Wadudu,magonjwa na magugu
Loading...
Date
2009
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Tanzania Organic Agriculture Movement - TOAM
Abstract
Kwa mtazamo wa kiekolojia, viumbe wote ni sehemu ya mfumo asilia bila kujali
vinafanya nini. Kwa mkulima, viumbe vyote ambavyo hupunguza mavuno ya mazao
yake huchukuliwa kuwa ni wadudu waharibifu, magonjwa au magugu. Wadudu, ndege
au wanyama wengine pia ni waharibifu wakati wanapo sababisha uharibifu kwa mimea
au mazao yaliyohifadhiwa ghalani. Fangasi, bakteria na virusi pia hutambulika kama
vijidudu vinavyosababisha magonjwa wakati vinapoingilia au kubadilisha michakato
muhimu kwenye mmea unaokua au mavuno yaliyohifadhiwa. Mimea yote isiyotakiwa
ambayo hustawi ndani ya shamba pamoja na mazao na kushindania virutubisho, maji
na mwanga huchukuliwa kuwa ni magugu. Mimea ya namna hii pia ndio inaweza kuwa
hifadhi kwa wadudu/wanyama waharibifu na magonjwa.
Kuwepo kwa viumbe hivi katika mashamba ya mazao sio tatizo mpaka pale idadi
yao inapoongezeka kupita kiwango ambacho wanaposhambulia husababisha kupungua
kwa kiasi kikubwa wingi wa mavuno na ubora wa mavuno na mazao yaliyohifadhiwa.
Wakulima wanaosubiri hadi wakati huu, mara nyingi hutegemea kutumia njia ambazo
zina athari na uharibifu mkubwa ili kudhibiti uharibifu kwa mazao. Hata hivyo, kwa vile
wakulima wengi wadogo wa Kiafrika hawawezi kupata au kumudu njia na bidhaa za
kufanya hivyo, matokeo yake ni hasara kubwa kwenye mavuno na ubora wa mazao. Kwa
ujumla, changamoto zinazo ambatana na udhibiti wa wadudu, magonjwa na magugu
zinaweza kufafanuliwa kwa muhtasari kama ifuatavyo;
Description
Keywords
Kilimo hai, Kilimo nadhifu, Wadudu, Magonjwa, Magugu