Mkulima
Permanent URI for this community
Browse
Browsing Mkulima by Subject "AINA ZA MPUNGA"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mwongozo wa kufundishia kilimo bora cha mpunga(Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Ukanda wa Tropiki (IITA), 2020) KILLENGA,Sophia Kashenge; CHUWA Charles; MVUKIYE Ndimubandi; ZAKAYO Joel; PAUL Ibrahim; KIMARO DidasMwongozo huu ni muhimu katika mpango rasmi wa mafunzo unaohakikisha utaratibu wa aina moja wa kuwasilisha mada katika ufundishaji. Unaweka katika eneo moja ujuzi, hatua mbalimbali na taarifa zote muhimu zinazohitajika katika kutekeleza kazi zinazohitajika. Mwongozo huu una sehemu tisa, sehemu ya kwanza inahusu dhana za aina bora za mpunga. Katika sehemu hii mwongozo umeeleza sifa za aina bora za mpunga. Sehemu ya pili inaeleza kuhusu maandalizi ya shamba (jaruba) ambayo yanahusisha kusafisha shamba, kulima (kutifua), kusawazisha, na kutengeneza kingo za shamba la mpunga. Sehemu ya tatu inahusu maandalizi ya mbegu ili kuhakikisha ubora wa mbegu. Sehemu ya nne inahusu upandaji wa mpunga ambapo shughuli kubwa ni kupanda shambani. Sehemu ya tano inahusika na utunzaji wa shamba ambapo matumizi ya maji na udhibiti wa magugu vimeelezwa. Sehemu ya sita inaeleza kuhusu kalenda ya zao la mpunga kuanzia kupanda, hadi kuvuna mpunga ambayo itawezesha upangaji mzuri wa kazi za shambani pamoja na gharama za uzalishaji. Sehemu ya saba inaeleza kuhusu udongo ulioathirika na chumvi na jinsi unavyoathiri tija ya uzalishaji wa mpunga. Sehemu ya nane inahusu namna ya kuongeza tija ya uzalishaji wa mpunga kwenye udongo ulioathiriwa na chumvi yenye madini mengi aina ya sodiamu ambapo mbinu zilizothibitika kuurekebisha zimejadiliwa. Sehemu ya tisa ambayo ni ya mwisho inahusu kuongeza tija za uzalishaji wa mpunga kwenye udongo ulioathiriwa na madini mengi aina ya Kalsiamu (chokaa), sehemu hii imejadili kwa kina mbinu zilizothibitika kuurekebisha udongo ulioathiriwa ili kuhakikisha uzalishaji endelevu wa mpunga kwa tija katika udongo wa aina hiyo. Mwongozo huu unalenga kuendelea kuwajengea uwezo wadau wa kilimo katika mchakato endelevu wa kuongeza tija ya zao la mpunga kwenye maeneo au mazingira yao