Mwongozo wa uzalishaji Mazao kulingana na kanda za kiikolojia

dc.date.accessioned2022-04-13T09:52:17Z
dc.date.available2022-04-13T09:52:17Z
dc.date.issued2022-03
dc.description.abstractKulingana na taarifa za Kituo cha Utafiti wa Udongo cha Mlingano (TARI-Mlingano) Tanzania ina jumla ya Kanda kuu saba (7) za Kiutafiti wa Kilimo na Kanda ndogo 64 za kiikolojia zinazoonyesha aina ya mazao yanayoweza kuzalishwa. Kanda kuu hizo ni Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Ziwa. Pamoja na Tanzania kuwa na Kanda Kuu saba (7) za Utafiti wa Kilimo na kanda ndogo 64 za Kiikolojia, kwa muda mrefu tija katika uzalishaji wa mazao hayo imekuwa ndogo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa mazao kutozingatia kanda hizo za kilimo za kiikolojia. Aidha, gharama za uzalishaji wa mazao nje ya ikolojia yake ni kubwa hususan wakati miundombinu ya umwagiliaji maji inapohitajika. Mwongozo huu utasaidia kufikia azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuwa mazao yatazalishwa kulingana na ikolojia na hivyo kutoa malighafi ya mazao kwa viwanda vinavyojengwa nchini. Uwepo wa viwanda hivyo utaongeza kasi ya uwekezaji katika kilimo kwa kutumia teknolojia za kisasa na kwa gharama nafuu. Mwongozo umeainisha ni wapi na ni zao gani linastahili kuzalishwa. Kwa mfano, maeneo yanayopata mvua chache yatatumika kwa kuzalisha mazao yanayostahimili ukame kama vile Mtama, Muhogo, Viazi vitamu na mazao ya jamii ya mikunde (mbaazi na kunde). Ili mwongozo utumike kikamilifu, pia kalenda ya kilimo imeandaliwa kwa kuzingatia mwenendo wa mvua katika mikoa mbalimbali nchini. Hata hivyo, kwa kuwa kumekuwepo na mabadiliko ya tabianchi kilimo kinachohimili mabadiliko hayo kinahamasishwa, pia wadau katika sekta ya kilimo wanashauriwa kuwasiliana na watafiti na wataalam wa kilimo walioko katika maeneo yao. Serikali itaendelea kuhimiza huduma za ugani zitolewe kwa kuzingatia mwongozo. Mamlaka za Mikoa na Wilaya zinashauriwa kutunga sheria ndogo katika maeneo yao na kubuni njia bora za kutumia mwongozo huu. Wizara itaendelea kutoa maelekezo pale yanapohitajika ili kuhakikisha lengo la mwongozo huu linafikiwa. Mwongozo huu pia unapatikana katika tovuti ya Wizara www.kilimo.go.tz.en_US
dc.identifier.urihttp://10.10.11.5/xmlui/handle/123456789/601
dc.language.isootheren_US
dc.publisherWizara ya Kilimo: Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaen_US
dc.relation.ispartofseriesKilimo ni Biashara;Agenda 10/30
dc.subjectKilimoen_US
dc.subjectBiasharaen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleMwongozo wa uzalishaji Mazao kulingana na kanda za kiikolojiaen_US
dc.typeBooken_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mwongozo wa Uzalishaji.pdf
Size:
1.64 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: