Lishe kwa mtoto mwenye virusi vya ukimwi umri wa miaka 2 hadi 9

Loading...
Thumbnail Image

Date

2006-08-15

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

COUNSENUTH

Abstract

Lishe bora ni rnuhimu kwa watoto wote hususan wenye virusi vya UKIMWI kwa ajili ya ukuaji na maendeleo yao. Watoto wanakua kwa haraka hivyo wana mahitaji makubwa ya chakula ili kuwapatia virutubishi muhimu yaani nishati-lishe, protini, madini na vitamini. Watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI na wenye UKIMWI wako katika hatari kubwa ya kupata utapiamlo kutokana na: • Ongezeko la mahitaji ya virutubishi hasa nishati-lishe. • Maradhi ya mara kwa mara. • Ulaji duni. • Uyeyushwaji na ufyonzwaji duni wa virutubishi mwilini. Mengi ya maradhi yanayoambatana na kuishi na virusi vya UKIMWI na UKIMWI huathiri mfumo mzima wa ulaj i wa chakula na kusababisha lishe duni. Lishe duni hudhoofisha mfumo wa kinga na hivyo humuweka mtoto katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali kwa urahisi. Maradhi na utapiamlo kwa pamoja huhatarisha maisha ya mtoto mwenye virusi vya UKIMWI.

Description

Keywords

Virutubishi mwilini, UKIMWI, Lishe ya mtoto, Dalili za UKIMWI, Lishe bora

Citation

Collections