Nguvu kazi, mitizamo juu ya hali ya hewa na udongo kwenye maeneo ya umwagiliaji yaliyopo Siipow nchini Kenya na Engaruka nchini Tanzania
Loading...
Date
2015
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Department of Human Geography - University of Stockholm
Abstract
Kijitabu hiki kinatoa matokeo ya mradi wa miaka 4 (2011-2015) yaliyofanywa na wanajiografia wanne kutoka chuo kikuu cha Stockholm. Utafiti huu ulifanyika katika vijiji vidogo viwili, ambavyo ni Siipow nchini Kenya na Engaruka nchiniTanzania. Kwa ujumla mradi huu uliangalia vitu vikuu vitatu: udongo, hali ya hewa na nguvu kazi. Mambo haya makuu yanaweza kuonyesha aina ya mabadiliko yaliyowahi kujitokeza katika mifumo ya umwagiliaji katika maeneo haya na sababu mahususi zilizosababisha mabadiliko hayo. Katika kijitabu hiki matokeo ya utafiti yameonyeshwa kufuatana na maeneo ya utafiti na hususani: mbinu za kilimo, mgawanyo wa majukumu ya kazi kwa wanawake na wanaume, sifa za udongo na maji, mabadiliko ya hali ya hewa na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na jinsi ambavyo mambo haya yote kwa ujumla yamekuwa yakibadilika kadri muda unavyokwenda.
Description
Keywords
Hali ya hewa, Mazingira, Udongo, Nguvu kazi, Kilimo, Maji