Kanuni 10 za Kilimo Bora cha Pamba
| dc.contributor.author | Wizara ya kilimo | |
| dc.date.accessioned | 2026-10-16T06:49:38Z | |
| dc.date.available | 2026-10-16T06:49:38Z | |
| dc.date.issued | 2024 | |
| dc.description | Kipeperushi | |
| dc.description.abstract | Pamba ni zao muhimu la kimkakati na biashara nchini, linachangia takriban asilimia kati ya 10 na 20 ya pato la taifa la fedha za kigeni, linatoa ajira kwa karibu asilimia 40 ya Watanzania wote walio ndani ya mnyororo wa thamani na chanzo cha malighafi kwa viwanda vya nyuzi, nguo na mafuta. Uzalishaji wa pamba hutekelezwa Kanda ya Magharibi na Kanda ya Mashariki. Pamba kwa Kanda ya Magharibi huzalishwa katika mikoa kumi na mbili (12) ambayo ni Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Tabora, Mara, Kagera, Katavi, Kigoma, Singida, Manyara na Dodoma na uzalishaji ni zaidi ya asilimia 98.Aidha pamba huzalishwa Kanda ya Mashariki katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Iringa, Kilimanjaro na Tanga ambapo uzalishaji ni chini ya asilimia 2. Ili kuongeza tija na ubora wa pamba, mkulima anatakiwa kuzingatia kanuni za kilimo bora cha Pamba kama ifuatavyo; tayarisha shamba mapema, tumia mbolea ya samadi na virutubisho vingine, panda pamba mapema, panda kwa mistari na kwa nafasi maalum, panda idadi halisi ya mbegu katika kila shimo, punguza miche, palizi kwa wakati na kunyunyizia viuadudu kuzuia wadudu waharibifu . | |
| dc.identifier.uri | https://www.mkulima.sua.ac.tz/handle/123456789/1047 | |
| dc.language.iso | other | |
| dc.publisher | Bodi ya pamba Tanzania | |
| dc.subject | Pamba | |
| dc.subject | Mbolea | |
| dc.subject | Mbegu | |
| dc.title | Kanuni 10 za Kilimo Bora cha Pamba | |
| dc.type | Other |