Nini maana ya mifumo ya chakula ?
| dc.contributor.author | The Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) | |
| dc.date.accessioned | 2026-10-16T07:40:46Z | |
| dc.date.available | 2026-10-16T07:40:46Z | |
| dc.date.issued | 2021 | |
| dc.description | Kipeperushi | |
| dc.description.abstract | Mifumo ya Chakula ni watu, maeneo na shughuli ambazo hutupatia chakula. Huwezesha uwepo wa chakula kwa njia nyingi tofauti ambazo hushawishi na kuchagiza maamuzi tunayofanya kuhusu kinacholiwa, kwa wakati upi na namna gani. Mifumo hii ina mchanganyiko wa mambo mengi na hubadilika mara kwa mara -inajumuisha masuala mtambuka na yaliyochangamana na husaidia watu wengi kupata riziki zao. Mifumo ya chakula hujumuisha minyororo ya ugavi wa chakula, mazingira ya chakula na tabia za watumiaji au walaji. Hutegemea vigezo mbalimbali vikiwemo uchumi, utamaduni, teknolojia, na demografia, pamoja na maamuzi na shughuli nyingine za kitaasisi.Mifumo yetu ya chakula kwa maana ya tunakula nini, kwa namna gani na kinatoka wapi, kwa kiasi kikubwa inaamua uwezo wetu wa kufanikisha malengo ya kidunia kwa ajili ya ustawi wa binadamu na sayari yetu nzima. Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yakiwemo kutokomeza umasikini, kutokomeza njaa, afya bora na ustawi, na ulaji na uzalishaji makini yanahusiana moja kwa moja na chakula. Mifumo ya chakula ipo katika kiini cha changamoto nyingi ambazo zinatukabili hivi sasa, zikiwemo afya duni inayochochewa na lishe duni na uharibifu wa mazingira. Theluthi tatu ya dunia inakabiliwa na njaa au lishe duni, zaidi ya nusu ya mzigo wa magonjwa duniani husababishwa na lishe duni, na mifumo ya chakula inachangia uzalishaji wa robo ya gesi ya ukaa duniani. Mifumo ya chakula ipo pia kwenye kiini cha ufumbuzi wa matatizo mengi. Mifumo hiyo hulisha mamilioni ya watu zaidi leo kuliko wakati wote ule. Inaweza sasa kutoa chakula chenye lishe bora zaidi, riziki kubwa zaidi kwa wafanyakazi katika sekta hii, na kurutubisha sayari yetu kwa usalama. | |
| dc.identifier.uri | https://www.mkulima.sua.ac.tz/handle/123456789/1053 | |
| dc.language.iso | other | |
| dc.publisher | The Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) | |
| dc.subject | Chakula | |
| dc.subject | Milo | |
| dc.subject | Lishe | |
| dc.title | Nini maana ya mifumo ya chakula ? | |
| dc.type | Other |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- Nini maana ya mifumo ya chakula_.pdf
- Size:
- 2.96 MB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
License bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- license.txt
- Size:
- 1.71 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description: