Uboreshaji wa vikundi vya wakulima - Utafiti Juu ya Mbinu za Uboreshaji wa Vikundi vya Wakulima Chiniya Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo, Tanzania (TARP II-SUA Project)
dc.contributor.author | Wambura, R. M | |
dc.contributor.author | Rutatora, D. F | |
dc.contributor.author | Shetto, M | |
dc.contributor.author | Ishumi, O | |
dc.contributor.author | Oygard, R | |
dc.date.accessioned | 2020-10-07T06:19:38Z | |
dc.date.available | 2020-10-07T06:19:38Z | |
dc.date.issued | 2003-12 | |
dc.description.abstract | Kilimo ndio tegemeo kubwa na ndicho kinachohusisha idadi kubwa ya watu nchini Tanzania. Hata hivyo matokeo yake bado hayajawa ya kuridhisha kutokana na ukweli kwamba wakulima walio wengi uwezo wao bado ni mdogo kiasi cha kilimo chao kushindwa kutosheleza hata mahitaji ya familia. Hali hii imekuwa ikiendelea kuwa duni kwani mahitaji ya kilimo yamekuwa yakipanda siku hadi siku na hivyo mkulima mmoja mmoja kushindwa kuboresha kilimo kutokana na matatizo mbalimbali kama vile ushauri na pembejeo. Aidha kwa upande mwingine kidogo ambacho wakulima wamekuwa wakikipata kutokana na mfumo mzima wa soko kimekuwa hakipati bei ya kutosha ukilinganisha na gharama ya uzalishaji. Moja ya mikakati inayotiliwa mkazo na serikali ni kuwafundisha wakulima kwamba ili kujikwamua wanahitajika kuunganisha nguvu na kujenga mitaji itakayowawezesha kuboresha kilimo na hatimaye hali yao ya maisha kwa ujumla. Kwa kuzingatia hali hii, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH) kinatekeleza mradi wa uhakika wa chakula na pato la kaya kwa wakulima wadogowadogo nchini Tanzania. Mradi wa uboreshaji wa vikundi vya wakulima chini ya mradi wa TARP II-SUA unaendeshwa katika Mkoa wa Morogoro. Kwa kuanzia, kuna vijiji vinne katika Wilaya za Mvomero (Mkindo na Lusanga) na Kilombero (Sonjo na Mbasa). Kijarida hiki kimeandikwa ili kitumike katika kueneza mbinu mbalimbali za mradi kuhusu uimarishaji wa vikundi vya wakulima ambavyo ni vyombo vya kiuchumi ambapo mtu anaweza kujiunga na wenzake ili aweze kujiendeleza zaidi kiuchumi na hata kijamii katika lengo zima la kuondoa umaskini. Mambo muhimu yanayozingatiwa katika vikundi vya wakulima ni pamoja na: nia ya kufanya jambo kwa pamoja; shughuli au tatizo linalolengwa katika kutatuliwa; na mafanikio yanayotarajiwa kutokana na nguvu za pamoja. | en_US |
dc.identifier.isbn | 9987 605 90 7 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/handle/123456789/505 | |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | TARP II-SUA Project | en_US |
dc.relation.ispartofseries | ;TS 2-81 | |
dc.subject | Vikundi | en_US |
dc.subject | Ushirika | en_US |
dc.subject | Wakulima | en_US |
dc.title | Uboreshaji wa vikundi vya wakulima - Utafiti Juu ya Mbinu za Uboreshaji wa Vikundi vya Wakulima Chiniya Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo, Tanzania (TARP II-SUA Project) | en_US |
dc.type | Book | en_US |