Funza wa vitumba vya pamba (Helicoverpa armigera)
Loading...
Date
2014-11
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
CABI
Abstract
Funza wa vitumba ni mdudu msumbufu wa mimea mingi muhimu ya chakula, mafuta
na fedha duniani kote, ikiwa ni pamoja na nafaka, mikunde, matunda na mboga. Ushambulizi mkali
wa viwavi wa nondo huyu kunaweza kusababisha hasara kwa mavuno yote. Kudhibiti kwa njia ya
kemikali kunapaswa kufanywa kwa makini na wakati mwafaka kwa kuwa viwavi hutoboa na kuingia
ndani ya nafaka au matunda ya mmea, hivyo kuweza kulindwa. Usugu kwa dawa, kama vile za
pyrethroid, kumeripotiwa katika nchi nyingi. Bakteria aina ya Bacillus thuringiensis(Bt) na madawa
ya mwarobaini hutoa udhibiti wa ufanisi dhidi ya viwavi na wakati huo huo kupunguza uharibifu wa
maadui wa kiasili. Udhibiti muhimu wa kitamaduni ni pamoja na kuondoa na kuharibu mabaki ya
mimea baada ya kuvuna, kulima udongo ili uwatoe nje pupae na kupanda kwa wakati mmoja.
Description
Keywords
Funza, Wadudu, Pamba