tunalo eneo la ekari 21,300 ambazo zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji maji. Hadi sasa eneo lililojengwa miundombinu ni ekari 1,750 sawa na asilimia 8% tu ya eneo lote. Eneo lililobaki lenye ukubwa wa ekari 19,550 kati ya hizo ekari 200 zimejengwa makinga maji, ekari zilizobaki 19,350 zinaendelea kutumika kwa uzalishaji wa mpunga wa kutegemea mvua. Ndugu Wakulima pamoja na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu, bado tunakabiliwa na changamoto za gharama kubwa za ujenzi wa miundombinu, ukarabati wa visima na pampu kutokana na teknolojia duni upungufu wa wataalamu na elimu ya uendeshaji wa jumuiya za wakulima na upungufu mkubwa wa mitaji, utegemezi mkubwa wa nishati ya umeme, uharibifu wa vianzio vya maji pamoja na ukosefu wa zana maalum za utayarishaji wa ardhi. Kutokana na changamoto hizo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya eneo linalofaa kwa umwagiliaji maji linalimwa kwa kutegemea mvua hali ambayo inapelekea uzalishaji na tija ndogo. Ndugu Wakulima, kwa kipindi cha miaka mitano ijayo 2011 – 2016 Wizara ya Kilimo na Maliasili imekusudia kuutekeleza kikamilifu Mpango Mkuu wa Umwagiliaji maji ambao unatarajiwa kutatua changamoto zote za kilimo hicho. Wizara imezungumza na Serikali ya Korea kupitia Benki ya EXIM – ambao wamekamilisha uhakiki wa eneo la ekari 5250 ambalo litajengwa mindombinu ya umwagiliaji maji. Serikali ya Japan na Benki ya BADEA pia wameonesha nia ya kutusaidia katika Kilimo cha umwagiliaji maji. Ndugu Wakulima, Wizara imekusudia kuendeleza ujenzi wa miundombinu na utunzaji wa vianzio vya maji ili sekta ya umwagiliaji maji ipate maendeleo endelevu na kuwawezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga. Kuzijengea uwezo Jumuiya za Wakulima wa umwagiliaji maji ziweze kushiriki kikamilifu katika uendeshaji na utunzaji wa miundombinu, uhifadhi wa vianzio vya maji na utoaji wa huduma za Kilimo. Wizara inaendelea kuwashajihisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kuchagua miradi ya kijamii ya umwagiliaji maji ikiwemo ujenzi wa miundombinu na makinga maji kila wanapopata fursa ya usaidizi wa Washirika wa Maendeleo. Ndugu Wakulima, napenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa wakulima wa mpunga wa umwagiliaji maji watumie mbegu bora na pembejeo zinazotolewa na Wizara ya Kilimo na Maliasili ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo na kuhakikisha kuwa miundombinu ya umwagiliaji maji iliyojengwa kwa gharama kubwa tunaitumia kikamilifu katika uzaalishaji wa zao hili.Item MATANDAZO KUZUIA MMOMONYOKO WA UDONGO KTK SHAMBA(Fodeco, 2019) FodecoItem Mbinu mbalimbali za kuhifadhi maji na udongo na kuzuia mmomonyoko wa ardhi(Echo community, 2013) Kinsey, ErwinItem Njia boa za kukinga Mimea ako dhidi ya jua kali na mvua kubwa(Holly green agric group LTD, 2022-07-20) Lasway, Octavian JItem Mafunzo ya kilimo.(INADES-FORMATION TANZANIA., 1990-07-19) Inades-formation, TanzaniaNi asubuhi na mapema Bwana shamba anakutana na Matonya akiwa na shoka beganiJ hengo mkononi na kibuyu cha maji. Hiki ni kipindi cha kiangazi Miti imepNkutisha majani nyasi na vichaka vyote vimekauka majani yote. Upepo unatimua vumbi kila mahali hasa katika maeneo yenye njia za mifugo mashambani na hata barabarani. Na maeneo ya milimani yameanza kuchomwa moto.Item Taasisi ya utafiti na utetezi wa haki za ardhi(HAKIARDHI, 2011-01-06) Fabian, Beatha; Eliseus, GogfreyMfumo wa milki ya ardhi nchini Tanzania umefanyiwa maboresho makubwa kuanzia miaka ya tisini kwa kutunga sera ya ardhi ya taifa ya mwaka 1995 iliyofuatiwa na sheria mpya za ardhi namba 4 na sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 zote 1999.Item Virus diseases of orchids(Califonia Agricultural, 2008-09-18) Kado, Clarence I.Virus diseases are probably responsible for the mosaic and necrotic symptoms in orchids that are often blamed on other disorders. This circular discusses the four viruses of orchids that have been identified thus far: cymbidium mosaic, orchid tobacco mosaic, vanda mosaic, and cymbidium ringspot. Symptoms in several orchid genera are described, and methods are suggested for disease control. It also tells how to test for these orchid virus diseases on non-orchidaceous, herbaceous plants.Item Mwongozo wa uzalishaji Mazao kulingana na kanda za kiikolojia(Wizara ya Kilimo: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2022-03)Kulingana na taarifa za Kituo cha Utafiti wa Udongo cha Mlingano (TARI-Mlingano) Tanzania ina jumla ya Kanda kuu saba (7) za Kiutafiti wa Kilimo na Kanda ndogo 64 za kiikolojia zinazoonyesha aina ya mazao yanayoweza kuzalishwa. Kanda kuu hizo ni Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Ziwa. Pamoja na Tanzania kuwa na Kanda Kuu saba (7) za Utafiti wa Kilimo na kanda ndogo 64 za Kiikolojia, kwa muda mrefu tija katika uzalishaji wa mazao hayo imekuwa ndogo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa mazao kutozingatia kanda hizo za kilimo za kiikolojia. Aidha, gharama za uzalishaji wa mazao nje ya ikolojia yake ni kubwa hususan wakati miundombinu ya umwagiliaji maji inapohitajika. Mwongozo huu utasaidia kufikia azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuwa mazao yatazalishwa kulingana na ikolojia na hivyo kutoa malighafi ya mazao kwa viwanda vinavyojengwa nchini. Uwepo wa viwanda hivyo utaongeza kasi ya uwekezaji katika kilimo kwa kutumia teknolojia za kisasa na kwa gharama nafuu. Mwongozo umeainisha ni wapi na ni zao gani linastahili kuzalishwa. Kwa mfano, maeneo yanayopata mvua chache yatatumika kwa kuzalisha mazao yanayostahimili ukame kama vile Mtama, Muhogo, Viazi vitamu na mazao ya jamii ya mikunde (mbaazi na kunde). Ili mwongozo utumike kikamilifu, pia kalenda ya kilimo imeandaliwa kwa kuzingatia mwenendo wa mvua katika mikoa mbalimbali nchini. Hata hivyo, kwa kuwa kumekuwepo na mabadiliko ya tabianchi kilimo kinachohimili mabadiliko hayo kinahamasishwa, pia wadau katika sekta ya kilimo wanashauriwa kuwasiliana na watafiti na wataalam wa kilimo walioko katika maeneo yao. Serikali itaendelea kuhimiza huduma za ugani zitolewe kwa kuzingatia mwongozo. Mamlaka za Mikoa na Wilaya zinashauriwa kutunga sheria ndogo katika maeneo yao na kubuni njia bora za kutumia mwongozo huu. Wizara itaendelea kutoa maelekezo pale yanapohitajika ili kuhakikisha lengo la mwongozo huu linafikiwa. Mwongozo huu pia unapatikana katika tovuti ya Wizara www.kilimo.go.tz.Item Kijitabu cha viua magugu na matumizi yake(CROPBASE (T) L, 1996) CFU-TanzaniaJapokuwa kitengo cha Kilimo Hifadhi (CFU) hakihimizi matumizi ya Viua Magugu vya aina fulani au Viuatilifu vingine vya kukinga mimea, wakulima wanafahamu kuwa Viua Magugu vikitumika kwa usahihi aidhaa kwenye Kilimo Hifadhi au Kilimo cha mazoea huokoa muda mwingi unaotumika kwenye palizi linaloumiza mgongo. Wakulima ambao wanatumia viuatilifu hivi kwa usahihi wanaokoa muda mwingi na gharama zinazotumika kuajiri vibarua kufanya palizi. Wazalishaji na wafanyabiashara wanaosambaza Viua Magugu na Viuatilifu vingine vya mimea wamerahisisha upatikanaji wa viuatilifu husika kote nchi Zambia na ukanda mzima wa kusini mwa Afrika. Hii imefanya wakulima wengi kununua na kutumia viuatilifu mara kwa mara kwenye mashamba yao bila hata kuwa na mafunzo/elimu yakutosha. Wakulima aidha wa Kilimo Hifadhi au wa kilimo cha mazoea hutumia viuatilifu katika mfumo wao wa uzalishaji ili kuongeza kipato kwa lengo la kuongeza ubora wa maisha katika familia. CFU ni shirika kubwa na lenye uzoefu wa kutoa mafunzo ya Kilimo Hifadhi nchini Zambia na kwingineko. Hivyo basi, itakuwa ni kutokuwajibika kama CFU haitatoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu. CFU inaendelea kutoa mafunzo ya kina kuhusu Viua Magugu na matumizi yake kwa wafanyakazi/watumishi wake wote. Mafunzo haya hutolewa kwa Mabwana shamba ambao nao wanawafundisha waratibu wa wakulima. Baada ya hapo waratibu hutoa mafunzo hayo kwa wakulima wengine. Mafunzo haya ni kwa yeyote anayetaka kushiriki na hakuna malipo au gharama yoyote. Watumishi wengi kutoka wizara ya kilimo na kutoka mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali wamenufaika na mafunzo haya yanayotolewa kwa kina na kwa mbinu shirikishi. Kijitabu hiki kimeandaliwa na CFU kama muhtasari wa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya Viua Magugu ambayo yameshatolewa kwa maelfu ya wakulima na wanyunyizaji wa viatilifu hivi. Kijitabu hiki hakilengi kuwa mbadala wa mafunzo ya ana kwa ana.Item Zifahamu mbolea za asili na matumiz yake kwaajili ya kuotesha mazao(2020-12-11) Mkulima mbunifuWapendwa wasomaji wa makala za kilimo katika blog yetu ya Kilimo bora leo tumekuandalia makala nzuri juu ya Mbolea . Mbolea kwa maana ya kueleweka kwa haraka ni kitu chochote kinacho ongeza virutubisho muhimu kwenye udondo ambavyo hutumiwa na mimea ili kuboresha ukuaji wa mimea na upatikanaji wa mavuno mazuri. Kuna aina mbalimbali za mbolea kama mbolea za asili Mbolea za asili mfano, Samadi, Mboji, mbolea za kijani na Mbolea za viwandani mfano DAP, YaraMila
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »