BRICS: Mkakati mbadala wa ushirikiano wa kimaendeleo?

Loading...
Thumbnail Image

Date

2014

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Policy Forum

Abstract

Mandhari ya hali halisi ya ushirikiano wa kimaendeleo inabadilika huku kukiwa na ongezeko la washirika wapya ambao ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, unaojulikana kwa pamoja kama BRICS . Washirika hawa wapya ambao wanawakilisha fursa mpya, rasilimali mpya na makubaliano mapya ya mikataba; huku mkazo mkubwa zaidi ukilenga katika mwelekeo thabiti wa ukuaji wa kiuchumi, kupunguza umaskini na kupata maendeleo ndivyo vinavyoleta changamoto kwa mashirika ya kimaendeleo na wajasiriamali wa nchi za magharibi. Utafiti huu unatokana na kusoma vitabu pamoja na nyaraka mbalimbali za kitaalam, unachangia katika uchambuzi wa maslahi ya sasa ya BRICS kwa Tanzania kwa upande mmoja, (na maslahi ya Tanzania-kwa nchi hizi-kwa upande mwingine), kwa kutoa mtazamo wa kuongeza maarifa na ufahamu wa nafasi ya BRICS na, faida na athari zake kwa Tanzania.

Description

Keywords

Uchumi, Ushirikiano, Maendeleo, Tanzania

Citation