Chakula na Lishe
Permanent URI for this collection
Browse
Recent Submissions
Item Ufugaji bora wa samaki(International Tanfeeds, 2023) Iternational TanfeedsMBINU MUHIMU WAKATI WA UANZISHAJI UFUGAJI WA SAMAKI • Mfugaji anatakiwa awe na shauku na dhamira ya kweli ya ufugaji. • Kufanya tathmini ya rasilimali alizonazo kwa ajili ya mradi wa ufugaji wa samaki. • Chanzo endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi. • Hulka ya uvumilivu na kuthubutu. • Tathmini ya soko la bidhaa za samaki. • kujipatia maarifa ya msingi ya ufugaji wa samakiItem Ufugaji bora wa samaki 2025(International Tanfeeds LTD, 2025) International TanfeedsMBINU MUHIMU WAKATI WA UANZISHAJI UFUGAJI WA SAMAKI Mfugaji anatakiwa awe na shauku na dhamira ya kweli ya ufugaji. Kufanya tathmini ya rasilimali alizonazo kwa ajili ya mradi wa ufugaji wa samaki. Chanzo endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi. Hulka ya uvumilivu na kuthubutu. Tathmini ya soko la bidhaa za samaki. kujipatia maarifa ya msingi ya ufugaji wa samakiItem Kilimo cha viazi vitamu - Tanzania(Kituo cha Utafiti wa Miwa Kibaha, 2024) Kituo cha Utafiti wa Miwa KibahaViazi vitamu ni zao mojawapo muhimu la chakula na lishe bora nchini Tanzania. Viazi vitamu vina wanga mwingi hivyo ni njia rahisi ya kuupatia mwili nguvu. Majani ya viazi vitamu yanatumika kama mboga na kuupatia mwili vitamini na madini. Pia viazi vitamu ni chanzo cha kipato. Hata hivyo, wastani wa uzalishaji shambani ni mdogo kiasi cha 5.6t/ha ukilinganisha na uzalishaji unaoweza kufikiwa wa 20–40t/ha. Soko la viazi vitamu sio maalum, kuna wauzaji wadogo na wakubwa.Item Maonyesho ya kimataifa ya Nanenane(Wizara ya Mifugo na Uvuvi, 2025) Wizara ya Mifugo na UvuviBodi ya Nyama Tanzania imeundwa chini ya Sheria ya Nyama Namba 10 ya Mwaka 2006 na kuzinduliwa tarehe 14 Novemba 2008. Bodi imepewa mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa Sheria ya nyama kwa lengo la kuweka misingi madhubuti ya kiutawala ili kuhakikisha uzalishaji, usindikaji na biashara ya nyama na bidhaa zake unazingatia viwango vya ubora ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje.Item Usindikaji rahisi wa muhogo(Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo( SUA ), 2022) Silayo V. C. K.; Laswai H. S.; Mpagalile J. J.; Ballegu W. R.; Makungu P. J.; Mtunda K.; Chilosa D.; Nyborg I.Muhogo ni zao mbadala kwa wakulima wa "Tanzania. Faida za muhogo ni nyingi na hasa katika kuongeza uhakika wa chakula na pato la kaya. Uboreshwaji wa njia za kusindika muhogo ili kupata aina mbalimbali za vyakula umeongeza nafasi ya muhogo katika kilimo hapa Tanzania. Shime sote tuongeze juhudi katika kilimo cha muhogo - MUHOGO NI MALI.Item Zijue taratibu za uzalishaji wa mbegu za viazi vitamu zilizothibitishwa ubora wake(Mradi wa Bioinnovate - ICOPSEA, 0209-07) Taasisi ya Utafiti wa Kilimo MikocheniViazi vitamu ni zao muhimu la chakula na lishe bora nchini Tanzania. Viazi vitamu vina wanga mwingi hivyo ni njia nafuu ya kuupatia mwili nguvu. Majani ya viazi vitamu hutumika kama mboga na hivyo ni chanzo cha vitamini na madini joto mwilini. Pia viazi vitamu ni chanzo cha kipato kwa familia na taifa.Item Matunzo ya shamba na uvunaji wa zabibu(TARI, 2024) Taasisi ya utafiti wa kilimo TanzaniaMATUNZO YA SHAMBA NA UVUNAJI Ili kupata mavuno yenye tija ni muhimu kutunza vizuri shamba la mizabibu. Matunzo ya shamba ni pamoja na kupalilia, kutifulia, kudhibiti visumbufu na kukatia mizabibu. Palilia shamba mara kwa mara ili kudhibiti magugu, kwa wastani palizi tatu zinatosha katika msimu mmoja . Ni muhumu kutifulia udongo kwenye shamba la mizabibu kila wakati ili kuvuna maji ya mvua.Item Utayarishaji wa mboga za