Kilimo bora cha alizeti
Loading...
Date
2021-05-12
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Sokoine University of Agriculture
Abstract
Alizeti hutambulika kitaalamu Kama Helianthus Annus na hulimwa kwa wingi karibu maeneo
yote nchini Tanzania katika nyanda za kaskazini, kati, mashariki pamoja na nyanda za juu kusini
hasa katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya,
Arusha, Manyara na Rukwa. Hii inatokana na uwezo wa alizeti kustawi vizuri katika mazingira
mengi tofauti bila ya kuwa na utofauti mkubwa katika uzalishaji wake. Vilevile ni zao ambalo
halihitaji mbembejeo za gharama sana ukilinganisha mazao mengine kama mahindi, ngano, n.k.
Asili ya zao hili ni nchini Marekani ambako lilienea katika maeneo ya Ulaya na baadae
kusambaa sehemu nyingine za dunia ambapo kwa sasa Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa
uzalishaji wa alizeti nyuma ya Afrika ya kusini
Description
Keywords
Alizeti, Mbegu, Kiikolojia