Misitu na Nyuki

Permanent URI for this collection

Browse

Recent Submissions

Now showing 1 - 20 of 45
  • Item
    Kijarida cha mradi wakuongeza dhamani ya milima katika misitu ya Tao la mashariki
    (Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania, 2016-03) Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania
    Ili lengo la mradi la kusaidia vijiji kutekeleza mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu kwa Jamii litimie, Mradi unaendelea kupanua elimu na kusaidia vijiji vingine 2 (Ndole na Magunga) kuanzisha misitu ya Hifadhi ya Kijiji na pia kijiji kingine cha Diburuma kilipata elimu na uamasishwaji wa usimamizi wa misitu ya jamii. Sheria ya msitu ya mwaka 2002 inatoa fursa nyingi kwa jamii kusimamia na kulinda misitu Sheria inasema kuwa miongoni mwa malengo yake makuu ni kuwapa wajibu na haki ya kusimamia misitu wananchi ndani na kandokando ya misitu Wanajamii walielimishwa kwamba wakiweza kutunza misitu yao watapata motisha kama: ❖ Kubaki na 100% ya mapato yatokanayo na mauzo ya mazao ya misitu. ❖ Kubaki na tozo na faini. Faini inayotozwa katika ardhi ya kijiji kutokana na Misitu ya Hifadhi ya Kijiji au Misitu ya jamii inabaki kijijini ili mradi imeelezwa kwenye sheria ndogo za kijiji. ❖ Utaifishaji wa mazao ya misitu na vifaa kutokana na uvunaji haramu. ❖ Wanaweza kufanya uvunaji endelevu wa mazao ya misitu ili mradi imeelezewa kwenye mpango wa uvunaji wa kijiji Baada ya kuelimishwa wanavijiji wa vijiji vya Ndole, Diburuma na Magunga walianza mchakato wa kusimamia Misitu ya Hifadhi yaVijiji.Vijiji vyote vitatu viliunda kamati ya maliasili ya kijiji yenye wajumbe 12 ikijumuisha wanaume na wanawake. Vijiji vya Magunga na Ndole walifanikiwa kutenga maeneo ya Misitu. Ndole hekta 1,238.81 na Magunga hekta 1,277.3, pia waliandaa mpango wa usimamizi wa misitu, sheria ndogo na kuidhinishwa na Mkutano mkuu wa kijiji na kupelekwa kwenye Halmashauri ya Wilaya kwa idhini na kwaajili ya kusajiliwa kwenye daftari la usajili wa misitu ya vijiji. Hii inapelekea kufanya jumla ya hekta 10,131.22 kwa vijiji 8 (Bwage, Mziha, Difinga, Msolokelo, Masimba, Makuyu Magunga na Ndole) ambavyo vinatekeleza Usimamizi Shirikishi wa Misitu kwa Jamii na kuidhinishwa na mkutano mkuu wa kijiji. Kwa kipindi cha mwaka 2015 mpango wa usimamizi wa misitu na sheria ndogo za vijiji 3 (Makuyu, Msolokelo na Masimba) zimeidhinishwa na Halmashauri yaWilaya ya Mvomero na kusajiliwa kwenye daftari la usajili wa misitu ya vijiji.
  • Item
    Mwongozo wa uanzishwaji na usimamizi wa hifadhi za nyuki na manzuki Tanzania
    (Wizara ya Maliasili na Utalii, Tanzania, 2021-01) Idara ya misitu na nyuki
    Ufugaji Nyuki ni miongoni mwa sekta muhimu za kiuchumi nchini Tanzania, yenye mchango mkubwa kwenye maisha ya watu wengi mijini na vijijini. Sekta hii inakadiriwa kuajiri zaidi ya watu milioni mbili nchini kwenye mnyororo wake mzima wa thamani. Mazao ya nyuki kama vile asali, nta, chavua, gundi ya nyuki, maziwa ya nyuki na sumu ya nyuki, yanatumika yakiwa kwenye hali tofauti pia kama malighafi ya viwanda vya chakula, urembo, dawa, nguo, ngozi, umeme na mishumaa. Ufugaji Nyuki umedhihirisha kuchangia ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa kuongeza ubora wa mbegu na uhifadhi wa bioanuai kwa njia ya uchavushaji unaofanywa na nyuki. Kutokana na umuhimu kwenye uchavushaji, ufugaji nyuki umetambuliwa kama nyenzo ya uhifadhi. Pamoja na michango hii yote, bado sekta ya ufugaji nyuki haijaonekana kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi na uzalishaji wa mazao ya nyuki kutokana na kutofuatwa kwa taratibu bora za ufugaji nyuki. Tangu kuanza kutumika kwa Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, ambayo inahimiza uanzishwaji na umiliki wa Hifadhi za Nyuki na manzuki ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki, kumekuwa na maendeleo yasiyolingana kwenye maeneo tofautitofauti ndani ya sekta. Mfano, hakuna maendeleo yanayoridhisha kwenye uanzishwaji wa Hifadhi za Nyuki na manzuki. Aidha, kuna zaidi ya misitu 100 inayomilikiwa na Serikali na Sekta Binafsi iliyobainishwa kuwa hifadhi za nyuki lakini haijatangazwa kwenye Gazeti la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Ufugaji Nyuki Na. 15 ya mwaka 2002. Hali hii inaifanya baadhi ya misitu kupoteza hadhi yake ya kutumika kama hifadhi za nyuki na kutangazwa kisheria. Kwa miaka kadhaa, wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Serikali, Asasi Zisizo za Serikali (AZISE), Asasi za Kijamii, Sekta binafsi na vijiji vimeanzisha hatua za kutangaza Hifadhi za Nyuki lakini vimeshindwa kukamilisha hatua za kutangaza hifadhi hizo kisheria. i Sababu zilizokwamisha zinaweza kuwa ni pamoja na kukosekana kwa mwongozo unaoongoza na kusimamia uanzishwaji na usimamizi wa Hifadhi za Nyuki na manzuki. Hivyo ili kuhakikisha utendaji wenye ufanisi na kiwango katika maeneo yote ya Hifadhi za Nyuki na manzuki; Wizara imeandaa mwongozo huu ili kuwaongoza wadau katika uanzishwaji na usimamizi wa Hifadhi za Nyuki na Manzuki. Mwongozo huu, unalenga kutoa mwanga kwa wadau kuhusu taratibu za uanzishwaji na usimamizi wa Hifadhi za Nyuki na manzuki pamoja na viwango vyake vya usimamizi wa uwandani. Serikali inatarajia kuwa mwongozo huu utakuwa nyenzo muhimu na ya msaada ya kuimarisha usimamizi na uanzishwaji wa Hifadhi za Nyuki na manzuki. Aidha, mwongozo huu utaimarisha uhifadhi wa rasilimali za nyuki na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa maendeleo endelevu.
  • Item
    Tathmini ya athari kwa mazingira na jamii (tamj)
    (Spring Lodge, 172 Barabara ya Chester, Helsby, WA6 0AR, UK, 2019-08) Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira
    Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) litasafirisha mafuta kutoka kwenye kituo cha mafuta, kilichopo Wilayani Hoima, nchini Uganda, kuelekea kwenye kituo cha kuhifadhia na kituo cha kupakia mafuta kwenye meli kwenda nchi za nje, vilivyopo kwenye rasi ya Chongoleani, kaskazini mwa mji wa Tanga katika Pwani ya Afrika Mashariki, Tanzania. Athari zinazoweza kutokana na mradi, faida na hasara kwa uchumi, jamii na mazingira nchini Tanzania zimefanyiwa tathmini na kuelezwa kwa kina katika nyanja mbalimbali zilizodhaniwa kuwa za thamani na muhimu katika jamii (kwa mfano, kudumisha njia za kujikimu). Mbinu za kuepuka au kupunguza athari zilizo mbaya zimeelezwa na baada ya hatua hizo kutekelezwa, athari zinazofikiriwa kubakia pia zimeelezwa. Taarifa ya Tathmini ya Athari za kimazingira na kijamii imeandaliwa kwa kuzingatia:
  • Item
    Jarida la mbinu bora
    (Echo community, 2011) Kinsey, Erwin
    Ufugaji wa mifugo kiasili ni mfumo wa maisha ambao watu au jamii husika wanaishi maisha yao kwa kutegemea mifugo. Katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, wafugaji hawa hutegemea zaidi mifugo ya aiana mbali mbali kama; ng’ombe, kondoo, mbuzi, punda, na ngamia ili kukimu maisha yao na familia zao. Mifugo iliyotajwa, imeorodheshwa kwa kigezo cha kuanzia na lile kundi ambalo sio stahimilivu sana (ng’ombe) na kumalizia na lililo stahimilivu zaidi (punda na ngamia), pia kwa kuzingatia maeneo ya ufugaji kuanzia na yaliyo makame kiasi hadi makame zaidi. Wafugaji hawa wana mchango mkubwa sana katika sekta/idara husika lakini bado hawajaweza kuthaminiwa ipasavyo. Kwa mfano: uwezo wa kutunza/ kuendeleza kizazi cha ng’ombe wa asili. Katika utunzaji wa mifugo yao, wafugaji hawa wana uwezo wa kipekee wa kutumia maeneo yanayokabiliwa na ukame kwa njia ya kuhama hama kwa ajili ya kupata malisho bora na maji. Ni ukweli usiopingika kwamba, katika/ ukanda wa Afrika ya mashariki maeneo ya hifadhi nyingi tunazozifurahia kwa sasa ni matokeo ya wafugaji kuhamahama na kuweza kuyatunza maeneo haya kwa ajili ya malisho na hasa kuweza kuyalinda/kuzuia yasiingiliwe na shughuli za kilimo.
  • Item
    Ugonjwa wa miti
    (Rich Mathey - M&M Tree Care, 2019-01) Rich Mathey - M&M Tree Care
    Kuvu kwenye miti yako inaweza kuja kwa aina nyingi kama vile uyoga wa rafu usio na madhara kwa kitu hatari zaidi kwa miti yako kama vile Rhizosphaera Needle Cast ambayo itaua mti wako wa Colorado Blue Spruce. Huwezi kamwe "kuponya" mti wa Kuvu, lakini unaweza kupata kuvu kwenda "katika msamaha" ambapo mti wako unarudi kwa afya na nguvu.
  • Item
    Misitu na hifadhi ya Mazingira
    (Tanzania Educational publishers L.T.D, 2002) Ngara, Lulenge
  • Item
    Wanyamapori Tanzania
    (Wizara ya maliasili na utalii, 2006-12) Wizara ya maliasili na utalii
    Taarifa za wataalam zinaonyesha kuwa vina vya maji katika Ziwa Victoria na Ziwa Rukwa vimepungua sana kutokana na uharibifu wa mazingira ambao nchi zilizoendelea hupendelea kuuita Mabadiliko ya Hali ya Hewa" ili kuficha ukweli wakati ni malokeo ya uharibifu wa mazinbgira. Kwa ujumla, mabadiliko ya hali ya hewa ni matokeo ya uharibifu wa mazingira unaotokana na binadamu. pia hutokana na kazi za viwandani ambazo pia zimekuwa zikisababisha moshi ambao huharibu kiambaza kinachozuia watu wa.siaihirike na niiale ya jua.
  • Item
    Ufugaji nyuki kibiashara
    (Chuo Kikuu Mzumbe, 2018) Chuo Kikuu Mzumbe, Skuli ya Biashara
    Kitabu hiki ni zao la uzoefu, kujifunza na utafiti wa miaka mitano katika sekta ya nyuki. Baada ya kufanya kazi na wajasiriamali katika sekta ya misitu na nyuki, fursa katika ufugaji-nyuki zilikuwa ni wazi. Hata hivyo, uwezo wa wajasiriamali kuwekeza katika sekta hii umekuwa na changamoto lukuki. Nchini Tanzania, uwindaji, ukusanyaji wa mazao ya nyuki na ufugaji nyuki umekuwepo toka enzi. Hata hivyo sekta hii imeendelea kuwa isiyo na manufaa kwa mfugaji. Wafugaji wa nyuki hufanya shughuli hii kwa mazoea, pasipo kuzingatia mbinu na utaalamu wa kisasa; Wanategemea zana, utaalamu na uzoefu wa asili. Hivyo, uzalishaji umekuwa mdogo, usiokuwa na tija. Pia, mazao ya nyuki hayana ubora stahili, na hivyo yasiyoleta tija kwa mfugaji. Hali hii hupelekea kushindwa kupata soko lenye tija. Hata hivyo, ikiwa ufugaji nyuki utafanyika kwa kuzingatia mbinu za kisasa; kanuni, zana na nyenzo bora; basi uzalishaji unaweza kuongezeka. Pia, yatapatikana mazao yenye ubora stahili na ambayo yataweza kufikia masoko yenye tija. Kwa kuzingatia changamoto zilizopo katika sekta ya nyuki; hasa suala la elimu, ujuzi na utaalamu wa kufuga kwa tija. Ujio wa kitabu hiki, “Ufugaji nyuki kibiashara: Nadharia na vitendo” kitachangia katika kuleta ufanisi katika sekta ya nyuki nchini. Ni matumaini yetu kuwa ujuzi uliomo katika kitabu hiki utawafaa wadau mbalimbali katika sekta ya nyuki. Asanteni sana.
  • Item
    Asali na faida zake
    (Sokoine university of agriculture, 2022-12-22)
    Ikiwa ni tamu kuliko sukari, je asali, ni kimiminika asilia kinachochukua nafasi ya sukari? Mtaalamu wa lishe Jo Lewin anaainisha faida za kiafya na madhara ya asali. Asali hutengenezwa na nyuki. Hutokana na mkusanyiko wa vimiminika vyenye sukari nyingi itokayo kwenye mimea ya maua. Huhifadhiwa katika sega la asali ili kutoa chakula kwa nyuki.
  • Item
    Fahamu Umuhimu Wa Ndege Kama Kiashiria Cha Hali Ya Mifumo Ya Ikologia Katika Maeneo Mbali Mbali
    (Sokoine university of agriculture, 2021-07-08) Mrosso, Hillary Thomas
    Kiashiria ni alama ambayo inatoa taarifa au tahadhari juu jambo fulani zuri au baya na kukufanya uweze kuchukua hatua mapema. Katika uhifadhi au sayansi ya wanyamapori kiashiria ni biolojia ya viumbe ambayo hutumia kuwepo au kutokuwepo kwao katika ikolojia au mazingira Fulani kama kipimo cha afya, ubora au mabadiliko. Wanyama jamii ya amphibia na reptilia wanaweza kutumika kupima mabadiliko ya hali ya hewa kama , ukame, uchafuzi wa mazingira na kuharibika au kusitawi kwa ikolojia, nk.
  • Item
    Uchakataji Ngozi Kwa Kuzingatia Utunzaji wa Mazingira
    (Sokoine university of agriculture, 2012-06-22) Kok, Jaap
    Kitabu hiki kimejikita katika mafunzo ya Uchakatajina mtunzikukitwaana kukisambaza kwa kikundi cha watu waliojihusisha katika mpango wa maendeleo ya kijiji huko Msekhocika, Zambia. Kitabu hiki kimelenga watu wenye nia ya kuanzisha uchakatajimdogo wa ngozi. Pia kwawale wanaopata ugumuwa kuanza kwa kutumia ujuzi walioupata kwa kusoma vitabu vingine vya nadharia. Vitabu ambavyo huenda vinaelezea mbinu za juu zaidi za Uchakataji, Mbinu ambazo zinatumika katika viwanda vikubwakama vile mashine, bidhaa za kemikali na uwekezaji mkubwa.Kitabu hiki kimekusudiwa kuwa mwongozo kwa vitendo, kwa wale wanaotakakuchakata ngozi kwa idadi ndogo kuanzia ngozi tanohadi kumi za mbuzi ambazo huweza kupatikana katika machinjio kila wiki.Piakimezingatia upatikanaji wa vifaa, zana na uwekezaji mdogo katika vijiji na maeneo ya jirani. Katika kitabu hiki neno Vitendo litakuwa la muhimu sana kuliko neno la kisayansi. Hata hivyo kitabu kitatoa maelezo ya awalikuhusiana nahatua zinazohusika katika mchakato wa kubadilisha ngozi na kuwa ngozi iliyochakatwa. (Ngozi iliyotayari kutengenezea bidhaa).
  • Item
    Improved Tree seed Production Manual
    (Ministry of Natural Resources and Tourism - Forestry and Bee keeping Division, United Republic of Tanzania, 2020-11) Komakech, C; Nshubemuki, L; Swai, R. L; Kasase, A. S
    Plantation forestry resources are managed for the production of both timber and non-timber forestry products (NTFPs). The quality of these end-products is determined by both the quality of the germplasm used in the initial establishment of the plantations and the management practices applied to the planted trees. Broadly, two types of planting materials are used to establish plantations: seeds (sexual reproduction) and vegetative material (asexual reproduction). Regardless of which type of germplasm is used, however, various tree breeding operations need to be followed the planted forestry resources are to see sustainable improvements in both growth and wood quality. The development of tree breeding activity guidelines can help stakeholders involved in establishing research infrastructures apply standardised procedures which will guarantee that they meet their research objectives.
  • Item
    Tree planting for wood fuel
    (Sokoine University of Agriculture, 2020-08-20) Lusambo, L.P
    SUMMARY • Wood fuel is the principal source of energy, accounting for 91 per cent of the total energy consumed in Tanzania. • The dependency on wood fuel is expected to continue for the foreseeable future but the supply of wood fuel is dwindling in all regions. • The Government has accorded high priority to the production of wood fuel and to environmental protection. • Evidence suggests a number of factors influencing overwhelming dependence on wood fuel: poor availability of alternative sources of energy and escalating prices of the available non-wood fuels. • Effects of these factors are exacerbated by poverty among the community. • NAFORMA (2015) reported the consumption of wood exceeds the sustainable supply, causing an annual wood deficit of 19.5 million m3 (MNRT, 2015). • Lusambo (2009) found that 36% of the wood fuel (round wood equivalent) consumption was in the form of charcoal, while 64% was in the form of firewood. • Household fuel consumption in the study areas was found to be unsustainable: heavy dependency on wood fuel was found to be responsible for net deforestation rate of 12.48 ha/day, translating to 45% of total deforestation in Tanzania (Lusambo, 2009). • Several technologies for tree planting for wood fuel exist: establishment of communal woodlots, combination of land reclamation with wood fuel production, central and individual nurseries, use of cuttings and self-germinating seedlings, individual tree- planting based on agro-forestry and intensification of women involvement in tree planting programmes. • This presentation focuses on extent of wood fuel consumption, tree planting, constraints and opportunities for engaging in tree planting
  • Item
    REDD architecture in Tanzania
    (CCIAM, 2012-10-16) Silayo, Dos S.; Kajembe, George C.
    Reducing emissions from deforestation and forest degradation (REDD) in developing countries is an innovative approach for conserving forests to reduce negative impacts of climate change. REDD is considered a significant, cheap, quick and win-win way to curb global greenhouse gases (GHGs) emissions.
  • Item
    Controlling the -4 Greater Wax Moth
    (United States Department of Agriculture, 1981-01-23)
    The greater wax moth is also known as the bee moth, the bee miller, the wax miller, and the web worm. In its larval stages, it damages combs and honey and is responsible for large losses to bee keepers in the United States. This insect is found almost everywhere that bees are raised. Its greatest damage is done in the Southern States, where its season of activity. is longest.
