Mkulima
Permanent URI for this community
Browse
Browsing Mkulima by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 954
Results Per Page
Sort Options
Item KILIMO CHA MTAMA(20-03-13) KILIMO BLOGMtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya ukame kuliko mazao mengi ya jamii yake,Hivyo hulimwa maeneo mengi Duniani yenye mvua Pungufu na hata yenye mvua za kutosha.Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri husaidia kwa kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia katika vita ya kuzuia njaa.Mtama hutumika Kama vile unga wa ugali,kupikia mikate ya mtama,kupika ubwabwa wa mtama,Unaweza kuchemshwa na Kuliwa (mnyoma-lugha ya kiasili),Viwanda vya bia kutengeneza bia,Pia majani na mabua yake yanaweza kutumika kama chakula cha mifugo,na pia mabua Makavu yanaweza kutumika katika kujengaea uwa .Item Zijue taratibu za uzalishaji wa mbegu za viazi vitamu zilizothibitishwa ubora wake(Mradi wa Bioinnovate - ICOPSEA, 0209-07) Taasisi ya Utafiti wa Kilimo MikocheniViazi vitamu ni zao muhimu la chakula na lishe bora nchini Tanzania. Viazi vitamu vina wanga mwingi hivyo ni njia nafuu ya kuupatia mwili nguvu. Majani ya viazi vitamu hutumika kama mboga na hivyo ni chanzo cha vitamini na madini joto mwilini. Pia viazi vitamu ni chanzo cha kipato kwa familia na taifa.Item Udder diseases of diary cows(U. S. DEPARTMENT OF AGRICULTURE, 1961-05-08) Brown, Richard Y.T IlE DAIRY cow'S udder (fig. 1) has been highly developed by cen turies of careful, selective breeding. It is complex in its structure and physiology. The secretory tissue of the gland is made up of great numbers of alveoli or hollow balls composed of milk-secreting cells which are mi croscopic in size and grouped like clusters of grapes around the ducts (fig. 2). The milk is formed in the alveoli and travels down through the ducts to the gland cistern and teats. The size of the passageway through the teat is greatly reduced at its lower end. This constriction prevents escape of milk from the udder and acts as a barrier against entrance of micro-organisms. Each quarter of the udder is separate and milk is being continually secreted in active glands. Much of it, however, is only forced down.Item Halmashauri ya taifa ya mazao(Nuta Press, 1971) wizara ya kilimoKabla ya Tanzania kupata uhuru, serikaii ya kikoloni ilijiingiza sana katika mazao ya biashara na nchi za nje na haikujali sanajuu ya mazao yaliyotumika humu nchini hasa yale ya chakula ambayo wananchi hutumia. Siasa yao ya kikoloni wakati huo ilikuwa kuku- za mazao ambayo yangeuzwa na kukuza uchumi wa nchi zao. Siasa hiyo kwa kweli iliweza kuleta madhara kwa mazao ambayo yangetumika au kuliwa humu nchini, kwa hiyo upanuzi wa kilimo cha mazao machache kuliifanya Tanganyika kutesemea mazao kama katani na kahawa kuwa mazao makuu ya biashara na nchi za nje.Item Tomato disease control(NEW-MEXICO STATE UNIVERSITY COOPERATIVE EXTENSION SERVICE., 1971-08) Shannon, EmroyTomatoes are attacked by several disease organisms that reduce both yield and quality. Control of these diseases means the difference between profit and loss. Effective control consists of knowing what diseases you have and implementing an effective control program.Item Grasshopper control(Washington, D.C., 1973-05-08) Western Region, Agricultural Research ServiceGrasshoppers are found in every part of the United States, but serious outbreaks seldom develop east of the Mississippi River; they occur mostly in the western two-thirds of the country. Grasshoppers often severely damage range grasses. They also contribute to soil erosion and "dustbowl" conditions. Their feeding is one of the principal reasons for loss of productive grasslands in many of the Western States. Many cultivated crops are also damaged by grasshoppers. When range grass is scarce and outbreaks are severe, grasshoppers often migrate into and severely damage the foliage of alfalfa, clover, corn, small grains, tobacco, sugarbeets, cotton, lettuce, potatoes, and fruit trees. In fruit orchards, grasshoppers sometimes completely strip the leaves and may kill young trees. You can control grasshoppers by applying insecticides. If