majani(Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA ), 2015) Kinabo J. L.; Msuya J.M.; Mnkeni A.P.; Nyaruhucha C.; Ishengoma J.Mboga za majani zinashika nafasi muhimu sana katika vyakula vyetu. Zinaliwa kila siku na mara nyingi zaidi ya mara moja kwa siku. Zipo aina nyingi za mboga za majani, nyingine zinalimwa na nyingine zinaota zenyewe porini na mashambani wakati wa msimu wa mvua. Mboga zina virutubishi kama madini na vitamini ambavyo vinahitajika mwilini kwa afya bora. Hata hivyo pamoja na kwamba zina virutubishi vya kutosha na zinaliwa kila siku, watu wengi wanapata matatizo ya afya yanayotokana na ukosefu wa virutubishi vinavyopatikana katika mboga za majani kwa mfano upofu na upungufu wa damu. Hali hii inajitokeza kwa sababu gani?Item Utayarishaji wa mboga za majani(Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), 2015) Kinabo J. L; Msuya J.M; Mnkeni A.P; Nyaruhucha .C; Ishengoma .JUtangulizi Mboga za majani zinashika nafasi muhimu sana katika vyakula vyetu. Zinaliwa kila siku na mara nyingi zaidi ya mara moja kwa siku. Zipo aina nyingi za mboga za majani, nyingine zinalimwa na nyingine zinaota zenyewe porini na mashambani wakati wa msimu wa mvua. Mboga zina virutubishi kama madini na vitamini ambavyo vinahitajika mwilini kwa afya bora. Hata hivyo pamoja na kwamba zina virutubishi vya kutosha na zinaliwa kila siku, watu wengi wanapata matatizo ya afya yanayotokana na ukosefu wa virutubishi vinavyopatikana katika mboga za majani kwa mfano upofu na upungufu wa damu. Hali hii inajitokeza kwa sababu gani?Item Uhakika wa Chakula Katika Kaya(Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, 2001) Kinabo J. L.Uhakika wa chakula unamaanisha kuwepo kwa chakula cha kutosheleza mahitaji ya jamii nzima kwa muda wote kwa ajili ya afya bora. Kaya ambayo hai- wezi kutimiza mahitaji yake ya chakula kwa kipindi cha mwaka mzima haina uhakika wa chakula. Kaya hiyo inatambulika kuwa ina tatizo sugu la uhakika wa chakula. Mara nyingi kaya hizo huwa ni maskini kupindukia na hasa wale wasio na ardhi au kitega uchumi chochote. Tatizo la muda mfupi wa uhakika wa chakula ni lile ambalo kaya ina uwezo wa kupata chakula kwa kipindi kifupi tu cha mwaka.Item Zao la iliki(Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), 2022) TARIUtangulizi Iliki ni moja kati ya mazao ambayo yanatumika sana karibia kila siku kwenye matumizi ya nyumbani, hutumika kama viungo kwenye chai, chakula na pia kama tiba ya magonjwa mbalimbaliItem Kilimo cha karafuu(Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), 2022) TARIUtangulizi Kuna ukuaji mkubwa wa mahitaji ya mazao ya viungo duniani ingawa uzatishaji na uuzaji wa viungo ni wa chini pamoja na kuwa na maeneo mazuri ya uzalishaji. Ikiwa uzalishaji utakuwa na ubora hasa matumizi ya mbegu bora na kilimo kisichotumia mbolea za viwandani soko lake ni ufumbuzi kwa mkulima. Soko la nje ni kama Afrika ya kati, Asia, Ulaya, Afrika na Amerika. Soko la ndani linajumuisha Zanzibar na Tanzania Bara.Item Kilimo bora cha alizeti(Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania( TARI), 2022) TARIZao la alizeti ni miongoni mwa mazao ya mbegu za mafuta, zao hili hutoa mafuta ya kula kwa binadamu na mashudu kwa ajili ya chakula cha mifugo. Alizeti ni zao lenye thamani kiuchumi na mafuta hutumika katika utengenezaji wa vipodozi, madawa na nishati mbadala kwenye viwanda Maua ya alizeti hutumika kama mapambo na kutoa chavua kwa ajili ya nyuki kutengeneza asaliItem Ijue Faida Ya Kula Magimbi Kiafya Muungwana Blog ,2018(Muungwana Blog, 2018) Muungwana BlogMagimbi ni kinga na pia ni tiba kama ambavyo nitakueleza leo faida za magimbi.Item Faida za kiafya za Mayai(Uly Clinic, 2020-04-05) Uly ClinicMayai ni aina ya chakula muhimu kwa binadamu, huwekwa kwenye kundi la vyakula vyenye protini. Mbali na kuwa na protini mayai ni chanzo kizuri cha vitamini A, B, B12 na D, kolesto kwa wingi na madini ya lutein na zeaxanthin . Yai huweza kuliwa likiwa bichi, kuchemshwa au kukaangwa. Kama ilivyo kwa baadhi ya vyakula, yai hupoteza virutubisho linapochemshwa kwa muda mrefu au kukaangwa. Vitamin D kwenye yai hupungua kwa kiwango kikubwa endapo yai litapikwa kwa muda mrefu. Hata hivyo kuchemsha au kukaanga yai kwa muda mrefu hupunguza kwa asilimia kwa asilimia 90 hivyo kupoteza umuhimu wake katika mwiliniItem Vitamini Muhimu kutoka kwa kuku(Timu ya Medicover, 2024-08-05) Timu ya MedicoverKuku ni chakula kikuu katika lishe nyingi ulimwenguni, sio tu kwa utangamano wake na ladha yake, lakini pia kwa faida zake za lishe. Miongoni mwa faida hizo ni vitamini na madini muhimu ambayo kuku hutoa, ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa afya yetu kwa ujumla. Makala hii itachunguza vitamini muhimu vinavyopatikana katika kuku, ikiwa ni pamoja na Vitamini C na Vitamini B12, pamoja na virutubisho vingine muhimu.Item MWONGOZO WA MAFUNZO YA ULISHAJI WA WATOTO WACHANGA NA WADOGO(Taasisi ya chakula na lishe, 2014) Wizara ya afya na ustawi wa jamiiUnyonyeshaji wa maziwa ya mama una faida nyingi na unachangia kwa kiasi kikubwa, katika afya na maendeleo ya mtoto, pamoja na afya ya mama. Unyonyeshaji unaboresha afya ya mtoto kwa kumpatia chakula kinachohitajika kwa ukuaji na maendeleo yake. Mtoto mwenye hali nzuri ya lishe huweza kupambana na magonjwa kuliko yule mwenye utapiamlo. Ulishaji sahihi huchangia katika kupunguza makali ya ugonjwa hasa maradhi ya kuhara na yale ya njia ya hewa, endapo mtoto ataugua. Kwa muda mrefu, mpango wa kuzuia magonjwa ya kuhara umetambua kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee bila kumpa mtoto hata maji kwa miezi sita ya mwanzo, kunapunguza kwa kiasi kikubwa maambukizo na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kuhara. Pia kuendelea kumnyonyesha na kumpa mtoto chakula cha nyongeza kuanzia miezi 6 hadi miaka 2 au zaidi ni muhimu.Item Karafuu(Muungwana blog, 2016-10-02) Muungwana Blog.Karafuu ni zao linalotokana na mkarafuu, ingawa karafuu hazimo katika kundi la vyakula wala vinywaji lakini ni kiungo na dawa muhimu sana kwa maisha ya binadamu.Mikarafuu ilianza kupandwa kwenye visiwa vya Shelisheli, Mauritius na sehemu nyinginezo katika karne ya 19. Miche ya mikarafuu ililetwa Zanzibar kutoka Indonesia, mashariki ya mbali mwaka 1818. Mikarafuu inastawi zaidi Visiwani vya Unguja na Pemba ambapo katika miaka 30 iliyopiata Zanzibar ilikuwa inazalisha asilimia 80 ya karafuu zote zinazohitajika duniani ambapo uchumi wake ulitegemea sana zao la karafuu.Item Faida za Mwani Kiafya(Swahili BBC, 2022-12-26) Swahili BBCMwani wa bahari 'Chondrus crispus' ni mwani wa kuliwa unaokua katika maeneo ya pwani ya Atlantiki, pamoja na yale ya Uropa na Amerika Kaskazini, na pwani ya Afrika. Kama magugu mengine ya baharini, ni chanzo tajiri cha virutubishi vingi ambavyo ni vigumu kupata. Inajulikana zaidi kama 'seamoss' mwani wa baharini, matumizi yake makubwa hutumika kwa kuongeza uzito na hutumiwa sana na watengenezaji wa vyaula vya kusindika.Item Kilimo cha Majani ya Malisho ya Mifugo(SUA, 2022-09) SUAWafugaji nchini Tanzania wametakiwa kuanza kulima majani aina ya JUNCAO yanayozalishwa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kutokana na majani hayo kuonekana kuwa na faida nyingi kwa mifugo na uwezo wake wa kukua haraka na kuvumilia ukame na hivyo kupunguza changamoto za malisho wakati wa kiangazi na kumaliza migogogo ya wakulima na Wafugaji.