  • Item
    Nakala ya Ufugaji wa Nyuki (1)
    (Gay Marris, UK National Bee Unit (Fera), 2011) Gregory, Pam
    Imetambulika ya kuwa ufugaji wa nyuki inaweza kuwapa watu wa mashambani njia ya kujipatia mapato zaidi. Ijapokuwa ufugaji wa nyuki sio rahisi kila wakati. Nyuki wanaweza kudunga mara nyingi bila kutarajiwa. Uvunaji wa asali inategemea mbinu nyingi kama vile hali ya anga na kwa kupata soko. Asali ya hali ya juu lazima uwe na ubora zaidi. Nta pia ni bidhaa ya muhimu na wakati mwingine huaribiwa. Mwongozo huu wa shambani imetengenezwa ili kusaidia wakufunzi wanaofanya kazi katika Afrika kusini mwa Sahara. Picha yenye rangi ziko na maneno machache. Nakala hii pia inaeleza mbinu rahisi zinazohitajika kuanzisha biashara ya ufugaji wa Nyuki. Pia inatupatia mawazo au mbinu zinazohitajika kuanzisha ufugaji wa Nyuki kwa kutengeneza vyombo vyao wenyewe wakitumia vifaa vya kiasili. Natumaini kuwa hii itasaidia watu kuanzisha ufugaji wa nyuki kwa bei nafuu na labda kufanya majaribio na vitu vipya. Picha hizi zinaonyesha kati ya njia nyingi ambazo watu hutumia kufuga nyuki. Hii inatarajiwa kuwezesha majadiliano na ushirikiano ili kusaidia watu kutatua shida zao wenyewe. Nakala hii inaegemea ufugaji wa nyuki kutumia mzinga wa ‘top bar’ lakini kuna mbinu nyingi na mawazo zinazoweza kutumika na wafugaji nyuki wa kitamaduni na wale wa kisasa wanaotumia mzinga wa fremu. Inatarajiwa kuwa wakufunzi wataweza kutafsiri mbinu hizi kwa lugha ya kiasili. Shukrani kwa usaidizi wa Waterloo Foundation, kwani nakala nyingine itakuwa tayari ifikapo mwaka 2010. Hii itajumuisha mbinu za kisasa za ufugaji wa nyuki na mbinu za kutatua shida. Nakala ya maandishi pekee kwa wakufunzi pia inaweza kupatikana, kwa kutuma ombi kwa Pam Gregory ambayo inafafanua ‘sababu’ na ‘njia’ za ufugaji wa nyuki. Tuma barua pepe kwa: pamgregory@phonecoop.coop
  • Item
    UFUGAJI NYUKI
    (MUMARU (REMP)Mradi wa Usimamizi wa Mazingira Rufiji, 1999) Kisenga, Narcis
    Tokea zama za kale binadamu wamekuwa wakitafuta asali inayozalishwa na nyuki. Kwa azma hiyo shughuli yoyote ya ufugaji nyuki ni kuendeleza zaidi ufanisi wa haya. Binadamu na nyuki hutegemeana. Kwani kwa upande wa nyuki badala ya kuwindwa na kuuawa kwa ajili ya asali yao hutunzwa na kulindwa. Matokeo ya haya siyo tu kupatikana kwa asali na nta bali pia kutambuliwa kwa nyuki kama rasilimali muhimu ya kuhifadhiwa kulindwa na kustawishwa. Ukusanyaji wa asali na nta ni shughuli ya kijadi katika karibu bara lote la Afrika. Wafugaji nyuki wa jadi hutumia mizinga rahisi ambayo njia ya uvunaji asali huluta maangamizo ya makundi ya nyuki. 1 Kwa hiyo iko haja ya kubadilisha njia hii kali ya ufugaji nyuki na kuanzisha ufugaji nyuki mzuri wenye ufanisi zaidi. Huu ni ufugaji wa kutumia mizinga ya masanduku yenye viunzi vya juu au masanduku yenye fremu. Shughuli yenyewe inaweza ikawa ni mradi wa kiwango kidogo ambao unaweza kuendeshwa kirahisi. Nyuki wanasaidia kuchavusha mimea ya asili na ile ya kilimo na biashara. Mizinga haichukui eneo lolote la ardhi na haitegemei pembejeo kutoka nchi za nje. Yeyote anaweza akaanza ufugaji nyuki na familia nzima ikaweza kushirikishwa. Njia nzuri ya kujifunza juu ya ufugaji nyuki ni kufanya kwa vitendo.
  • Item
    Jarida la TAFORI
    (Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), 2019-06-15) TANZANIA FORESTRY RESEARCH INSTITUTION (TAFORI)
    Siku ya nyuki duniani ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutunza viumbe wanaochavusha mimea hususan nyuki, kutambua madhara ambayo yanakabili viumbe hao na kujua mchango wake kwa maendeleo endelevu. Nyuki ni mdudu muhimu sana katika mfumo ikolojia na maisha ya mwanadamu, kwani huchavusha asilimia 70 ya mimea inayohudumia asilimia 90 ya watu duniani. Nyuki wana mchango mkubwa katika maisha ya mwanadamu, hivyo jamii inatakiwa kuwatunza. Kwa kutambua umuhimu wa nyuki, Baraza la Umoja wa Mataifa (“The United Nations General Assembly”) lilipitisha azimio kuwa kila tarehe 20 Mei iwe Siku ya Nyuki Duniani. Azimio hilo liliridhiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuatia pendekezo la Solvenia la Desemba 2017 la kuifanya tarehe 20 Mei kuwa siku ya nyuki duniani. Chimbuko la siku ya nyuki duniani lilitokana na Bwana Anton Jansa aliyezaliwa siku ya tarehe 20/5/1734. Bwana Anton alikuwa mwalimu na mwasisi wa ufugaji nyuki duniani. Alifafanya ufugaji wa nyuki kitaalamu, aliandika vitabu na kufundisha ufugaji nyuki nchini Slovania. Bwana Anton aliwathamini sana nyuki na moja ya kati ya vitabu vyake alivyoandika ni“Bees are a type of fly, hardworking, created by God to provide man with all honey and wax” maana yake nyuki ni wadudu wachapakazi walioumbwa na Mungu kumpatia mwanadamu mahitaji yake yote ya asali na nta. Hivyo, sherehe za kuadhimisha siku ya nyuki duniani hufanyika kila mwaka tarehe 20 Mei kwa heshima ya Bwana Anton Jansa
  • Item
    Mifumo endelevu ya nishati ya miti (mkaa na kuni) Tanzania : mwongozo wa mafunzo ya awali
    (WORLD AGROFORESTRY CENTRE, 2018-10-09) TAREA
    Nishati ya miti (mkaa na kuni) ni aina ya nishati inayotumika zaidi kwenye kupikia na kwenye kuota moto kusini mwa Jangwa la Sahara na hutumika kwenye biashara ndogo ndogo kama migahawa, uokaji, biashara za mamantilie, utengenezaji wa matofali, pamoja na ukaushaji wa mazao kama chai na tumbaku.  Zaidi ya 90% ya wakazi kusini mwa Jangwa la Sahara inategemea ama kuni au mkaa.  Nishati ya miti huchangia yapata 90% ya nishati ya miti nchini Tanzania.  Mkaa unatumika zaidi mijini wakati kuni hutumika zaidi vijijini. Yapata 70% ya kaya za mijini hutegemea mkaa.  Afrika huzalisha 62% ya mkaa wote duniani ambao unakisiwa kufikia tani milioni 52.  Tanzania inashika nafasi ya saba kwa uzalishaji wa mkaa duniani, ikichangia kama 3% ya uzalishaji wa mkaa wote duniani, kwa kiasi cha zaidi ya tani 1.6.
  • Item
    Mwongozo wa kuandaa maandiko ya mradi na utaratibu wa kutoa ruzuku
    (Wizara ya Mali asili na Utalii, 2013-03-13) Wizara ya Mali asili na Utalii, T
    Mwongozo huu ni tafsiri ya toleo la Kiingereza la Mwaka 2012. Mfuko wa Misitu Tanzania umetayarisha Mwongozo wa kuandaa maandiko ya Miradi na Utaratibu wa Kutoa Ruzuku ikiwa ni jitihada ya kuepuka upendeleo, kuwa na uwazi na ufanisi katika kazi zake. Ni dhahiri kuwa Taasisi zenye sera na utaratibu ulio wazi wa kuitisha maombi ya ruzuku kwa ajili ya kutekelezea miradi na kusimamia ruzuku hiyo zinaheshimika kwa uwazi huo na uadilifu. Aidha, kuwa na utaratibu sanifu kunasaidia kudumisha mawasiliano muhimu kati ya waombaji wa ruzuku na waliopatiwa ruzuku hiyo.