Majaribio kuhusu uhifadhi wa nafaka kijiji cha Mlali

Loading...
Thumbnail Image

Date

2014

Authors

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Wizara ya Kilimo na Chakula, Tanzania

Abstract

Wakulima wengi Tanzania wanapata hasara kubwa inayosababishwa na wadudu waharibifu wa mazao yanapohifadhiwa kwenye maghala. Uharibifu huu unatishia uhakika wa chakula kwa kaya. Kaya zingine zina uwezo wa kununua madawa ya kuulia wadudu, lakini madawa haya yana gharama kubwa na yaweza kuwa na madhara kwa afya zao, (na kama yakiwa yameharibika huwa hayafai kwa matumizi). Mradi huu umebuniwa kutafiti ubunifu kwa ajili ya wakulima kuhusu matumizi ya madawa asilia ya “diatomaceous earths” (vumbivumbi linalotokana na masalia ya zamani ya viumbe wa majini), katika kuhifadhi mazao kama njia mbadala vijijini. Kwa njia hiyo watafiti watawajibika kwanza kufanya majaribio na kulinganisha uwezo wa madawa mbalimbali katika zoezi zima la kudhibiti wadudu waharibifu wa nafaka, ziwapo ghalani. Awali, majaribio haya linganifu yatafanywa kwa kipindi cha miezi 8 kuendana na msimu wa kuhifadhi mazao, kuanzia Julai 2002 hadi Machi 2003.

Description

Keywords

Mahindi, Hifadhi, Mlali, Tanzania

Citation