Killimo cha viazi vitamu

Loading...
Thumbnail Image

Date

2023-03-14

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

chuo kikuu cha kilimo cha sokoine

Abstract

Viazi vitamu ni zao mojawapo muhimu la chakula na lishe bora nchini Tanzania. Viazi vitamu vina wanga mwingi hivyo ni njia rahisi ya kuupatia mwili nguvu. Majani ya viazi vitamu yanatumika kama mboga na kuupatia mwili vitamini na madini. Pia viazi vitamu ni chanzo cha kipato. Hata hivyo, wastani wa uzalishaji shambani ni mdogo kiasi cha 5.6t/ha ukilinganisha na uzalishaji unaoweza kufikiwa wa 20–40t/ha. Soko la viazi vitamu sio maalum, kuna wauzaji wadogo na wakubwa. Aina za Viazi Vitamu Asilimia kubwa ya viazi vitamu vinavyolimwa nchini ni vyeupe, maziwa au zambarau, pia za kuna viazi vya rangi ya karoti ambavyo vina virutubisho vyenye vitamin A kwa wingi. Aina viazi zilizoboreshwa ni Simama, Ukerewe, Sinia, Jitihada, Vumilia, Mvuno, Mataya, Polyster na NASPOT-1. Aina hizi zina uwezo wa kutoa kati ya tani 10 mpaka 30 kwa hektari hukomaa kati ya miezi minne hadi mitano na zina unga mwingi.

Description

Keywords

kilimo, viazi vitamu, mseto

Citation

Collections