Baiashra ya ufugaji bora wa kuku wa asili: kitabu cha mwongozo

dc.date.accessioned2018-02-23T11:55:25Z
dc.date.available2018-02-23T11:55:25Z
dc.date.issued2008
dc.description.abstractUfugaji wa kuku ni nyenzo nzuri ya kujipatia kipato katika kaya kwa sababu ufugaji wa kuku hauhitaji mtaji mkubwa na hauna kazi kubwa kiuendeshaji. Katika ufugaji huria kuku hujitafutia chakula wenyewe. Pia inapowezekana hupewa mabaki ya chakula, chenga, pumba au nafaka yoyote inayopatikana katika mazingira husika. Kwa walio wengi ifikapo nyakati za jioni, kuku hulala jikoni au ndani nyumbani kwa mfugaji mwenyewe. Ufugaji huu ni rahisi kwa kuwa hauna gharama kubwa ila faida yake ni kitoweo tu au fedha kidogo sana. Kutokana na lishe duni na kuzaana wenyewe kwa wenyewe (bila kubadili jogoo), kuku wa kienyeji walio wengi wana uzito mdogo. Wana wastani wa uzito wa robo tatu za kilo hadi kilo moja wakiwa na umri wa zaidi ya mwaka mmoja. Ila wakitunzwa vizuri zaidi na kuboreshwa wana uwezo wa kufikia uzito wa kilo moja hadi moja na nusu katika umri wa miezi sita hadi nane. Kwa upande wa utagaji wa mayai kuku wa kienyeji kwa wastani hutaga mayai 50 hadi 65 kwa mwaka. Wakitunzwa vizuri zaidi huweza kufikia uzalishaji wa mayai 80 hadi 100 kwa mwaka. Kijitabu hiki kinatoa maelezo ya njia na kanuni mbalimbali rahisi za kuzingatia ili mfugaji aweze kuzitumia kupata mazao mengi na bora zaidi yatakayomnufaisha kimapato na kwa matumizi mengine. Kanuni hizi ni pamoja na: √ Kuchagua njia bora ya kufuga na sifa za mabanda bora ya kuku √ Kuchagua aina bora ya kuku wa kufuga, kuzaliana na kutotolesha √ Utunzaji wa vifaranga √ Kutengeneza chakula bora cha kuku √ Kudhibiti na kutibu magonjwa √ Kutunza kumbukumbu √ Kutafuta masokoen_US
dc.identifier.urihttp://10.10.11.5/handle/123/116
dc.language.isootheren_US
dc.publisherRural Livelihood Development Company - RLDCen_US
dc.subjectKuku wa asilien_US
dc.subjectKukuen_US
dc.subjectBiasharaen_US
dc.titleBaiashra ya ufugaji bora wa kuku wa asili: kitabu cha mwongozoen_US
dc.typeBooken_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
ufugaji-bora-wa-kuku-wa-asili.pdf
Size:
1.03 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections