Mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji: Mbinu ya mapinduzi ya kijani wilayani Mbarali, Mbeya
Loading...
Date
2014-10
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
EcoAgriculture
Abstract
Nchini Tanzania, mpango wa matumizi bora ya ardhi vijijini
ulirasimishwa miaka ya hivi karibuni ikiwa ni moja ya mikakati
katika mchakato wa kuleta maendeleo endelevu vijijini.
Utekelezaji wa mpango huu hauna budi kuwa mikononi
mwa wanavijiji wenyewe kwa kiasi kikubwa katika kugawa
ardhi yao kwa matumizi mbalimbali ya kujikimu kimaisha
kwa sasa na siku za baadaye na kuwa na uhifadhi endelevu
wa mazingira. Maendeleo endelevu katika Wilaya ya Mbarali
mkoani Mbeya yanaathiriwa na migogoro ya matumizi ya
rasilimali ardhi na maji kwa muda mrefu sasa. Hii imetokana
na uwezo wa ardhi kupungua kutoa mavuno ya kutosha
na uhaba wa maji kwa matumizi mbalimbali hususan
umwagiliaji, unyweshaji mifugo, uendelevu wa miminiko
la maji kwenye bwawa la umeme, uhifadhi ya bionuai
na mazingira. Mpango wa matumizi bora ya ardhi vijijini
unasaidia kusimamia na utatuzi wa migogoro ya matumizi
ya ardhi, maji na hifadhi ya mazingira.
Description
Keywords
Kilimo Salama, Kilimo Mazingira, Hifadhi ya mazingira, Ardhi