Kilimo cha Mkonge Tanzania -
Loading...
Date
2018-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kituo cha Utafiti Mlingano - ARI
Abstract
Zao la mkonge liliingizwa nchini mwaka 1892 na mtaalamu wa kijerumani Dr. Richard Hindorff
ambaye alikuwa ni mtafiti wa mimea na udongo. Mtaalamu huyo alichukua miche 1000 kutoka
pwani ya Mexico kwenye jimbo la Yuctan ambalo ambalo ndilo asili ya jina katani na kuisafisha
kwa magendo kwa kupitia Frolida , Marekani na Humburg Ujerumani. Kati ya miche 1000, ni
miche 62 tu ndiyo iliyofika Tanganyika na ilipandwa sehemu iitwayo kikokwe huko Pangani Tanga.
Mkonge ulisambaa maeneo mengi ya Tanganyika mpaka kufikia mwanzoni mwa miaka 1960
Tanganyika ilikuwa inaongoza kwa uzalishaji wa mkonge ikifatiwa na Brazil na mexico kwa mauzo
ya tani 230,000 kwa mwaka nje ya nchi .
Description
Keywords
Mkonge, Katani, Tanga