your farming practices will permit, cultural measures can be used to help keep grasshoppers in check.Item Controlling Diseases of Raspberries and Blackberries(U.S. DEPARTMENT OF AGRICULTURE., 1975-04-30) Agriculture, U.S. departmentThe most effective control measures for raspberry and blackberry diseases are those taken before the diseases become serious. Varieties adapted to a locality and resistant to the major diseases should be planted, if available. Plants certified as being substantially disease free by a State plant inspection service should be used. Cultural practices that promote vigorous growth are also important in growing healthy raspberries and blackberries.Item Siasa ya Tanu katika Kilimo.(Afisa kilimo msaidizi ofisi yakilimo Tanu., 1977) Kimiti, P.PTANU ya sasa ina kazi kubwa sana, maana TANU inafanya kazi ya kuelimisha, kueleza na kujcnga Taifa letu ili litoke katika hali ya unyongc na kuwa katika hali ya neema na nguvu. Kania sote tunavyoelcwa ni kwamba katika kuwaongoza wananchi. ni budi kwanza tuwasikilize, tushirikiane nao na tufanye kazi pamoja nao. Uhusiano uliopo kati ya Serikali na chama cha TANU ni mkubwa. J ambo la kukumbukwa ni kwamba chama siyo chombo cha Serikali, bali ni Serikali ambayo ndiyo chombo kinachotumiwa na chama katika kutekeleza matakwa yo vote ya wananchi ambao sisi sote tunawatumikia. Hii ndiyo maana tunasema kuwa chama kina wajibu mkubwa wa kufanya, katika kufikiria misingi ambayo baada ya kuwekwa kwa uwazi, ni budi Serikali ifuate na kutekeleza. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ni sehemu ya Serikali. Hivyo Wizara hii ina wajibu mkubwa sana katika kuitekeleza siasa ya TANU ambayo ndiyo inayoongoza Serikali.Item Controlling the -4 Greater Wax Moth(United States Department of Agriculture, 1981-01-23)The greater wax moth is also known as the bee moth, the bee miller, the wax miller, and the web worm. In its larval stages, it damages combs and honey and is responsible for large losses to bee keepers in the United States. This insect is found almost everywhere that bees are raised. Its greatest damage is done in the Southern States, where its season of activity. is longest.Item Kichaa cha mbwa ni hatari(Ukulima wa kisasa, 1982-06)Kichaa cha mbwa ni ugonjwa wa hatari sana unaoleta vifo kwa binadamu na wanyama.Una dalili zinazoambatana na mishipa ya fahamu ambazo mwanzo huwa ni kuongezeka kwa furaha au hasira,kupoteza fahamu na mwishowe kupooza kwa viungo vya mwili,Item Korosho(Wizara ya kilimo, 1983) Mradi wa mafunzo ya wakulimaUzalishaji wa korosho duniani umekua ukiongezeka kila mwaka kutokana na jitihada zinazoendelea katika nchi mbalimbali kufanya upanuzi wa maeneo ya kilimo cha korosho, pamoja na matumizi ya teknolojiaka- ma vile matumizi ya mbegu bora. Aidha, katika bara la Afrika kumekuwa na jitihada za kuongeza ubanguaji wa korosho pamoja na kuongeza uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na korosho.Item Jarida la uenezi wa ufugaji wa samaki kwa wakulima(ALCOM/FAO/SUA, 1984)Jarida hili linajumuisha kwa pamoja majarida matatu; Jinsi ya kutengeneza bwawa lako la samaki, Jinsi ya kulisha samaki wako na Jinsi ya kutunza bwawa lako la samaki yaliyotolewa na ALCOM kwa matumizi ya jimbo la mashariki, Zambia. Kufuatia matokeo ya utafiti, marekebisho kadhaa yamefanywa ili kuimarisha elimu ya ufugaji wa samaki Tanzania.Item Karanga(Sokoine university of agriculture, 1987) wizara ya kilimoKaranga ni zao zuri sana ambalo hutumika kama chakula na mafuta pia,karanga hupandwa sehemu tofauti nchini Tanzania.karanga hupandwa kwa kufuata kanuni zifuatazo kabla ya kupanda, chagua mbegu ambazo hazishambuliwi na wadudu au magonjwa, ondoa mbegu zilizo sinyaa na kutupa mbali kabla ya kupanda.Item Kulima na kufuga kwa njia ya kisasa(INADES-FORMATION, 1987-11-13) Inades-formation, TanzaniaKijitabu kidogo hiki kina mambo ya msingi. Yafaa ukisome kabla hujaanza kujifunza. Kinaelekeza mambo muhimu matano: Masomo haya yatamsaidia na kumfaidi nani?, Zipo faida gani katika kujifunza?, Yakupasayo kujua juu ya masomo haya, Jinsi ya kujifunza masomo haya, Jinsi ya kufanya kazi za mazoezi.Item faida za mboga za majani na matunda(Ukulima wa kisasa, 1989-07)Mboga na matunda ni muhimu kwa ajili ya miili yetu.Hutupatia vitamini na madini,viini ambavyo hulinda miili yetu isishambuliwe na magonjwa pamoja na kujenga na kuimaiisha meno na mifupa.Item Kilimo bora cha nyasi(Shirika la kilimo Uyole, 1990-05) Myoya, T.JKatika Nyanda za Juu za Kusini ni Mikoa miwili tu (Iringa na Mbeya) ambayo idadi ya ng'ombe wa maziwa imeongezeka sang. Hii ni baada ya kuanzishwa kwa mradi wa kushughulikia wafugaji wadogo wadogo kati ya nchi ya Uswisi na Tanzania. Katika sehemu hizi nyasi za asili zilizopo ni zile za kuezekea na utafiti uliofanyika Uyole unaonyesha kuwa nyasi hizi kutoa chakula kidogo kwa msimu. Vile vile baada ya msimu wa-mvua kuanza nyasi hizi hukua upesi upesi na baada ya miezi miwili tu, hutoa mbegu na hivyo ubora wake kupungua. Hi mifugo ya kisasa iweze kutoa maziwa mengi inahitaji chakula chenye asili mia protini zaidi ya saba kiasi ambacho hakipatikani kwenye nyasi za asili. Hivyo kwa ufugaji wa kisasa ni lazima mbinu nyingine za kuweza kupata malisho bora zitumike. Hata hivyo katika nyanda hizi msimu wa ukuaji wa mimea ni siku 180 tu yaani toka mwanzo wa Desemba hadi mwisho wa Mei. Baada ya hapo malisho hayakui kwa sababu ya baridi kali ya usiku, hasa mwezi wa sita mpaka wa nane, na baada ya hapo kwa ajili ya ukosefu wa unyevu. Hivyo tunakabiliwa na miezi sita ambayo lazima mbinu ya kupata chakula bora zitumike.Item Manufaa ya kilimo bora cha maboga(Ukulima wa kisasa, 1990-07) Magembe, AMaboga ni zao la chakula ambalo hulimwa katika sehemu nyingi nchini Tanzania, lakini kwa kiasi kidogo kidogo sana, aghalabu hua linapandwa katika mashamba ya mahindiItem Mafunzo ya kilimo.(INADES-FORMATION TANZANIA., 1990-07-19) Inades-formation, TanzaniaNi asubuhi na mapema Bwana shamba anakutana na Matonya akiwa na shoka beganiJ hengo mkononi na kibuyu cha maji. Hiki ni kipindi cha kiangazi Miti imepNkutisha majani nyasi na vichaka vyote vimekauka majani yote. Upepo unatimua vumbi kila mahali hasa katika maeneo yenye njia za mifugo mashambani na hata barabarani. Na maeneo ya milimani yameanza kuchomwa moto.Item Kanuni za kilimo bora cha minazi(Dar Es Salaam University Press, 1992) National Coconut Development ProgrammeIli kupata mnazi ulio bora mkulima ni lazima awe muangalifu wakati wa kupanda. Mche uliopandwa vibaya huchelewa kukua na hata wakati mwingine hufa. Mazingira kama vile aina ya udongo, kiasi cha mvua, joto, na mwinuko lazima yaangaliwe kwa makini kabla ya kupanda.Item Mafunzo ya ufugaji(inades formation Tanzania, 1992) Inades formation TanzaniaTanzania ina idadi kubwa ya kuku wa kienyeji wanaofugwa kwa mtindo wa huria vijijini na hata mijini. Katika mtindo huu wa ufugaji, kuku huachwa huru mchana kutwa kujitafutia chakula wao wenyewe. Pengine baadhi ya wakulima huwatupia kuku wao mabaki ya chakula, chenga za nafaka au nafaka zenyewe. Wapo pia wakulima walio na utaratibu wa kuwapa kuku wao pumba za nafaka na maji ya kunywa kila inapowezekana. Zinapofika nyakati za jioni kuku hulala jikoni, au ndani ya nyumba ya mkulima mwenyewe. Ingawaje ufugaji wa aina hii ni rahisi, lakini faida inayopaikana (kama ipo) ni ndogo sana. Kutokana na kuzaana wenyewe wa wenyewe (kutobadili jogoo), lishe duni n.k., kuku hawa wana umbo dogo. Hutaga mayai machache, tena madogo madogo. Nyama yao ina ladha nzuri, lakini kwa vile wana umbo dogo, kiasi cha nyama wanayotoa ni kidogo tu. Katika kijitabu hiki “Kufuga na Kuboresha Kuku wa Kienyeji” tutazungumzia jinsi ya kuboresha kuku wa kienyeji kwa njia ya uzalishaji, kutumia jogoo bora, kuboresha lishe ya kuku. Tutazungumzia pia njia mbalimbali za kufuga zinazoweza kumnufaisha mfugaji mdogo. Kutokana na maarifa haya wewe mkulima utaweza kuona haja ya kufanya mabadiliko katika ufugaji wako. Hi uweze kunufaika na ufugaji ni lazima uwe na mifugo bora. Kitabu hiki kimeandikwa ili kukupatia maarifa na mbinu za kutumia ili upate kuku bora kutokana na kuku wako wa kienyeji. Katika kitabu kingine “ Kufuga kuku wa biashara” Utajifunza maarifa na mbinu bora za ufugaji wa kuku wa biashara. Hawa ni kuku wa kigeni. Wanahitaji matunzo maalum tofauti na yale ya kuku wa kienyeji wanaoboreshwa.