Muongozo wa utunzaji bora wa mashamba ya miti ya wananchi

Loading...
Thumbnail Image

Date

2012-01

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Climate Change Impacts, Adaptation and Mitigation Programme - CCIAM

Abstract

Upandaji wa miti nchini Tanzania umekuwa ukisisitizwa kwa miongo kadhaa lakini kukubalika kwa shughuli hizi kumekuwa hakuridhishi. Tofauti na watu wa sehemu nyingine za nchi, watu wa Wilaya ya Makete wamehamasika kupanda miti kutokana na hali mbaya ya hewa na ukosefu wa rutuba kwenye udongo sababu ambazo zilisababisha mazao duni ya kilimo. Pia kwa muda mrefu, wananchi wa Wilaya ya Makete wameshajua umuhimu wa miti kwa kuwa kwa kiasi kikubwa mauzo ya miti na mbao yanachangia kipato cha wakulima. Kabla ya kujikita kwenye kilimo cha miti, kipato cha wananchi wa Wilaya ya Makete kilitegemea zaidi mazao ya kilimo kama vile mahindi, ngano, mchele, viazi miviringo na pareto. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, uzalishaji wa mazao hayo umepungua kwa kiasi kikubwa na wakati mwingine kusababisha tishio la njaa.

Description

Keywords

Miti, Utunzaji, Mashamba, Wakulima, Tabianchi, Makete

Citation

Collections