UENDELEZAJI WA VIKUNDI VYA WAKULIMA KANDA YA MASHARIKI - Warsha ya Nane ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki Iliyofanyika Ukumbi wa CCM, Lushoto, Tanga - 21-23 Juni 2004
Loading...
Date
2005
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
TARP II-SUA Project
Abstract
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na
Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), na Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa
Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima
Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi
mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway.
Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya
mradi na kuimarisha uhusiano na wakulima, watafiti na washauri
wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo:
• Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo
ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji
kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo
na ufugaji
• Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili
wakulima wadogowadogo
• Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au
kipaumbele
• Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya
kilimo na mifugo.
Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya nane ya
wakulima wa Mikoa ya kanda ya Mashariki kuhusu Uendelezaji
wa Vikundi vya Wakulima iliyofanyika ukumbi wa CCM,
Lushoto, Tanga, 21-23, Juni 2004. Mwenendo wa warsha
umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na
Kiingereza.
Description
Keywords
Ushirika, Vikundi