Usindikaji na Masoko

Permanent URI for this collection

Browse

Recent Submissions

Now showing 1 - 20 of 56
  • Item
    Tunamuunganisha Mkulima na mnunuzi Kupitia vyama vya ushirika ili kupata bei nzuri.
    (Tume ya maendeleo ya ushirika., 2023-08-12) Tume ya maendeleo ya ushirika.
    Tume kupitia Ushirika imefanikiwa kuboresha maisha ya wananchi kupitia shughuli wanazozifanya zinazowaingizia kipato kwa muunganiko wa Ushirika. Kwa mfano, wakulima wameweza kulipwa fedha zao za mazao kwa uharaka baada ya kuuza mazao yao kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala. Tume imeendelea kufanya Usimamizi thabiti wa Vyama vya Ushirika ambao umechangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la Pato la Taifa. Mfano, kati ya mwaka 2019/2020 hadi 2021/2022 jumla ya Tani 9,804,347 za mazao ya kimkakati ziliuzwa kupitia Vyama vya Ushirika, na jumla ya Shilingi 2,917,816,152,983.61 zililipwa kwa wakulima. Vilevile, Serikali inakusanya tozo na kodi mbalimbali kupitia Mamlaka zake zikiwemo Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Vyama vya ushirika. Mfano, Serikali katika mwaka 2021/2022 ilipokea jumla ya Shilingi 15,144,077,319.16 zikiwa ni fedha za ushuru unaotokana na zao la korosho uliolipwa na vyama vya TANECU, MAMCU, RUNALI, LINDI MWAMBAO, TAMCU na CORECU. Vilevile, jumla ya Shilingi 1,041,957,051.00 zimepokelewa kama ushuru kutoka katika Vyama vya Ushirika vya KDCU na KCU kupitia zao la kahawa. Viwanda Vidogo, vya Kati na Vikubwa 279 vimeanzishwa nchini kupitia Mfumo wa Uendeshaji wa Vyama vya Ushirika. Katika Msimu wa 2022/2023 Vyama Vya Ushirika vilitumia jumla ya Shillingi 397,706,245,786 kununua pembejeo za kilimo kwa ajili ya wakulima wa zao la Korosho, Kahawa, Tumbaku na Pamba. Tume pia kupitia Vyama vya Ushirika imeendelea kuratibu masoko na biashara ya zao la Ufuta nchini ambapo katika msimu wa 2022/2023 jumla ya kilo 79,170,426 zenye thamani ya Shilingi 245,130,400,328.00 zimeuzwa kupitia ushirika katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na Songwe na kuwezesha Halmashauri zake kupata ushuru wa zao wenye thamani ya Shilling 6,022,450,313.00 Tume vilevile inasimamia Vyama vya Ushirika vya Kifedha (SACCOS) ambapo hadi kufikia mwaka 2021 kabla ya kuanza kutekeleza Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha kulikuwa na SACCOS 3,831 zenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.6 na Akiba ya Shilingi Bilioni 803 pamoja na Amana za Shilingi Bilioni 149.2. Baada ya usajili mpya kwa mujibu wa Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha, hadi kufikia mwezi Novemba, 2022 kuna jumla ya SACCOS 743 zenye wanachama 1,731,237 wenye Amana za Shilingi Bilioni 713.6, Mali za Shilingi Bilioni 945.3 na Hisa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 149.2. Kutokana na mafanikio yanayopatikana, Vyama vya Ushirika chini ya usimamizi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika vinafanya kazi nzuri ya kukuza kipato na uchumi wa wananchi. Kwa hiyo, Watanzania walioko katika sekta zote wanaendelea kuhimizwa kujiunga katika Vyama vya Ushirika ili waweze kuinua uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla. Endelea kupata elimu, habari na matukio mbalimbali ya Ushirika kupitia Jarida hili. Karibu sana
  • Item
    Mbolea yetu
    (Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania, 2023-06) Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania
    Maelfu ya wakulima walionufaika na mpango wa ruzuku ya mbolea kwa msimu wa 2022/2023 wana hadithi ndefu ya kuwasimulia wenzao ambao hawakubahatika kujiunga na mpango huo. Mpango huu wa ruzuku ya mbolea umebuniwa na serikali ili kuimarisha sekta ya kilimo na kuchochea ongezeko la pato la taifa na hatimaye kuwatajirisha wakulima ambao kwa miongo mingi walishindwa kupiga hatua za maana katika ustawi wao. Katika Tanzania zimepita kampeni nyingi zilizolenga kuimarisha kilimo tangu kupatikana kwa uhuru zaidi ya miaka 60 iliyopita. Nyingi ya kampeni hizo zilifanikiwa kuleta hamasa miongoni mwa wakulima ili waongeze tija katika uzalishaji wa mazao mbalimbali. Hata hivyo, kwa bahati mbaya kampeni hizo hazikuwa endelevu kiasi cha kuwakwamua wakulima waondokane na umaskini. Ndiyo maana katika kukifanya kilimo chetu kiwe endelevu na kilete tija kwa wakulima serikali imebuni mpango huu wa ruzuku ya mbolea ili kuzalisha chakula kwa wingi na kupata malighafi viwandani kwa bidhaa zitokanazo na juhudi za wakulima wanaounda uti wa mgongo wa uchumi wa taifa. Ni jambo la kutia moyo kwamba baada ya kubaini mafanikio yatokanayo na mpango huu wa ruzuku ya mbolea kwa msimu wa 2022/2023 serikali kwa kauli moja imeamua kuuendeleza kwa misimu mingine “kuanzia 2023/2024 hadi 2025/2026.” Sasa hivi kinachosuburiwa ni maelekezo ya serikali jinsi mpango huu utakavyotekelezwa kwa misimu hiyo miwili. Nia ya serikali ni kuwawezesha mamilioni ya wakulima wazidi kunufaika na ruzuku ya mbolea ili kuchochea kukua kwa uchumi wa taifa. Vyama vya ushirika vilivyozagaa nchi nzima ni lazima vijipange kikamilifu katika utekelezaji wa mpango huu huko vijijini. Ni jukumu la serikali za mitaa huko vijiijini zisaidie usimamizi wa bei elekezi ya mbolea kwa kila kituo kutegemeana na mazingira halisi ya sehemu inayohusika. Tunatarajia kwamba vituo vya mauzo ya mbolea vikiwa karibu na wakulima, kundi hilo la wachapa kazi wa Tanzania litahamasika zaidi katika kutumia mbolea ili kukuza uzalishaji. Kampeni hii ya ruzuku ya mbolea ni lazima iote mizizi katika ngazi zote kuanzia vitongoji, vijiji, kata na tarafa – maeneo ambayo kuna idadi kubwa ya wananchi. Viongozi wa ngazi zote kuanzia vijiji hadi taifa ni lazima wasimame kidete kuhakikisha kampeni hii inafanikiwa kwa sababu imebuniwa kumkomboa mkulima wa Tanzania katika karne hii inayoshuhudia maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia. Miaka ya mwanzo ya uhuru, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, altuasa kutimiza wajibu wetu ili kujiletea maendeleo. Kwa sasa hamasa hii ni lazima ihamie kwa wakulima kwa kuwataka wajisajili kwa wingi ili waweze kufaidi matunda ya ruzuku ya mbolea. Kwa njia hiyo watakuwa wanapiga vita umaskini na kubadili hali zao za maisha. Ni vizuri kwa Watanzania kuchangamkia fursa kama hizi zinazotolewa na serikali ambazo zinalenga kubadili maisha yao baada ya miongo mingi ya kuelea kwenye dimbwi la umaskini.
  • Item
    Unafuu wa mbolea za ruzuku.
    (Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania, 2023-09) Mamalaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania
    Katika harakati za kuimarisha kilimo, serikali ya Tanzania mwaka jana ilitenga shilingi bilioni 150 kama ruzuku ya mbolea kwa wakulima kuwasaidia waongeze uzalishaji na kupunguza makali ya bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia, hasa baada ya kuzuka kwa vita kati ya Urusi na Ukraine. Kwa mujibu wa Dkt. Ngailo, katika siku za usoni Tanzania itakuwa kitovu cha mbolea barani Afrika kama mikakati ya sasa iliyobuniwa na serikali ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya mbolea itakwenda kama ilivyopangwa. Hivi sasa Tanzania inashuhudia kasi ya ujenzi wa viwanda vya mbolea ili kukidhi mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo katika sekta ya kilimo. Nia ya kasi ya ujenzi wa viwanda vya mbolea ni kuwapunguzia wakulima bei ili mbolea ipatikane kwa urahisi kwa kuwafikia wakulima hao mahali walipo. Lengo jingine la kuwavuta wawekezaji katika ujenzi wa viwanda ni kuwa na soko linaloaminika la bidhaa hiyo kwa nchi jirani za Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika pamoja na mataifa mengine ya Ulaya ambayo yamekuwa yakiiagiza mbolea kutoka kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara. Mahitaiji ya mbolea kwa wakulima wa Tanzania katika miaka ya karibuni yameongezeka kutoka tani 42,000 mpaka tani165,000 baada ya kuwepo kwa jitihada za kuwaelimisha wakulima kutumia mbolea ili waongeze tija katika mashamba yao, kwamujibu wa Bole. Ni faraja kwamba ongezeko la matumizi ya mbolea limezaa matunda baada ya kushuhudia ongezeko la uzalishaji wa chakula kutoka tani milioni 17 hadi kufikia tani milioni 20, anaeleza Dkt. Ngailo. “Kazi ya kuwaelimisha wakulima kutumia mbolea ni suala endelevu kwa kushirikiana na serikali za mitaa. Kuna uwezekano mkubwa kwa wakulima wengi Tanzania kutumia mbolea na hatimaye kulilisha bara la Afrika,” anaeleza Dkt. Ngailo. “Ruzuku ya mbolea imesaidia sana wakulima kununua mbolea kwa wingi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.’ Dkt. Ngailo anaeleza kuwa ongezeko la matumizi ya mbolea miongoni mwa wakulima limewapa viongozi ari ya kujiamini kwamba Tanzania katika miaka michache ijayo itafikia lengo lake la kulisha bara zima la Afrika kutokana na ziada ya chakula kinachozalishwa. “Inawezekana kwa Tanzania kulisha Afrika na dunia nzima. Tuna uwezo wa kuzalisha chakula cha ziada kukidhi mahitaji ya Afrika na dunia nzima,” anasema kwa kujiamini , huku akiungwa mkono na mchumi mwandamizi wa TFRA, Elizabethi Bole. Kwa dhamira ya Tanzania kujitosheleza kwa chakula na kuwa ghala la kuaminika kwa Afrika na dunia nzima, mkutano wa 13 wa Jukwaa la Chakula Afrika 2023 utakuwa na mambo mengi ya kujionea ambayo yatafaa yaigwe na mataifa mengine kuwa fundisho. Kama alivyosema Dkt. Stephan Ngailo, dunia itakuja Tanzania kushuhudia yaliyopo na itaondoka na mafunzo kwenda kuyapandikiza sehemu nyingine; na hivyo kuliuza jina la Tanzania ughaibuni.
  • Item
    FAHAMU KUHUSU BIASHARA YA MKONGE NCHINI TANZANIA NA CHANGAMOTO ZAKE
    (Jamii Forum, 2017-01) Jamii forum
    Mkonge au Katani ni moja kati ya zao la biashara Jina la kisanyansi inaitwa Agave sisalana. Asili ya zao hili ni Mexico na baadae likasambaa katika nchi nyingine, kwa mara ya kwanza lilitambushwa katika nchi za kitropikia na subtropikia India,Tanzania, Brazil, Kenya south Africa, Angola, Mozambique Morocco Uganda, Zimbabwe na Mauritius. Zao la mkonge liliingizwa nchini mwaka 1892 na mtaalamu wa kijerumani Dr. Richard Hindorff ambaye alikuwa ni mtafiti wa mimea na udongo. Mtaalamu huyo alichukua miche 1000 kutoka Pwani ya Mexico kwenye jimbo la Yuctan na kuisafisha kwa kupitia Frolida, Marekani na Humburg Ujerumani. Kati ya miche 1000, ni miche 62 tu ndiyo iliyofika Tanganyika na ilipandwa sehemu iitwayo Kikokwe huko Pangani Tanga. Mkonge ulisambaa maeneo mengi ya Tanganyika mpaka kufikia mwanzoni mwa miaka 1960 Tanganyika ilikuwa inaongoza kwa uzalishaji wa mkonge ikifatiwa na Brazil na mexico kwa mauzo ya tani 230,000 kwa mwaka nje ya nchi. Kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza miaka ya 1970 uzalishaji ulipungua toka tani 230,000 hadi tani 19,700 kwa mwaka 1997. Hata ivyo mageuzi ya kiuchumi yaliyoanza miaka 1980 ambayo yalilenga katika ubinafisishaji na biashara huria , uhuru wa taasisi za kifedha za ndani na nje ya nchi yalifufua kilimo cha mkonge na hasa kukamilika kwa ubinafishaji mwaka 2005 uzalishaji umepanda hadi kufikia tani 40,000 mwaka 2015 hii inatokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mkonge na bidhaa zake pamoja na kupanda bei kwenye soko la dunia pamoja na ndani. Soko kuu la mkonge wa Tanzania ni china, Saudi Arabia , India, Uhispania, Ujerumani, Uingereza, Kenya, Uganda na Nigeria.
  • Item
    Kilimo bora cha pilipili kichaa
    (Mjasiriamali Hodari, 2020-01) Mjasiriamali Hodari
    Zao la Pilipili kichaa 'Hot pepper' au 'Chilli pepper' (Capsicum frutescens) hulimwa maeneo mengi ulimwenguni ikiwemo nchini Tanzania. Matunda ya pilipili hutumika kwa matumizi mbali mbali kama chakula au kama tiba (medicinal properties) na kuimarisha afya ya mraji. Kwa upande wa chakula pilipili hutumika kama kionjo cha vyakula mbalimbali kama Supu, kachumbali, nyama choma, nyama rosti, maharage, mboga za majani, kutengenezea chilli sauce n.k. Kwenye chakula pilipili huongeza radha maridhawa kabisa, ndio maana mtu aliyezoea kula vyakula vyenye pilipili huwa hafurahii chakula kisichokua na pilipili. Kwa upande wa tiba pilipili/pilipili kichaa ina vitamini nyingi (Capsaicin compounds) ikiwemo niacin, pyridoxine, riboflavin, na thiamine n.k. Uwepo wa vitamini hizi pilipili hutumika katika kutengenezea madawa (Ointment) ya kuondoa maumivu ya viungo na misuli. Kufahamu faida nyingi za kiafya za kutumia pilipili.
  • Item
    Kifahamu kilimo cha maua
    (Jamii Forums, 2016-10-13) Jamii Forums
    Kilimo cha maua ni sayansi au sanaa ya kukuza matunda, mboga mboga, maua, au mimea ya mapambo. ). Wafanyabiashara wa maua wanafahamu sana katika uwanja huu, lakini ufafanuzi wake kamili ungeenea zaidi ya kile tunachofikiri kawaida kama bustani au kilimo.
  • Item
    Utaratibu wa kuuza na kununua zao la dengu kupitia soko la bidhaa Tanzania (TMX)
    (Soko la bidhaa Tanzania (TMX), 2020-09-04) Malekano, Godfrey
    Zao la dengu ni moja ya mazao muhimu katika kuinua pato la mkulima nchini Tanzania, hivyo katika msimu wa202012021, Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) kwa kushirikiana na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) pamoja na uongoziwa mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Manyara na halmashauri zake husika zitasimamia uendeshaji wa minada ya dengu katika ghala zinazotumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala. Mauzo hayo yanalenga kuleta bei zenye ushindani wa haki, uwazi na kupunguza gharama za ununuziwa zao la dengu.
