Ongeza maziwa na upunguze gharama kwa kulisha mifugo kaliandra

dc.contributor.authorLyamchai, C. J
dc.contributor.authorKweka, E. S
dc.contributor.authorMwikari, M. M
dc.contributor.authorKingamkono, M. N
dc.contributor.authorWambugu, C
dc.date.accessioned2018-02-23T10:34:04Z
dc.date.available2018-02-23T10:34:04Z
dc.date.issued2005
dc.description.abstractKaliandra (Calliandra calothyrsus) ni mmea aina ya mikunde wenye asili ya Amerika ya Kati na Mexico. Ulipandwa mara ya kwanza nchini Indonesia kwa ajili ya kivuli katika mashamba ya kahawa, lakini kwa sasa mti huo umeonyesha faida zaidi kwa kutumika kama chakula cha mifugo, kuni na kuhifadhi udongo. Katika nchi nyingi ikiwemo Kenya, Tanzania na Uganda, Kaliandra hutumika kama lishe ya ng’ombe wa maziwa na mifugo wengine. Kaliandra ina kiasi kikubwa cha protini (asilimia ishirini hadi ishirini na tano) na huchanganywa na aina nyingine za majani yenye kiwango kidogo cha protini kama vile matete au majani tembo (Napier kwa Kiingereza) ili kuongeza lishe kwa mifugo, uzalishaji wa maziwa na kiasi cha mafuta katika maziwa. Ijapokuwa Kaliandra haichavulishwi na nyuki, imekuwa chanzo kikubwa cha asali. Nchini Indonesia, nyuki wameweza kutengeneza kilo elfu moja ya asali kwa mwaka kutoka ekari mbili za shamba iliyopandwa Kaliandra. Faida zingine ni kuboresha uchavushaji wa kahawa na kuni ambazo hukauka vizuri na kuwaka kwa urahisi.en_US
dc.identifier.urihttp://10.10.11.5/handle/123/113
dc.language.isootheren_US
dc.publisherWorld Agroforestry Centre - ICRAFen_US
dc.subjectKaliandraen_US
dc.subjectNg'ombeen_US
dc.subjectMaziwaen_US
dc.subjectChakula cha mifugoen_US
dc.subjectCalliandra calothyrsusen_US
dc.titleOngeza maziwa na upunguze gharama kwa kulisha mifugo kaliandraen_US
dc.typeBooken_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
le05155.pdf
Size:
1.88 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections