Kanuni za Kilimo Bora cha Alizeti Tanzania
Loading...
Date
2018-03
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Mogriculture TZ
Abstract
Alizeti hutambulika kitaalamu kama Helianthus Annus na hulimwa kwa wingi karibu maeneo yote nchini Tanzania katika nyanda za kaskazini, kati, mashariki pamoja na nyanda za juu kusini hasa katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara na Rukwa. Hii inatokana na uwezo wa alizeti kustawi vizuri katika mazingira mengi tofauti bila ya kuwa na utofauti mkubwa katika uzalishaji wake.
Asili ya zao hili ni nchini Marekani ambako lilienea katika maeneo ya Ulaya na baadae kusambaa sehemu nyingine za dunia ambapo kwa sasa Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa uzalishaji wa alizeti nyuma ya Afrika ya kusini.
Description
Keywords
Alizeti, Mbegu za mafuta