Uzalishaji Mazao
Permanent URI for this collection
Browse
Recent Submissions
Item Kilimo cha Pilipili Mtama(Wizara ya kilimo na Chakula, Tanzania, 2022) Sehemu ya Uinuaji Mazao, Wizara ya Kilimo Chakula na UshirikaPilipili mtama ni zao ambalo asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar. Matumizi Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki na kwa mapishi mengine mbalimbaliItem Kilimo bora cha zao la mkonge(Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), 2022) TARIMkonge ni zao linalostahimili sana ukame, ma- gonjwa, na wadudu waharibifu. Hivyo mkonge unahitaji pembejeo chache kuliko mazao men- gine katika uzalishaji. Mkonge hustawi kuanzia usawa wa bahari Mita 0 - 750 na kwenye mae- neo yenye mvua kiasi cha Milimita 500 - 1200 kwa mwaka.Item Kitabu cha mafunzo cha mbinu za kilimo hai za uzalishaji wa mazao ya msimu(Suistanable Agriculture Tanzania - SAT, 2019-11-06) Suistanable Agriculture Tanzania - SATKitini hiki cha “Mbinu za kilimo hai za uzalishaji wa mazao ya msimu” ambacho kimezungumzia kwa undani juu ya uzalishaji wa karanga, alizeti, korosho, choroko, njugu, mahindi, mtama na muhomo kimeandaliwa na shirika la SWISSAID Tanzania kwa ushirikiano na Kilimo Endelevu Tanzania (SAT – Sustainable Agriculture Tanzania). Kitini hiki kimepitiwa na kuidhinishwa na wawakilishi wa Ofisi ya Kilimo ya Mkoa wa Mtwara, Ministry of Agriculture Training Institute (MATI) Naliendele, Sustainable Agriculture Tanzania (SAT), Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM), Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO), Tanzania Official Seed Certification Institute (TOSCI-Mtwara), Shirika la Uhifadhi Misitu Asilia Tanzania (TFCG), wawakilishi wa wakulima na SWISSAID Tanzania katika warsha iliyofanyika tarehe 25 – 27 September 2019 katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara. Pia, msaada wa kifedha kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Liechtenstein Development Service (LED) na Swiss Agency for Development and Cooperation (SDC) umefanikisha kwa kiwango kikubwa katika kugharamia uandaaji, kupitia na kukamilisha uchapishaji wa kitini hiki.Item Jinsi ya kulima mgagani: kilimo bora cha mgagani(Melkisedeki, 1998) Melkisedeki, MelkisedekiMigagani, migange, mikabili au miangani ni mimea ya jenasi Cleome katika familia na oda Brassicales (kabichi). Mgagani (Cleome gynandra) au Spider plant kwa kingereza, ni mmea wa asili ya Afrika unaostawi vizuri kwa kumwagiliwa hapa afrika ya mashariki wakati wa joto. Pia huchumwa mashambani ikiwa imeota yenyewe zao hili hushambiliwa na magonjwa na wadudu mara chache. Majani na Matawi machanga yana virutubisho kuliko Sukuma wiki na kabichi. Mahitaji yake yanaongezeka kwenye miji midogo na mikubwa kila siku. Mgagani wa kawaida, huliwa takriban kila mahali pa Afrika na katika mabara mengine pia. Wanawake wengi wenye mimba au waliozaa hula mmea huu, kwa sababu una chuma nyingi kiasi na husaidia kuongeza damu. Mboga ya mgagani huitwa magagani.Item Kilimo Bila Udongo(Globalpublishers.co.tz, 2020-01) Globalpublishers, Globalpublisherskilimo Bila Udongo,katika teknolojia hii, kinachofanyika ni kujua ili mmea uweze kumea, kukua na kutoa mazao, huwa unahitaji virutubisho na madini gani katika ardhi? Ukishajua mahitaji hayo, basi zinatafutwa kemikali zenye virutubisho vinavyotakiwa, zinachanganywa kwenye maji na kuwekwa kwenye mabomba maalum ambayo kwa juu, huwa yana matundu maalum ambapo ndipo mmea unaotakiwa kulimwa,/huwekwa.Item Kilimo cha Nyanya Chungu(Mjasiriamali Hodari, 2018-02)Nyanya chungu ni zao jamii ya mbogamboga linalotumika kwa matumizi mengi kama mboga, dawa n.k. Zao hili hustawi maeneo yenye halijoto tofauti tofauti nchini Tanzania.Item Aina Tatu za Kahawa Tanzania(Mafatanzania blog/Mtanzania.co.tz, 2024-03) Matanzania blog, Mtanzania.co.tzKampuni ya ITO EN LTD, ambayo ni kampuni tanzu ya Tully’s Co. Ltd., inayomiliki migahawa maarufu ya Tully’s Coffee, imezindua aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania, nchini Japan katika hafla iliyofayika jijini Tokyo tarehe 14 Machi, 2024. Aina za kinywaji hicho pendwa nchini humo kinachotokana na kahawa kutoka Tanzania ni TULLY’s COFFEE BARISTA BLACK KILIMANJARO; TULLY’S COFFEE MY HOME BLACK KILIMANJARO; na TULLY’S COFFEE BARISTA ROAST COLD BREW – KILIMANJARO BLEND. Kahawa hizo ni kutoka mkoa wa Arusha, Tarime mkoani mara na mashamba ya GDM yaliyoko Mbozi mkoani Mbeya.Item Mafunzo ya kilimo cha maharage(SUA, 2024-03) Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine, Food LandKitabu hichi kimezungumzia mambo mbalimbali kama Maandalizi ya ardhi,namna bora ya upandaji, aina ya maharage na sifa zake na virutubisho vinavopatikana kwenye maharage.Item Kilimo Bora cha Migomba(Maendeleo Vijijini, 2017-03) Mbega, DanielKWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi, lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara.Item Kilimocha kunde(IIT, 2008-06) IIT, CGIARKunde ni zao jamii ya mikunde. Faida kubwa ya zao hili ni: • Chanzo cha viini lishe vya protini kwa binadamu na wanyama. • Mabaki ya mmea wa kunde ni chakula kizuri cha mifugo. • Hurutubisha udongo.Item Kilimo Cha Pamba Tanzania(Wauzaji Blog, 2024-08) Minja, LenaldKilimo cha Pamba hulimwa nchini Tanzania na hukuzwa mikoa mbalimbali na pia pamba ndio hutumika kutengenezea uzi na nguo,mafuta.Item Fahamu Kilimo Cha Njugu Mawe(Kilimoajira, 2018-09) KilimoajiraNjugu ni mbegu za mmea wa njugu. Mmea huo unapoendelea kusitawi huwa unachanua maua ya manjano ambayo hujichavusha yenyewe.Item Kilimo cha Matikiti Maji: Masoko na Fursa za Kibiashara(Mogri culture Tanzania, 2023-03) Mtalula, MohamedMatikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuri za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine (curcubitaceae family) kama matango, maboga na maskwash (squash). Tikiti maji ni zao la kipekee ambalo limekuwa likibamba soko la ndani na nje ya Tanzania kutokana na ladha yake nzuri, faida zake kiafya, na matumizi yake katika viwanda vya chakula na vinywaji. Hata hivyo, ili kuweza kunufaika na soko hili, mkulima anahitaji kujua mbinu bora za kilimo, mahitaji ya soko, na fursa za biashara. Katika makala hii, nitaelezea kwa kina kuhusu masoko ya matikiti maji Tanzania, mahitaji ya soko, jinsi ya kuongeza uzalishaji, na fursa za biashara. Nitakupa miongozo na mikakati ya kufikia masoko ya ndani na nje ya nchi, na kujenga uhusiano mzuri na wanunuzi na wazalishaji wa viwandani. Kupitia makala hii, utajifunza jinsi ya kuongeza uzalishaji wa matikiti maji, jinsi ya kujenga thamani ya matunda yako, na jinsi ya kufikia masoko ya ndani na nje ya nchi. Kwa hiyo, endelea kusoma ili kuweza kujifunza zaidi kuhusu Kilimo cha tikiti Maji Tanzania na fursa zake za biashara.Item Faida za Kiafya zinazopatikana katika ulaji waTikitimaji(TUKO, 2022-05) TUKOUnapokula tikitimaji, utafaidi protini, Calcium, Phosphorus, Iron, Vitamin A, B6, C. Potasium, Magnesium, Carotene, mafuta, nyuzinyuzi (fiber), na madini mengineyo. Pia mwili utapata nguvu za kupambana na maradhi na kukuondoa katika hali hatari. Read more: https://kiswahili.tuko.co.ke/367173-faida-10-za-kiafya-zinazopatikana-katika-ulaji-wa-tikitimaji.htmlItem Kilimo cha Binzari(Wizara ya kilimo, 2014-01-31) Wizara ya kilimoJina la kitalaam ni Curcuma domestica na kwa kiingereza ni turmeric. Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga, Kagera Kilimanjaro, Morogoro naZanzibar.Item Kupanda Mikorosho mipya(Taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendele, 2022-06-25) Taasisi ya utafiti wa kilimo NaliendeleKipeperushi kinazungumzia upandaji wa mikorosho mipya ambappo ni kitendo cha kuanzisha shamba jipya kwa kufuata kanuni za kilimo bora cha mikorosho.Mashamba ya wakulima wengi yana mavuno hafifu, uzaaji mdogo hali iliyotokana na upandaji holela na duni na utumiaji wa mbegu hafifu.Item Faida katika miradi ya kilimo - Maharage(Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, 2024-02-24) Mishili, Fulgence J.Kilimo Biashara ni shughuli za biashara na usimamizi zinazofanywa na makampuni na wazalishaji ambazo hujishughulisha katika utoaji wa pembejeo kwa sekta ya kilimo na ufugaji, kuzalisha mazao, uchakataji, usafirishaji, huduma za kifedha, usambazaji, au utafutaji wa masoko ya mazao.Item Matunzo ya Mikorosho shambani(Taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendele, 2022-06-25) Taasisi ya utafiti wa kilimo NaliendeleItem Upogoleaji mikorosho michanga iliyobebeshwa(Taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendele, 2022-06-25) Taasisi ya utafiti wa kilimo NaliendeleItem Uanzishwaji wa kitalu cha miche ya mikorosho.(Taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendele, 2022-06-25) Taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendele