Mafunzo ya ufugaji

dc.contributor.authorInades formation Tanzania
dc.date.accessioned2024-05-06T07:57:35Z
dc.date.available2024-05-06T07:57:35Z
dc.date.issued1992
dc.descriptionJaridaen_US
dc.description.abstractTanzania ina idadi kubwa ya kuku wa kienyeji wanaofugwa kwa mtindo wa huria vijijini na hata mijini. Katika mtindo huu wa ufugaji, kuku huachwa huru mchana kutwa kujitafutia chakula wao wenyewe. Pengine baadhi ya wakulima huwatupia kuku wao mabaki ya chakula, chenga za nafaka au nafaka zenyewe. Wapo pia wakulima walio na utaratibu wa kuwapa kuku wao pumba za nafaka na maji ya kunywa kila inapowezekana. Zinapofika nyakati za jioni kuku hulala jikoni, au ndani ya nyumba ya mkulima mwenyewe. Ingawaje ufugaji wa aina hii ni rahisi, lakini faida inayopaikana (kama ipo) ni ndogo sana. Kutokana na kuzaana wenyewe wa wenyewe (kutobadili jogoo), lishe duni n.k., kuku hawa wana umbo dogo. Hutaga mayai machache, tena madogo madogo. Nyama yao ina ladha nzuri, lakini kwa vile wana umbo dogo, kiasi cha nyama wanayotoa ni kidogo tu. Katika kijitabu hiki “Kufuga na Kuboresha Kuku wa Kienyeji” tutazungumzia jinsi ya kuboresha kuku wa kienyeji kwa njia ya uzalishaji, kutumia jogoo bora, kuboresha lishe ya kuku. Tutazungumzia pia njia mbalimbali za kufuga zinazoweza kumnufaisha mfugaji mdogo. Kutokana na maarifa haya wewe mkulima utaweza kuona haja ya kufanya mabadiliko katika ufugaji wako. Hi uweze kunufaika na ufugaji ni lazima uwe na mifugo bora. Kitabu hiki kimeandikwa ili kukupatia maarifa na mbinu za kutumia ili upate kuku bora kutokana na kuku wako wa kienyeji. Katika kitabu kingine “ Kufuga kuku wa biashara” Utajifunza maarifa na mbinu bora za ufugaji wa kuku wa biashara. Hawa ni kuku wa kigeni. Wanahitaji matunzo maalum tofauti na yale ya kuku wa kienyeji wanaoboreshwa.en_US
dc.identifier.urihttp://10.10.11.5/xmlui/handle/123/870
dc.language.isootheren_US
dc.publisherinades formation Tanzaniaen_US
dc.subjectKukuen_US
dc.subjectUfugajien_US
dc.subjectKuku wakienyejien_US
dc.subjectMafunzo ya Ufugajien_US
dc.titleMafunzo ya ufugajien_US
dc.title.alternative;kufuga na kuboresha kuku wa kienyeji.en_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
MAFUNZO YA UFUGAJI.pdf
Size:
4.29 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
pdf
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections