Browsing by Author "Kiranga, E"
Now showing 1 - 3 of 3
Results Per Page
Sort Options
Item MATUMIZI BORA YA ARDHI- Mafunzo kutoka Mlima Meru(Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania - TARP II - SUA Project), 2002-09) Lyimo-Macha, J. G; Malimbwi, R. E; Kiranga, E; Kawamala, PChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula (MAFS), pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo Wadogo Tanzania. Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya Wakulima, Watafiti na Wagani. IIi kufikia lengo hili, mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Makala hii inawasilisha mafunzo yatokanayo na ziara iliyofanyika Septemba 2002. Ziara hii iliwashirikisha wakulima na washauri wa wakulima kutoka Kanda ya Mashariki ikijumuisha wilaya za Kilosa, Handeni, Pangani, Mkuranga na Morogoro na kanda ya Nyanda za Juu Kusini ikiwajumuisha wakulima na wagani kutoka wilaya za Mbeya, Mafinga, Njombe, Mbinga na Mbozi ambao walitembelea wakulima wa wilaya ya Arumeru, Arusha walioshiriki katika rnradi wa SCAPA. Makala hii pia inapatikana katika lugha ya kiingereza.Item UENDELEZAJI WA VIKUNDI VYA WAKULIMA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI - Warsha ya Nane ya Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Iliyofanyika Ukumbi wa Allamano wa Vijana wa Kikatoliki Makambako, Njombe 7-9 Juni 2004(TARP II-SUA Project, 2004-06) Vallery, F; Kiranga, E; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLT-I), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula la Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania. Mradi huu arnbao ulianza rasrni mwczi Septernba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano na wakulima, watafiti na washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: I. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pandc zote kwa lengo la kufanikisha kilimo 11a ufugaji 2. Kucharnbua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutarnbua mambo gani yapewc uzito au kipaumbele 4. Kushiriki katika kupeana uzocfu wa maenco muhimu ya kilimo na mifugo. Chapisho hili linawasilisha rnwenendo wa warsha ya nane ya wakulima wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuhusu Uendelezaji wa Vikundi vya Wakulirna- iliyofanyika ukurnbi wa Allamano wa Vijana wa Kikatoliki, Makambako, Njombe, 7-9, Juni 2004. Mwenendo wa warsha umcchapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Item Ziara ya Mafunzo ya Wakulima - Vikundi vya Wakulima wa Wilaya ya Kongwa na Dodoma Vijijini(TARP II-SUA Project, 2004-06) Lyimo-Macha, R. E; Malimbwi, R. E; Kiranga, E; Kawamala, PChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya Wakulima, Watafiti na Wataalamu wa ugani. IIi kufikia lengo hili, mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Makala hii inawasilisha ripoti ya ziara mbili zilizofanyika mwezi Aprili na Mei 2004. Ziara hizi ziliwashirikisha wakulima na wataalamu wa ugani kutoka Kanda ya Mashariki ikijumuisha wilaya za Tanga, Pwani, Morogoro na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ikiwajumuisha wakulima na wataalamu wa ughani kutoka Iringa, Mbeya na Rukwa ambao walitembelea wakulima wa wilaya ya Dodoma vijijini na Kongwa, Mkoa wa Dodoma. Washiriki wengine walikuwa ni watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Taasisi za Utafiti wa Kilimo Mikocheni, Dar es salaam na Uyole, Mbeya na wakufunzi watatu toka INADES-Formation, Dodoma. Chapisho hili pia linapatikana katika lugha ya kiingereza.