Ziara ya Mafunzo ya Wakulima - Vikundi vya Wakulima wa Wilaya ya Kongwa na Dodoma Vijijini
Loading...
Date
2004-06
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
TARP II-SUA Project
Abstract
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na
Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), pamoja na Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa
Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo
Tanzania.
Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya
Wakulima, Watafiti na Wataalamu wa ugani. IIi kufikia lengo hili,
mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima
kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda.
Makala hii inawasilisha ripoti ya ziara mbili zilizofanyika mwezi
Aprili na Mei 2004. Ziara hizi ziliwashirikisha wakulima na
wataalamu wa ugani kutoka Kanda ya Mashariki ikijumuisha
wilaya za Tanga, Pwani, Morogoro na Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini ikiwajumuisha wakulima na wataalamu wa ughani kutoka
Iringa, Mbeya na Rukwa ambao walitembelea wakulima wa wilaya
ya Dodoma vijijini na Kongwa, Mkoa wa Dodoma. Washiriki
wengine walikuwa ni watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo, Taasisi za Utafiti wa Kilimo Mikocheni, Dar es salaam na
Uyole, Mbeya na wakufunzi watatu toka INADES-Formation,
Dodoma. Chapisho hili pia linapatikana katika lugha ya kiingereza.
Description
Keywords
Mafunzo, Wakulima