Tathmini ya Hali ya Lishe, Unasihi na Huduma za Lishe (NACS) - KITABU CHA MWEZESHAJI Mafunzo kwa Watoa Huduma katika Ngazi ya Jamii

dc.date.accessioned2019-02-19T07:07:46Z
dc.date.available2019-02-19T07:07:46Z
dc.date.issued2017
dc.description.abstractLishe ina uhusiano mkubwa na afya. Lishe duni au utapiamlo unaotokana na ulaji duni na maradhi ni mojawapo ya matatizo makubwa ya afya nchini Tanzania. Utapiamlo unawaathiri zaidi watoto wenye umri chini ya miaka mitano na akina mama walio katika umri wa kuzaa hasa wajawazito na wanaonyonyesha. Utapiamlo kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha unaweza kusababisha madhara ya muda mrefu kwa watoto wao. Pia, utapiamlo unahusishwa na magonjwa sugu kama vile kifua kikuu (TB) na UKIMWI, ambayo ni matatizo makuu hapa nchini Tanzania. Upungufu wa lishe katika kipindi cha miaka miwili (siku 1,000) ya mwanzo ya maisha ya mtoto unahusishwa na maradhi, vifo na uchelewaji wa ukuaji wa mwili na maendeleo ya akili. Upungufu huo unaweza kuathiri utendaji wa akili, matokeo ya uzazi, afya na tija ya kiuchumi wakati wa utu uzima. Watoto wachache tu wenye utapiamlo pamoja na watu wazima wametambuliwa na kutibiwa kwa kupitia vituo vya kutolea huduma ya afya. Lakini wengi wa watu hawa wakisha ruhusiwa toka vituo vya kutolea huduma ya afya baada ya kutibiwa utapiamlo huwa hawarejei tena kwa ajili ya ufuatiliaji. Watoa huduma katika ngazi ya jamii watasaidia katika kuimarisha utoaji wa huduma kati ya vituo vya kutolea huduma ya afya na jamii ili watu wenye utapiamlo waweze kutambuliwa, kutibiwa na kufuatiliwa mapema na hivyo kuboresha hali zao za lishe, kugundua dalili za utapiamlo mapema na kuepuka maambukizi. Shughuli hizi zitaimarisha mwendelezo wa utoaji wa huduma kati ya vituo vya kutolea huduma ya afya na jamii.en_US
dc.identifier.isbn978-9976-910-93-3
dc.identifier.urihttp://10.10.11.5/handle/123/448
dc.language.isootheren_US
dc.publisherTaasisi ya Chakula na Lishe Tanzaniaen_US
dc.subjectLisheen_US
dc.subjectChakulaen_US
dc.subjectAfyaen_US
dc.titleTathmini ya Hali ya Lishe, Unasihi na Huduma za Lishe (NACS) - KITABU CHA MWEZESHAJI Mafunzo kwa Watoa Huduma katika Ngazi ya Jamiien_US
dc.typeBooken_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Tanzania-Community-NACS-Facilitators-Guide-2017.pdf
Size:
4.06 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections