Jinsi wakulima hukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Loading...
Thumbnail Image

Date

2009-12

Authors

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Farm Radio International - FRI

Abstract

Kujifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu kwa wakulima kwa sababu ya athari wanayoweza kuwa nayo kwenye kilimo. Wakulima wanaweza kutarajia kiasi cha joto kilichopanda na dhoruba za mara kwa mara, mafuriko na hali za ukame. Hali ya hewa itakuwa inabadilikabadilika zaidi na hivyo ngumu kutabiri. Wakulima wanahitaji kuelewa mabadiliko ya hali ya hewa na anga ili kufanya mipango kuhusu mavuno yanayobadilika na tofauti, ukosefu wa maji, na uwezekano wa ongezeko la wadudu waharibifu na magonjwa. Makala haya yanatoa habari msingi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa itakayokusaidia kutayarisha vipindi vya redio kuhusu mada hii. Unavweza kuwaambia wakulima katika eneo lako kuhusu njia kadhaa ambazo kwazo, mabadiliko ya hewa huwaathiri wakulima. Kisha unaweza kujadili mikakati ambayo wakulima wa eneo hilo wanaweza kutumia ili kufanikiwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ongea na wakulima ili uelewe changamoto yao imekuwa nini kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa. Je, wamepata njia mpya, au kutumia njia za jadi zinazowasaidia kukabiliana na hali hii mpya.

Description

Keywords

Mazingira, Hali ya hewa, Kilimo

Citation