  • Item
    Elimu ya Ujasiriamali: Kuelekea kwenye Maendeleo Endelevu Tanzania
    (Haki Elimu, 2021) Muhura, Chiraka
    Nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa mfano, zimejaliwa raslimali ambazo zinaweza kub- adilishwa kuwa mali. Lakini suala ni jinsi ya kuzigeuza raslimali hizo ili kuwa vitu halisi. Elimu isiyofaa imeelezwa kuwa ndiyo kikwazo kikubwa kinachokwamisha kuzibadilisha raslimali hizo kuwa vitu halisi. Elimu ya Tanzania inasemekana kuwa ni elimu inayowaandaa watu kuwa waajiriwa wa maofsini, japokuwa nafasi za kazi ni chache ukilinganisha na idadi ya watu wanaotafuta kazi za kuajiriwa. Kwa ufupi, elimu yetu haijengi ubunifu na udadisi ambao ungewawezesha watu ama kujiajiri (ujasiriamali) au kuzipanua fursa za ajira ambazo zingewawezesha watu wengi kupata ajira. Fursa za ajira hazijatumiwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuweza kuwachukua watu wote wenye sifa za kuajiriwa. Chapisho hili kwa hiyo linaibua jinsi elimu ya ujasiriamali inavyoweza kuibadilisha nchi kutoka kwenye utegemezi na kuwa nchi yenye kujitegemea.
  • Item
    Job market surveys, training needs assessment and tracer studies for SUA undergraduate programmes.
    (SUA, 2008-06-25) PANTIL
    Sokoine University of Agriculture (SUA) through the FOCAL (Future Opportunities and Challenges in Agricultural Learning) Programme in 2005 commissioned studies to survey job markets, assess training needs and conduct tracer studies in relation to the current and future employment opportunities. The aim was to provide SUA with evidence of the required labour market demands hence training needs in terms of methods, contents and skills required. In order to facilitate the exercise, thirteen degree programmes were grouped into five agricultural and natural resources fields (clusters). Four firms were assigned consultancy works in the five clusters. These firms were: i) K-Rep Advisory Services (Cluster No. I), ii) Agrisystems (EA) Ltd (Cluster No.2), iii) Development Associates Ltd (Cluster No.3 & 4) and iv) Afrozone Ltd (Clusters No 5).
  • Item
    Usimamizi wa fedha
    (2015) Lyimo-macha, Dk.J.G; Malimbwi, Prof R. E; Kiranga, Bw.E.; Kawamala, Bw.P
    Katika kitabu cha bajeti ambacho ni cha kwanza katika seti hii ya USIMAMIZI WA FEDHA ulijifunza jinsi ya kutayarisha bajeti Uliona kuwa matayaisho ya bajeti ni hatua ya kwanza ya kupanga matumizi ya fedha za mradi ili kupata mafanikio katika utekelezaji.bajeti ni mpango wa matumizi ya fedha za mradi. bila kuwa na bajeti kikundi hakiwezi kujua kuwa mradi utaweza kutekelezwa kwa sababu ya gharama halisi za mradi hazitafahamika
  • Item
    Teknolojia za hifadhi usindikaji, na matumizi ya mazao ya mikunde baada ya kuvuna
    (Wizara ya Kilimo na Chakula., 2003-08-07) Jamhuri ya Muungano wa T anzania, Wizara ya Kilimo na Chakula
    Mazao jamii ya mikunde yanayolimwa hapa nchini ni maharage, soya, kunde na mbaazi. Sifa kubwa ya mazao haya ni kuwa na kiwango kikubwa cha protini nyingi na uwezo wa kuongeza naitrojeni kwenye udongo. Uzalishaji wa mazao haya ni wastani wa tani 490,000 kwa mwaka. (Takwimu, Wizara ya Kilimona Chakula) Hata hivyo kiasi kikubwa cha mazao hayo hupotea baada ya kuvuna. huu husababishwa na matumizi ya mbinu duni katika uvunaji, ukaushaji, usafirishaji, usindikaji na hifadhi. Kiasi kikubwa cha mikunde hupotea wakati wa kuvuna kutokana na kuchelewa kuvuna ambapo mapodo hupasukia shambani. Hali hii huruhusu mashambulizi ya wadudu waharibifu kwa urahisi na punje nyingi kuachwa shambani. Katika uvunaji, mazao mengi hupotea kwani mbinu zinazotumiwa na wakulima bado ni duni na za kuchosha, hivyo mazao mengi huachwa shambani.
  • Item
    Masoko ya mazao ya kilimo
    (Sokoine university of A griculture, 2020-05-20) Mtega, Wullystan
    Mkulima anatakiwa kutafuta soko la mazao yake kabla hajaanza shughuli ya uzalishaji shambani. Ili kupata taarifa za kutosha, mkulima anashauriwa kufanya utafiti wa soko. Mkulima anaweza tumia njia kuu mbili: (i) kuandaa dodoso na kuwauliza wadau muhimu wa soko la zao alilozalisha na, (ii) kutembelea masoko ya mazao na kukusanya taarifa kwa njia ya kuona. Utafiti wa soko humwezesha mkulima kutoa maamuzi sahihi juu ya uuzaji wa mazao yake. Katika kuuza mazao, mkulima lazima azingatie sheria, kanuni na taratibu za nchi na soko husika. Pia, ni muhimu kuelewa namna nguvu ya soko inavyofanya kazi. Hii itamsaidia mkulima kujua lini ayapeleke mazao sokoni na hivyo kupata bei nzuri zaidi
  • Item
    Utunzaji na uhifadhi wa nafaka ya mahindi
    (Emanueli Mabula, 2020-07-16) Mabula
  • Item
    MICHAKATO YA KUHIFADHI VYAKULA MBALIMBALI KWA KUKAUSHA.
    (Kilimo foram, 2017-05-12) Denis, Marco,D.
    Wakulima wengi huingia hasara kubwa pale mazao yao yanapoharibika kwa kukosa masoko. Kufahamu michakato ya ukaushaji mazao utawawezesha kuyaweka katika hali ya kutoharibika na hivyo kuweza kutumiwa kwa muda mrefu. Pia ukaushaji huwezesha vyakula kutumika kwa muda mrefu bila kuharibu ladha na ubora wake. Ukaushaji wa vyakula mbalimbali hutumiwa na wakulima wengi kama njia mojawapo ya kuepusha uharibifu wa mazao na kuviwezesha kutumika kwa muda mrefu. Yafuatayo ni maelezo ya michakato mbalimbali inayotumika kuvikausha vyakula hivyo.
  • Item
    Usindikaji wa ndizi
    (Muungwana blog, 2016-01-22) Denis, Marco D.
    Siku zote usipokuwa na juhudi na maarifa maisha ni magumu sana, lakini unapojituma na kutokukata tamaa, ni wazi utapata mafanikio. Jambo la msingi ni kujifunza mambo mbalimbali na kutenda kwa vitendo. Ndivyo alivyoanza kueleza Penina ambae ni msindikaji wa ndizi kutoka kijiji cha Nndatu wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha. Penina anaeleza kuwa, alianza usindikaji wa ndizi mwaka 2013, baada ya kuhudhuria semina ya usindikaji kutoka katika shirika lisilo la kiserikali la TeMdo. Anaeleza kuwa alifikia uamuzi wa kutafuta utaalamu wa kusindika ndizi, baada ya kuchukizwa na hali ya wakulima kupata hasara iliyotokana na ndizi kuoza na kutupwa msimu ambayo upatikanaji wake ni mkubwa. Pia uhitaji wa ndizi kavu kutoka kwa makundi mbalimbali kulishawishi zaidi kutafuta njia za kisasa za kufanya kazi hiyo.
  • Item
    Usindikaji wa bidhaa za viazi vitamu rangi ya chungwa (yellow sweet potatoes)
    (2016-06-05) Denis, Marco D.
    Leo hebu tuongelee kuhusu Usindikaji wa viazi hivi na bidhaa mbalimbali kutokana na viazi vitamu rangi ya chungwa. Lakini kumbuka kwamba lazima uzingatie kiwango cha Carotene kisipotee. Ili Kuhifadhi kiwango cha karotini, fanya yafuatayo kabla hujaanza kusindika:- – Sindika kwa haraka – Visindike vikiwa na maganda – Usihifadhi viazi vitamu rangi ya chungwa kwa muda mrefu.
  • Item
    Jinsi ya kuhifadhi chakula vizuri kwa muda mrefu
    (2020-05) Fam Radio Internationa, Fam Radio Internationa
    Kutokana na kuzuiwa watu kutembea katika nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa sababu ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19), masoko mengi ya vyakula halisi yamefungwa au kuzuiwa. Hii inathiri wachuuzi, wafanyabiashara, na watumiaji. Wakati, hadi sasa, minyororo ya thamani ya nafaka na kunde haijaathiriwa sana, watumiaji hawawezi kupata chakula halisi kwa ajili ya familia zao, haswa matunda na mboga, maziwa, na nyama. Vyakula hivi vinaweza kuharibika na, bila njia bora za kuweza kuzihifadhi na kubaki katika uhalisia vinaweza kuoza haraka. Ni vigumu kusisitiza sana umuhimu wa kula vyakula halisi. Matunda na mboga ni chanzo kingi na kisicho ghali cha nishati, virutubisho vya kujenga mwili, vitamini, na madini. Thamani yake kama lishe ni kubwa yanapokuwa halisi, lakini matunda na mboga nyingi hukaa katika hali ya uhalisi kwa muda mfupi sana, isipokuwa ikiwa yamehifadhiwa haraka na vizuri baada ya kuvunwa. Katika nchi ambazo vyakula halisi vinapatikana tu katika kipindi fulani cha mwaka, watu wametengeneza njia tofauti za kuhifadhi na kuongeza muda wa vyakula kubakia kuwa halisi ili viweze kuliwa wakati wa kipindi ambacho vyakula halisi havipatikani. Njia hizi ni muhimu sana kwa wakulima, wachuuzi, na wasindikaji. Vyakula halisi kwa kawaida huoza isipokuwa pale vinaposindikwa kwa njia fulani au kuhifadhiwa katika hali maalum. Mchakato wa kuoza ni kwa sababu ya vitendo vya viumbe-vidogo vinavyopatikana kwenye vyakula hivyo. Lakini kuoza kunaweza kupunguzwa kwa kuongeza uhifadhi, kusindika vyakula, na kutumia njia bora za uhifadhi. Matunda na mboga zinapaswa kutayarishwa kuhifadhiwa haraka iwezekanavyo baada ya kuvuna, ndani ya masaa 4 hadi 48. Uwezekano wa kuharibika huongezeka haraka kadiri wakati unavyopita.
  • Item
    MATATIZOYA MASOKO YA MAZAO YA WAKULIMA - Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki Iliyofanyika VETA Tanga 24-26 Juni 2002
    (TARP II-SUA Project, 2002-06) Razack, O. M; Lyimo-Macha, J. G
    Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo, kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na pia kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na ., washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya Wakulima waKanda ya Mashariki Kuhusu Matatizo ya Masoko ya Mazao ya Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa VETA, Tanga, tarehe 24-26 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Item
    MATATIZO YA MASOKO YA MAZAO YA WAKULIMA - Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Iliyofanyika Kituo cha Anglikana, Iringa Juni 6-8, 2002
    (TARP II-SUA Project, 2002-06) Msangi, R. O; Malimbwi, R. E
    Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo, kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji ushirikishwaji wa wadau wote kwa lengo la kufanikisha kilimo 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogo wadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Kuhusu Matatizo ya Masoko ya Mazao ya Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Anglikana, Iringa, tare he 6-8 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Item
    Mihogo - njia bora za ukaushaji na usindikaji
    (Mitiki Blogspot, 2009-12)
    Mihogo mibichi iliyovunwa huoshwa mara mbili. Uoshaji wa kwanza ni ule wa kuondoa udongo baada ya kuvuna, na uoshaji wa pili ni baada ya kumenya mihogo kabla ya kukausha.Baada ya kuoshwa mihogo humenywa kwa kutumia kisu kikali, na kutumbukizwa ndani ya maji safi. Baada ya kumenya kiasi kinachotakiwa mihogo huoshwa na maji safi hadi kuwa myeupe.